Ulimwengu wetu wa Leo:mabadiliko ya sayansi na teknolojia yameleta amani na furaha?

forumyangu

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
2,150
2,000
Habari zenu Ndugu Katika bwana,Aslam alyekum Ndugu.Binadam tangu mwanzo amepitia Vipindi mbalimbali vya maendeleo kulikuwa na Zama za mawe(mwanzo,kati,mwisho)Katika Vipindi hivi binadam alitumia mawe kufanyia shughuli mbalimbali,kikaja kipindi cha zama za chuma,Mara baada ya binadam kugunduwa chuma basi ilikuwa ni hatua muhimu sana katika maisha yake.Alitumia zana za chuma kulimia,kuwindia,kuulia wanyama.Baada ya hapo kikaja kipindi cha zama za sayansi na teknolojia hapa binadamu katika historia amefanya mageuzi makubwa sana katika kuyatawala mazingira yake.Kiumbe huyu anajaribu kugundua/kubuni njia mbalimbali za kumwezesha kuishi na kuyaelewa mazingira yake.
Je,
Mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanamuweza kiumbe huyu kuishi kwa amani na furaha?

Kama kila mmoja wetu akiulizwa swali hili atakuwa na majibu yake na sababu zake.Hivyo nami najibu swali hili kutokana na sababu zangu....
Ni kweli maendeleo ya elimu yanaduwaza sana.Binadamu wanafanya mambo Yale ambayo kipindi cha nyuma yalionekana yasiyowezekana kabisa.Binadamu anajaribu kufanya majaribio mbalimbali mfano jaribio la kupandikiza ubongo katika kichwa kingine(Transplantation).Uvumbuzi uliofanywa karne mbili zilizopita Ndege Ulaya(19o3),Aeroplane aina ya jet(1931),Simu ya mdomo telephone 1876 n.k.
Maendeleo makubwa katika ubingwa wa kupandikiza viungo yamefanya miili ya waliokufa sasa hivi kuwa kama akiba/banki ya viungo vya mwili.Figo,Ini na mfano wa hivyo huondolewa katika mwili wa mtu wakati huo huo anapokufa na kupandikizwa kama mbegu katika mwili wa mgonjwa hai wa viungo hivyo ili kumuwezesha kuendelea kuishi(Transplantation).

Ugunduzi vyombo mbalimbali vya angani.Fikiria ile darubini iitwayo"Hubble space Telescope.Darubini hii ina uwezo wa kuchukuwa picha duniani hata ya panya mdogo anayetambaa umbali wa km 711!.Hubble space Telescope hufungwa pamoja na satellite inayoenda angani.Satellite hiyo inazunguka dunia yetu katika urefu wa 595 kwenda juu.

Mabaharia waliofutana na Ferdinand Magellan ambaye alikuwa mtu Wa kwanza kuizunguka dunia kwa njia ya bahari,walitumia miaka mitatu(1519-1522) kumaliza mizunguko hiyo.Lakini siku hizi ndege aina ya Jet huchukuwa siku mbili kwa safari hiyo.Wakati wana anga(astronauts) hutumia saa moja na nusu tu kuzunguka dunia!
Ni vigumu sana kutaja kila aina ya maendeleo yaliyopatikana kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo yamebadilisha kabisa maisha ya mwanadamu.

VITA!
Vita baina ya mataifa mbalimbali yameongezeka sana,hivyo kusababisha misukosuko na taabu duniani.
Je,maendeleo haya yote yamemfanya mwanadamu aone raha na furaha moyoni?
Tangu kuisha kwa vita kuu I(1914-1918) sura ya vita imebadilika sana(yote).Kujengwa kwa viwanda vya silaha za kivita kumebadilisha sana sura ya vita,zamani wanajeshi walitumia Farasi kusafiri kwenda kwenye viwanja vya medani pia walitumia silaha duni sana.Lakini miaka hii askari wanaweza kupigana hata angani,manowari/submarine zilipigana bila hata kuonana kwa kutumia rada.Vita vya kwanza inakadiliwa askari waliouwawa walikuwa wengi zaidi kuliko waliouwawa katika vita vyote vya Napoleon katika Urusi.Askari milioni 12 walikufa katika vita vya kwanza,wakati vita vya pili idadi hiyo ilikuwa maradufu(askari+raia+mateka wa vita)inakadiliwa kuwa milioni 57,5.
Tangu kuisha kwa vita hizi mataifa mbalimbali yamejiimarisha katika kutengeneza silaha za maangamizi.Baada ya Marekani kurusha Bomu la Atomic ambalo liliangamiza watu zaidi ya 87521 mwaka 1945.Umoja wa Soviet waliunda kombola la maangamizi la Hydrogen ambaklo lilikuwa na uwezo Mara 4 zaidi ya Marekani.Baada ya maendeleo hayo sasa kila taifa linaboresha uwezo wake kijeshi.Bomu lililoangushwa Hiroshima linaonekana kama kitu cha zamani.

Kama Leo vita ya dunia ikitokea basi mataifa makubwa yataweza kutumia zana nzito na kubwa zenye nguvu zaidi ya Mara 800,000 kuliko Bomu lililotupwa katika miji wa Hiroshima.Submarine moja tu yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia inaweza kuangamiza mija zaidi ya 245.
Silaha hizi za nyuklia ambazo hutoa joto Kali na miale ya sumu aina ya radium (madini yanayotoa nuru na nguvu za umeme) kama zitatumika katika vita vya nyuklia,basi itakuwa ndiyo mwisho kabisa wa wanadamu wote ulimwenguni.

Nakumbuka miaka michache aliyopita Rais wa urusi aliyeitwa Mikhail Gorbachev alisema"Wanadamu wamekaribia sana ule mpaka ambao tikiupita hatutaweza kurudi tena.Mpaka inaonyesha tumeukaribia Kuna kila dalili zanaonyesha.
Je kwa mtazamo wako unadhani;Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaleta amani na furaha duniani?
Karibuni
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,853
2,000
Kuna muda yameleta amani na furaha LAKINI pia kuna muda mwingine yameleta majanga tupu balaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom