Ulinzi na Usalama - Polisi Wanaposhindwa Kutimiza Wajibu Wao

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Katiba yetu inatamka wazi kuwa jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi. Lakini tunapotimiza jukumu hili la msingi, tumegawana majukumu.

1. Mwananchi anatakiwa kuhakikisha anampa Polisi nyenzo za kupambana na uhalifu. Mwananchi huyu anampa nyenzo Polisi kupitia Serikali kwa njia ya kodi anayoitoa. Zaidi ya yote, mwananchi anatakiwa kutengeneza mazingira rafiki ya polisi kufanya kazi yao kiurahisi kwa njia ya kutoa taarifa za kufichua uovu, na wakati fulani kutoa msaada wa dharula na mahitaji kwa Polisi kama ikilazimu, hasa pale ambapo vyombo vya Serikali vinaweza kuwa mbali, na hitaji ni la haraka.

2) Serikali kama mkono wa wananchi, inampa askari polisi mafunzo, silaha, mavazi, magari, na zana nyingine zote. Serikali ndiyo inayotakiwa kuhakikisha inawaajiri Polisi wenye maadili, uwezo wa kufanya kazi, na pia kuwafukuza mara moja Polisi wahalifu au kuwapa adhabu nyinginezo.

3) Askari Polisi wanatakiwa kuwa watiifu kwa mwajiri wao mkuu, ambaye ni mwananchi, maana huyu ndiye anayemlipa mshahara, ndiye anayemnunulia hata suruali aliyoivaa, ndiye aliyemnunulia na bunduki, ndiye aliyemjengea nyumba na ofisi, ndiye aliyemnunulia gari, na mahitaji mengine yote.

USALITI MKUBWA

Kuna wasaliti wakubwa watatu katika kutimiza jukumu hili la msingi.la Ulinzi na Usalama:

1) Polisi Wenyewe - kuna matukio mengi, tena yenye ushahidi wa kutosha, ambapo Polisi wamekuwa wakiwaua waajiri wao wanaowalipa mishahara na kuwapa mahitaji yao yote. Mifano, ipo (wafanyabiashara wa madini ya ruby, mfanyabiashara wa madini huko Lindi, n.k.). Kuna matukio Polisi wamewahi kuwateka, kuwapoteza, kuwaua na kuwabambikia waajiri wao kesi za uwongo. Uthibitisho upo mpaka kwenye hotuba ya Rais Samia alipowataka Polisi wajirekebishe kwa sababu kuna mahabusu wanauawa kwenye mahabusu za Polisi, na **** malalamiko ya wananchi kubambikiwa kesi. Mwajiriwa Polisi amepewa haki ya Kisheria, hata ya kumkamata na kumwadhibu mwajiri mhalifu (mwananchi), lakini kumtengenezea uhalifu na kisha kumfungulia mashtaka au kumwua, ni uhalifu wa hali ya juu mwa mwajiriwa dhidi ya mwajiri wake. Mfanyakazi huyu Polisi anayemwua, kumteka au kumfungulia mwajiri wake kesi bandia, mwajiri wake ambaye hajafanya kosa lolote, ni adhabu gani imfaayo?

2) Serikali - Serikali imekuwa ndiyo mkono wa mwananchi kuhusiana na huyu mfanyakazi aitwaye Polisi. Serikali ambayo ni chombo cha mwananchi kuhusiana na kazi ya Polisi, mara kadhaa imemwelekeza mfanyakazi Polisi kutenda uovu dhidi ya mwajiri wake mkuu, mwananchi. Mara ngapi Polisi wametumiwa na Serikali dhidi ya wananchi wanaotaka Serikali iwajibike? Ni mara ngapi, maagizo ya Serikali kwa Polisi, yamesababisha vifo vya wananchi wasio na hatia? Serikali inayomtumia vibaya Polisi, na kumlazimisha Polisi atende uovu dhidi ya mwananchi ambaye hana hatia, na ndiye mwajiri wake yeye Serikalo na Polisi, inayemwamuru atende uovu, ni adhabu gani iifaayo Serikali ya namna hiyo?

2) CCM - msaliti mwingine mkubwa kuhusiana na utendaji kazi wa Polisi ni CCM. CCM mara kadhaa imelitumia Jeshi la Polisi, kuwafanyia uharamia vyama vya upinzani, wanachama wa vyama vya upinzani, wananchi wanaoikosoa CCM na Serikali yake, wananchi wanaotaka kuzuia uibwaji wa kura wakati wa uchaguzi. Mifano ni dhahiri, Jakaya Kikwete, alipokuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM aliwahi kuwasuta viongozi wenzie wa CCM na wanachama, akawauliza, "mnataka wapinzani wakisema CCM haijafanya kitu, nipeleke Polisi? Kwa nini tutegemee Polisi badala ya kujibu hoja?" Kuna ulevi mkubwa wa uovu kwa CCM, wa kuona Jeshi la Polisi, TISS, hata JWTZ, ni mali ya CCM. Kwaajili ya matakwa ya CCM, kwaajili ya kuitetea CCM inapokuwa imeshindwa kwenye majukwaa ya siasa, Polisi, directly or indirectly imewahi kuwaangamiza wananchi. Mpinzani wa CCM, Mawazo, Ben Sanane, mtangazaji huru wa habari Mwangosi, wote kupoteza kwao.

Ni dhahiri kunahusishwa na CCM kushindwa kwenye siasa za majukwaani. Kufungwa kwa viongozi mbalimbali wa CHADEMA, CUF, kote kunahusishwa na dhamira na mbinu chafu zilizofanywa na Polisi na mahakama kwaajili ya manufaa na matakwa ya CCM. Chama ambacho kipo tayari kuona wananchi wanatekwa, wanafungwa bila makosa, wanateswa, wanazuiwa kufanya shuguli za siasa, huku kikitumia jeshi la Polisi na mahakama, ili tu kiendelee kushika dola, kinastahili adhabu gani halali?

Uhalifu unaendelea sasa, ikiwa ni pamoja na PANYA ROAD, kwa kiasi kikubwa kuna mchango wa JESHI LA POLISI, SERIKALI na CCM.

Ni vigumu sana kwa Polisi kupata ushirikiano mzuri na wa uhakika kwa 100% toka kwa wananchi, kutokana na chombo hiki kukosa kuaminika kwa wananchi.

Ni kiongozi gani, ni mwanachama gani wa chama cha upinzani anaweza kwenda Polisi bila ya mashaka, kwenda kutoa taarifa ya uwezekano wa kutokea uhalifu?

Hivi ndugu na wanafamilia wa Azory Gwanda, wanaweza kwenda Polisi kutoa taarifa juu ya uovu wanaoufahamu au waliosikia, huku wakijua kabisa ndugu yao alichukuliwa na watu waliojitambulisha ni Polisi, na ndio ukawa mwisho wa kuonekana ndugu yao?

Hivi Mbowe anaweza kwenda kutoa taarifa ya uhalifu aliousikia kwa Kingai, Mahita, Goodluck au Jumanne?

Hivi wale wananchi ambao walikuwa wanamiliki maduka ya kubadilishia fedha ambao pesa zao ziliporwa kwa mtutu wa bunduki za Polisi, wanaweza kwenda kutoa taarifa Polisi zinazohusiana na uhalifu?

Wale wafanyabiashara waliokamatwa na polisi kisha kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi, wakasotishwa miaka Segerea, kisha pesa yao kuporwa na kuingizwa kwenye mifuko binafsi ya watawala (CAG ameweka wazi kabisa kuwa pesa hiyo haikuingia Setikalini), wanaweza kuwa na imani hata ya ukubwa wa chembe ya haradali kwa Jeshi la Polisi, Serikali na Mahakama?

Mazingira ya uovu ya Serikali, Polisi, Mahakama, Bunge, vyote kwa pamoja yanatengeneza mazingira rafiki kwa uhalifu. Bahati mbaya zaidi, hali hii, mwisho wa yote, anayeumia kuliko wote ni mwananchi. Tupiganie katiba mpya itakayowezesha kila mtu na kila taasisi kutimiza wajibu wake, kila mmoja akitambua, aliye mkubwa kuliko wote ni umma wa Watanzania, siyo CCM, siyo Rais, siyo Polisi, siyo TISS.

Kumtaka mwananchi kuwa sungusungu, afanye kazi ya ulinzi, ni tafsiri potofu ya juu ya kila mwananchi kushiriki kwenye ulinzi na usalama wa Taifa. Wote tunashiriki kwenye ulinzi na usalama wa Taifa, lakini kwa namna tofauti. Kama wote tutageuka kuwa Sungusungu, nani atazalisha pesa ya kuweza kumnunukia polisi silaha, gari, mafuta, n.k? Nani atamtibu mtoto na askari akiumia? Nani atawafundisha watoto watakaokuja kuwa polisi wa baadaye? Hivi tunatarajia daktari aliyekesha usiku kufanya kazi ya ulinzi, kesho ataweza kumtibu vizuri mgonjwa?

Wote ni walinzi wa Taifa letu na wananchi wake, lakini kila mmoja katika kutimiza hilo ana wajibu wake. Polisi watimize wajibu wao, na wananchi tutimize wajibu wetu wa kuwawezesha Polisi kufanya kazi kwa weledi.
 
Mkuu, umeanza vizuri hapo mwanzo lakini umeharibu katika mwendelezo. Suala la kitaaluma linahitaji fikra pevu na ukomavu wa mawazo, hoja na rai. Hekima kubwa, busara pamoja na maarifa hujenga hoja mujarabu.
Jitahidi kujiweka mbali na mawazo mgando, mahaba na hisia binafsi za kisiasa (prejudiced and unreasonable conclusions) unapofanya professional analysis ya mambo muhimu.
 
Katiba yetu inatamka wazi kuwa jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi. Lakini tunapotimiza jukumu hili la msingi, tumegawana majukumu.

1. Mwananchi anatakiwa kuhakikisha anampa Polisi nyenzo za kupambana na uhalifu. Mwananchi huyu anampa nyenzo Polisi kupitia Serikali kwa njia ya kodi anayoitoa. Zaidi ya yote, mwananchi anatakiwa kutengeneza mazingira rafiki ya polisi kufanya kazi yao kiurahisi kwa njia ya kutoa taarifa za kufichua uovu, na wakati fulani kutoa msaada wa dharula na mahitaji kwa Polisi kama ikilazimu, hasa pale ambapo vyombo vya Serikali vinaweza kuwa mbali, na hitaji ni la haraka.

2) Serikali kama mkono wa wananchi, inampa askari polisi mafunzo, silaha, mavazi, magari, na zana nyingine zote. Serikali ndiyo inayotakiwa kuhakikisha inawaajiri Polisi wenye maadili, uwezo wa kufanya kazi, na pia kuwafukuza mara moja Polisi wahalifu au kuwapa adhabu nyinginezo.

3) Askari Polisi wanatakiwa kuwa watiifu kwa mwajiri wao mkuu, ambaye ni mwananchi, maana huyu ndiye anayemlipa mshahara, ndiye anayemnunulia hata suruali aliyoivaa, ndiye aliyemnunulia na bunduki, ndiye aliyemjengea nyumba na ofisi, ndiye aliyemnunulia gari, na mahitaji mengine yote.

USALITI MKUBWA

Kuna wasaliti wakubwa watatu katika kutimiza jukumu hili la msingi.la Ulinzi na Usalama:

1) Polisi Wenyewe - kuna matukio mengi, tena yenye ushahidi wa kutosha, ambapo Polisi wamekuwa wakiwaua waajiri wao wanaowalipa mishahara na kuwapa mahitaji yao yote. Mifano, ipo (wafanyabiashara wa madini ya ruby, mfanyabiashara wa madini huko Lindi, n.k.). Kuna matukio Polisi wamewahi kuwateka, kuwapoteza, kuwaua na kuwabambikia waajiri wao kesi za uwongo. Uthibitisho upo mpaka kwenye hotuba ya Rais Samia alipowataka Polisi wajirekebishe kwa sababu kuna mahabusu wanauawa kwenye mahabusu za Polisi, na **** malalamiko ya wananchi kubambikiwa kesi. Mwajiriwa Polisi amepewa haki ya Kisheria, hata ya kumkamata na kumwadhibu mwajiri mhalifu (mwananchi), lakini kumtengenezea uhalifu na kisha kumfungulia mashtaka au kumwua, ni uhalifu wa hali ya juu mwa mwajiriwa dhidi ya mwajiri wake. Mfanyakazi huyu Polisi anayemwua, kumteka au kumfungulia mwajiri wake kesi bandia, mwajiri wake ambaye hajafanya kosa lolote, ni adhabu gani imfaayo?

2) Serikali - Serikali imekuwa ndiyo mkono wa mwananchi kuhusiana na huyu mfanyakazi aitwaye Polisi. Serikali ambayo ni chombo cha mwananchi kuhusiana na kazi ya Polisi, mara kadhaa imemwelekeza mfanyakazi Polisi kutenda uovu dhidi ya mwajiri wake mkuu, mwananchi. Mara ngapi Polisi wametumiwa na Serikali dhidi ya wananchi wanaotaka Serikali iwajibike? Ni mara ngapi, maagizo ya Serikali kwa Polisi, yamesababisha vifo vya wananchi wasio na hatia? Serikali inayomtumia vibaya Polisi, na kumlazimisha Polisi atende uovu dhidi ya mwananchi ambaye hana hatia, na ndiye mwajiri wake yeye Serikalo na Polisi, inayemwamuru atende uovu, ni adhabu gani iifaayo Serikali ya namna hiyo?

2) CCM - msaliti mwingine mkubwa kuhusiana na utendaji kazi wa Polisi ni CCM. CCM mara kadhaa imelitumia Jeshi la Polisi, kuwafanyia uharamia vyama vya upinzani, wanachama wa vyama vya upinzani, wananchi wanaoikosoa CCM na Serikali yake, wananchi wanaotaka kuzuia uibwaji wa kura wakati wa uchaguzi. Mifano ni dhahiri, Jakaya Kikwete, alipokuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM aliwahi kuwasuta viongozi wenzie wa CCM na wanachama, akawauliza, "mnataka wapinzani wakisema CCM haijafanya kitu, nipeleke Polisi? Kwa nini tutegemee Polisi badala ya kujibu hoja?" Kuna ulevi mkubwa wa uovu kwa CCM, wa kuona Jeshi la Polisi, TISS, hata JWTZ, ni mali ya CCM. Kwaajili ya matakwa ya CCM, kwaajili ya kuitetea CCM inapokuwa imeshindwa kwenye majukwaa ya siasa, Polisi, directly or indirectly imewahi kuwaangamiza wananchi. Mpinzani wa CCM, Mawazo, Ben Sanane, mtangazaji huru wa habari Mwangosi, wote kupoteza kwao
ni dhahiri kunahusishwa na CCM kushindwa kwenye siasa za majukwaani. Kufungwa kwa viongozi mbalimbali wa CHADEMA, CUF, kote kunahusishwa na dhamira na mbinu chafu zilizofanywa na Polisi na mahakama kwaajili ya manufaa na matakwa ya CCM. Chama ambacho kipo tayari kuona wananchi wanatekwa, wanafungwa bila makosa, wanateswa, wanazuiwa kufanya shuguli za siasa, huku kikitumia jeshi la Polisi na mahakama, ili tu kiendelee kushika dola, kinastahili adhabu gani halali?

Uhalifu unaendelea sasa, ikiwa ni pamoja na PANYA ROAD, kwa kiasi kikubwa kuna mchango wa JESHI LA POLISI, SERIKALI na CCM.

Ni vigumu sana kwa Polisi kupata ushirikiano mzuri na wa uhakika kwa 100% toka kwa wananchi, kutokana na chombo hiki kukosa kuaminika kwa wananchi.

Ni kiongozi gani, ni mwanachama gani wa chama cha upinzani anaweza kwenda Polisi bila ya mashaka, kwenda kutoa taarifa ya uwezekano wa kutokea uhalifu?

Hivi ndugu na wanafamilia wa Azory Gwanda, wanaweza kwenda Polisi kutoa taarifa juu ya uovu wanaoufahamu au waliosikia, huku wakijua kabisa ndugu yao alichukuliwa na watu waliojitambulisha ni Polisi, na ndio ukawa mwisho wa kuonekana ndugu yao?

Hivi Mbowe anaweza kwenda kutoa taarifa ya uhalifu aliousikia kwa Kingai, Mahita, Goodluck au Jumanne?

Hivi wale wananchi ambao walikuwa wanamiliki maduka ya kubadilishia fedha ambao pesa zao ziliporwa kwa mtutu wa bunduki za Polisi, wanaweza kwenda kutoa taarifa Polisi zinazohusiana na uhalifu?

Wale wafanyabiashara waliokamatwa na polisi kisha kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi, wakasotishwa miaka Segerea, kisha pesa yao kuporwa na kuingizwa kwenye mifuko binafsi ya watawala (CAG ameweka wazi kabisa kuwa pesa hiyo haikuingia Setikalini), wanaweza kuwa na imani hata ya ukubwa wa chembe ya haradali kwa Jeshi la Polisi, Serikali na Mahakama?

Mazingira ya uovu ya Serikali, Polisi, Mahakama, Bunge, vyote kwa pamoja yanatengeneza mazingira rafiki kwa uhalifu. Bahati mbaya zaidi, hali hii, mwisho wa yote, anayeumia kuliko wote ni mwananchi. Tupiganie katiba mpya itakayowezesha kila mtu na kila taasisi kutimiza wajibu wake, kila mmoja akitambua, aliye mkubwa kuliko wote ni umma wa Watanzania, siyo CCM, siyo Rais, siyo Polisi, siyo TISS.

Kumtaka mwananchi kuwa sungusungu, afanye kazi ya ulinzi, ni tafsiri potofu ya juu ya kila mwananchi kushiriki kwenye ulinzi na usalama wa Taifa. Wote tunashiriki kwenye ulinzi na usalama wa Taifa, lakini kwa namna tofauti. Kama wote tutageuka kuwa Sungusungu, nani atazalisha pesa ya kuweza kumnunukia polisi silaha, gari, mafuta, n.k? Nani atamtibu mtoto na askari akiumia? Nani atawafundisha watoto watakaokuja kuwa polisi wa baadaye? Hivi tunatarajia daktari aliyekesha usiku kufanya kazi ya ulinzi, kesho ataweza kumtibu vizuri mgonjwa?

Wote ni walinzi wa Taifa letu na wananchi wake, lakini kila mmoja katika kutimiza hilo ana wajibu wake. Polisi watimize wajibu wao, na wananchi tutimize wajibu wetu wa kuwawezesha Polisi kufanya kazi kwa weledi.
Inapofika wakati wa uchaguzi. Serikali, polisi na ccm ni zaidi ya simba au mbogo.

Baada ya hapo usingizi mnono.
 
Mazingira ya uovu ya Serikali, Polisi, Mahakama, Bunge, vyote kwa pamoja yanatengeneza mazingira rafiki kwa uhalifu. Bahati mbaya zaidi, hali hii, mwisho wa yote, anayeumia kuliko wote ni mwananchi. Tupiganie katiba mpya itakayowezesha kila mtu na kila taasisi kutimiza wajibu wake, kila mmoja akitambua, aliye mkubwa kuliko wote ni umma wa Watanzania, siyo CCM, siyo Rais, siyo Polisi, siyo TISS.
Well said.
 
Sasa wewe ulishaambiwa na waziri wako kuwa watu waliofaulu vizuri yani div 1,2&3 hawana sifa za kuwa askari polisi unategemea hao waliobaki wenye sifa (four na zero) ndo wakuletee positive output kweli!?

Karibu Tanzania nchi pekee duniani ambayo mwenye elimu hana sifa za kuwa mfanya kazi wa serikali, vilaza ndo wana sifa.
Nchi pekee ambayo haijiri wasomi wenye sifa bali inarudisha kazini vilaza waliofeli shule na kugushi vyeti vyao.

Sifa kuu ya kuwa askari Tanzania nikuwa kilaza na mjinga mjinga ili wanasiasa wa siasa za maji taka wakutumie kama mbwa wao kufanikisha udhalimu wao.

Huo ndo ukweli, ukichukia pasuka.
 
Katiba yetu inatamka wazi kuwa jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi. Lakini tunapotimiza jukumu hili la msingi, tumegawana majukumu.

1. Mwananchi anatakiwa kuhakikisha anampa Polisi nyenzo za kupambana na uhalifu. Mwananchi huyu anampa nyenzo Polisi kupitia Serikali kwa njia ya kodi anayoitoa. Zaidi ya yote, mwananchi anatakiwa kutengeneza mazingira rafiki ya polisi kufanya kazi yao kiurahisi kwa njia ya kutoa taarifa za kufichua uovu, na wakati fulani kutoa msaada wa dharula na mahitaji kwa Polisi kama ikilazimu, hasa pale ambapo vyombo vya Serikali vinaweza kuwa mbali, na hitaji ni la haraka.

2) Serikali kama mkono wa wananchi, inampa askari polisi mafunzo, silaha, mavazi, magari, na zana nyingine zote. Serikali ndiyo inayotakiwa kuhakikisha inawaajiri Polisi wenye maadili, uwezo wa kufanya kazi, na pia kuwafukuza mara moja Polisi wahalifu au kuwapa adhabu nyinginezo.

3) Askari Polisi wanatakiwa kuwa watiifu kwa mwajiri wao mkuu, ambaye ni mwananchi, maana huyu ndiye anayemlipa mshahara, ndiye anayemnunulia hata suruali aliyoivaa, ndiye aliyemnunulia na bunduki, ndiye aliyemjengea nyumba na ofisi, ndiye aliyemnunulia gari, na mahitaji mengine yote.

USALITI MKUBWA

Kuna wasaliti wakubwa watatu katika kutimiza jukumu hili la msingi.la Ulinzi na Usalama:

1) Polisi Wenyewe - kuna matukio mengi, tena yenye ushahidi wa kutosha, ambapo Polisi wamekuwa wakiwaua waajiri wao wanaowalipa mishahara na kuwapa mahitaji yao yote. Mifano, ipo (wafanyabiashara wa madini ya ruby, mfanyabiashara wa madini huko Lindi, n.k.). Kuna matukio Polisi wamewahi kuwateka, kuwapoteza, kuwaua na kuwabambikia waajiri wao kesi za uwongo. Uthibitisho upo mpaka kwenye hotuba ya Rais Samia alipowataka Polisi wajirekebishe kwa sababu kuna mahabusu wanauawa kwenye mahabusu za Polisi, na **** malalamiko ya wananchi kubambikiwa kesi. Mwajiriwa Polisi amepewa haki ya Kisheria, hata ya kumkamata na kumwadhibu mwajiri mhalifu (mwananchi), lakini kumtengenezea uhalifu na kisha kumfungulia mashtaka au kumwua, ni uhalifu wa hali ya juu mwa mwajiriwa dhidi ya mwajiri wake. Mfanyakazi huyu Polisi anayemwua, kumteka au kumfungulia mwajiri wake kesi bandia, mwajiri wake ambaye hajafanya kosa lolote, ni adhabu gani imfaayo?

2) Serikali - Serikali imekuwa ndiyo mkono wa mwananchi kuhusiana na huyu mfanyakazi aitwaye Polisi. Serikali ambayo ni chombo cha mwananchi kuhusiana na kazi ya Polisi, mara kadhaa imemwelekeza mfanyakazi Polisi kutenda uovu dhidi ya mwajiri wake mkuu, mwananchi. Mara ngapi Polisi wametumiwa na Serikali dhidi ya wananchi wanaotaka Serikali iwajibike? Ni mara ngapi, maagizo ya Serikali kwa Polisi, yamesababisha vifo vya wananchi wasio na hatia? Serikali inayomtumia vibaya Polisi, na kumlazimisha Polisi atende uovu dhidi ya mwananchi ambaye hana hatia, na ndiye mwajiri wake yeye Serikalo na Polisi, inayemwamuru atende uovu, ni adhabu gani iifaayo Serikali ya namna hiyo?

2) CCM - msaliti mwingine mkubwa kuhusiana na utendaji kazi wa Polisi ni CCM. CCM mara kadhaa imelitumia Jeshi la Polisi, kuwafanyia uharamia vyama vya upinzani, wanachama wa vyama vya upinzani, wananchi wanaoikosoa CCM na Serikali yake, wananchi wanaotaka kuzuia uibwaji wa kura wakati wa uchaguzi. Mifano ni dhahiri, Jakaya Kikwete, alipokuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM aliwahi kuwasuta viongozi wenzie wa CCM na wanachama, akawauliza, "mnataka wapinzani wakisema CCM haijafanya kitu, nipeleke Polisi? Kwa nini tutegemee Polisi badala ya kujibu hoja?" Kuna ulevi mkubwa wa uovu kwa CCM, wa kuona Jeshi la Polisi, TISS, hata JWTZ, ni mali ya CCM. Kwaajili ya matakwa ya CCM, kwaajili ya kuitetea CCM inapokuwa imeshindwa kwenye majukwaa ya siasa, Polisi, directly or indirectly imewahi kuwaangamiza wananchi. Mpinzani wa CCM, Mawazo, Ben Sanane, mtangazaji huru wa habari Mwangosi, wote kupoteza kwao
ni dhahiri kunahusishwa na CCM kushindwa kwenye siasa za majukwaani. Kufungwa kwa viongozi mbalimbali wa CHADEMA, CUF, kote kunahusishwa na dhamira na mbinu chafu zilizofanywa na Polisi na mahakama kwaajili ya manufaa na matakwa ya CCM. Chama ambacho kipo tayari kuona wananchi wanatekwa, wanafungwa bila makosa, wanateswa, wanazuiwa kufanya shuguli za siasa, huku kikitumia jeshi la Polisi na mahakama, ili tu kiendelee kushika dola, kinastahili adhabu gani halali?

Uhalifu unaendelea sasa, ikiwa ni pamoja na PANYA ROAD, kwa kiasi kikubwa kuna mchango wa JESHI LA POLISI, SERIKALI na CCM.

Ni vigumu sana kwa Polisi kupata ushirikiano mzuri na wa uhakika kwa 100% toka kwa wananchi, kutokana na chombo hiki kukosa kuaminika kwa wananchi.

Ni kiongozi gani, ni mwanachama gani wa chama cha upinzani anaweza kwenda Polisi bila ya mashaka, kwenda kutoa taarifa ya uwezekano wa kutokea uhalifu?

Hivi ndugu na wanafamilia wa Azory Gwanda, wanaweza kwenda Polisi kutoa taarifa juu ya uovu wanaoufahamu au waliosikia, huku wakijua kabisa ndugu yao alichukuliwa na watu waliojitambulisha ni Polisi, na ndio ukawa mwisho wa kuonekana ndugu yao?

Hivi Mbowe anaweza kwenda kutoa taarifa ya uhalifu aliousikia kwa Kingai, Mahita, Goodluck au Jumanne?

Hivi wale wananchi ambao walikuwa wanamiliki maduka ya kubadilishia fedha ambao pesa zao ziliporwa kwa mtutu wa bunduki za Polisi, wanaweza kwenda kutoa taarifa Polisi zinazohusiana na uhalifu?

Wale wafanyabiashara waliokamatwa na polisi kisha kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi, wakasotishwa miaka Segerea, kisha pesa yao kuporwa na kuingizwa kwenye mifuko binafsi ya watawala (CAG ameweka wazi kabisa kuwa pesa hiyo haikuingia Setikalini), wanaweza kuwa na imani hata ya ukubwa wa chembe ya haradali kwa Jeshi la Polisi, Serikali na Mahakama?

Mazingira ya uovu ya Serikali, Polisi, Mahakama, Bunge, vyote kwa pamoja yanatengeneza mazingira rafiki kwa uhalifu. Bahati mbaya zaidi, hali hii, mwisho wa yote, anayeumia kuliko wote ni mwananchi. Tupiganie katiba mpya itakayowezesha kila mtu na kila taasisi kutimiza wajibu wake, kila mmoja akitambua, aliye mkubwa kuliko wote ni umma wa Watanzania, siyo CCM, siyo Rais, siyo Polisi, siyo TISS.

Kumtaka mwananchi kuwa sungusungu, afanye kazi ya ulinzi, ni tafsiri potofu ya juu ya kila mwananchi kushiriki kwenye ulinzi na usalama wa Taifa. Wote tunashiriki kwenye ulinzi na usalama wa Taifa, lakini kwa namna tofauti. Kama wote tutageuka kuwa Sungusungu, nani atazalisha pesa ya kuweza kumnunukia polisi silaha, gari, mafuta, n.k? Nani atamtibu mtoto na askari akiumia? Nani atawafundisha watoto watakaokuja kuwa polisi wa baadaye? Hivi tunatarajia daktari aliyekesha usiku kufanya kazi ya ulinzi, kesho ataweza kumtibu vizuri mgonjwa?

Wote ni walinzi wa Taifa letu na wananchi wake, lakini kila mmoja katika kutimiza hilo ana wajibu wake. Polisi watimize wajibu wao, na wananchi tutimize wajibu wetu wa kuwawezesha Polisi kufanya kazi kwa weledi.
Wako busy na CHADEMA
 
Wenye akili hawana vyeo, na wenye Vyeo hawana Akili....

Na wenye Akili ukiwapa vyeo wanajitoa akili wanakuwa hawana akili...

Isomeke kama ilivyoandikwa.
 
Back
Top Bottom