Popomtata
Member
- Dec 20, 2011
- 63
- 10
Natumia Smart TV ambapo humo ndani kama nikitaka kufanya mirroring kuna teknolojia ya Intel®wireless display, ambapo unaweza kuunganisha devices nyingine kama Laptop, tablet, na smartphone: Kwa mujibu wa huduma hiyo unaweza kufanya mirroring kutoka kwa vifaa vyenye Intel widi kama laptop ama kwa smartphone zenye huduma ya WiFi direct pia ni rafiki kwa huduma hiyo! Sasa shida yangu ni kwamba nimejaribu Mara kadhaa kuunganisha smartphone yangu kupitia WiFi direct lakini naishia pale ambapo screen ya TV inaponiandia "enter the following security code" harafu chini ya maelekezo hayo kuna kijimstatili ndani yake kuna maneno yanasomeka "PUSH-BUT" . Sasa shida ni kwamba hainipi code ili niweze kujaza kwa smartphone yangu niweze kuwa connected kwa huduma, kila kitu kinaenda sawa tatizo ni jinsi ya kupata hizo security code! Kama kuna MTU ana ujuzi zaidi kwa masuala haya naomba msaada!