Ulimwengu Wa Plastiki Au Dunia Ya Watu.

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,808
3,733
Ulimwengu Wa Plastiki Au Dunia Ya Watu.
1551810998800-png.1038843

Waziri Wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba aliwai kusema “Ndugu zangu sina budi kuwa kumbusha kuwa siku hizi kuna Wakimbizi wa Mazingira, watu wanaharibu mazingira katika maeneo yao na kuhamia maeneo mengine, jitihada za maendeleo zote hazitakuwa na maana kama hatutatunza Mazingira yetu”.

Raisi wa Awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi alisema “Umaskini na uharibifu wa Mazingira ni watoto mapacha na mama yao ni Ujinga.”

Mwanadamu ndio chanzo cha uharibifu wa Mazingira na uharibifu huo unasababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo utupaji wa taka ovyo zikiwemo taka za plastiki.

Plastiki utengenezwa kwa kiasi kikubwa na malighafi aina ya organic polymers. Polyethylene na nylon ni mfano mzuri wa organic polymers. Kauli mbiu ya mazingira ya mwaka 2018 duniani kote ilisema "Kupiga vita uchafuzi wa plastiki" (Beat Plastic Pollution) na kilele cha kuadhimisha siku hiyo ya mazingira kilifanyika nchini India. Huku kauli mbiu ya mazingira mwaka 2018 Nchini Tanzania ikisema "Nitunze Nikutunze" ikilenga kusisitiza utumiaji wa nishati mbadala na watu kuachana na matumizi ya mkaa.

Kwa nini Plastiki? (Tuangalie Historia): Watafiti wanasema kuanzia mwaka 1950 mpaka 1970 asilimia ndogo sana ya plastiki ilikuwa ikizalishwa duniani kote. Kwa sababu hiyo waliweza kusimamia vizuri na kuzuia madhara yatokanayo na plastiki katika mazingira asilia. Lakini kuanzia mwaka 1990 mpaka hivi sasa, uchafu wa plastiki ambao umezalishwa ni mara tatu ya miongo miwili kutoka mwaka 1950 mpaka mwaka 1960 na kutoka mwaka 1960 mpaka mwaka 1970. Watafiti wamekadiria zaidi ya tani bilioni 8.3 za plastiki zimezalishwa kuanzia mwaka 1950 mpaka sasa. Asilimia 60 kati ya hizo zimeishia katika mazingira asilia. Pia kuanzia mwaka 1950 mpaka hivi sasa kiwango cha uzalishaji wa plastiki kimekuwa kwa kiasi kubwa hapa duniani.

Uchafu wa Plastiki kwa sasa umezagaa karibu kila sehemu ya Dunia. Wanasayansi wanaamini kuwa ni zama za Mwanadamu (Anthropocene era) na nimatokeo ya kuongezeka kwa shughuli za mwanadamu katika Dunia. Leo hii Mwanadamu uzalisha Tani milioni 300 za uchafu wa Plastiki kwa mwaka duniani, huku ikikadiriwa kuwa sawa na idadi ya uzito wa watu Duniani. Chupa za Plastiki milioni 1 ununuliwa kila baada ya dakika moja Duniani. Huku mifuko ya Plastiki trilioni 5 utumika mara moja tu kabla ya kutupwa kila mwaka (single-use plastic bags). Huku nusu ya plastiki zote zinazotengenezwa duniani zinatengenezwa kwa madhumuni ya kutumika mara moja tu, Ni Asilimia 9 tu ya uchafu wote wa Plastiki ambao unazalishwa unakuwa recycled. Huku asilimia 12 uchomwa moto, wakati asilimia 79 kati ya hizo ubakia katika mazingira yetu ya asili.

Mito 10 inayobeba zaidi ya asilimia 90 ya uchafu wa plastiki na kupeleka baharini.
1. Chang Jiang (Yangtze River) 1,469,481 tani
2. Indus 164,332 tani
3. Huang He (Yellow River) 124,249 tani
4. Hai He 91,858 tani
5. Nile 84,792 tani
6. Meghna, Brahmaputra, Ganges 72,845 tani
7. Zhujiang (Pearl River) 52,958 tani
8. Amur 38,267 tani
9. Niger 35,196 tani
10. Mekong 33,431 tani

Source: Data from “Export of Plastic Debris by Rivers into the Sea” by Christian Schmidt, Tobias Krauth, and Stephan Wagner, published in Environmental Science & Technology (2017)

Madhara ya Uchafu wa Plastiki katika Mazingira ya Viumbe hai
Uchafu wa plastiki una madhara makubwa sana kwa viumbe hai wote, wakubwa na wadogo. Sumu ipatikanayo kwenye uchafu plastiki kwa mfano Diethylhexyl Phthalate usababisha kansa kwa viumbe hai.
Plastiki inaweza kuharibu mfumo wa chakula na kusababisha vifo kwa samaki na wanyama wakubwa kwa kumeza kimakosa, kwa mfano Kasa (Sea Turtle), Nyangumi na Papa.
Uchafu wa plastiki unapochomwa kama utavuta moshi wake kwa muda mrefu au mara kwa mara, basi kuna uwezekano mkubwa wa kusababisha madhara katika mfumo wa upumuaji na kuharibu utendaji kazi wa mfumo wa Homoni kwa Binadamu. Kemikali aina ya BPA (Bisphenol A) inayopatikana kwenye plastiki uharibu utendaji kazi wa Thyroid Hormone na Sex Hormone kwa Binadamu.

Njia mbadala za kupunguza na kuzuia uchafuzi wa plastiki.
👉
Kutoa elimu na athari za uchafu wa plastiki kwa mazingira.
👉 Kuweka njia nzuri na salama za kurecycle uchafu wa plastiki.
👉 Kuweka faini na sheria za kuzuia aina za bidhaa za plastiki ambazo hutumika mara moja tu na zinamadhara makubwa katika mazingira yetu, mfano mzuri mifuko ya nylon na chupa za plastiki
👉 Kuweka sera ya mazingira ambayo itawabana watengenezaji na watumiaji wa bidhaa za plastiki ambao watakiuka maadili ya utupaji, utengenezaji na uhifadhi wa taka za plastiki.

Mazingira ni yetu sote ni haki yetu tuyalinde, tuyatunze na kuyahifadhi kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadae. Mazingira ni Uhai.
 
Nimeona mito mingi iliyoathirika ni Asia hasa mashariki ya mbali na Asia ya Kati. Hawa wanajali sana hela kuliko mazingira tofauti West Countries ambao wao mazingira na uchumi vinaenda kwenye mzani mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app

Well Said Frank Wanjiru nakubaliana na wewe 100% mkuu lakini naongezea kidogo kuhusu ishu ya population ukiangalia vizuri nchi za bara la Asia zinaidadi kubwa ya watu ukilinganisha na Western Countries (Nchi za Magharibi). Kwa mfano Idadi ya watu wa china 1.4 Billion) + (Idadi ya watu wa India 1.3 Billion) = 2.7 Billion....wakati Dunia nzima total population inakadiriwa kuwa 7.7 Billion. (2.7/7.7 x 100) = 35% ni population ya India na China peke yake out of 100% ya Dunia.
 
Wangepiga marufuku kabisa kwani inauwa mpaka samaki na ni hatari kwa afya zetu pia.
Kuna visiwa vya plastics siku hizi yaani uchafu umejikusanya mpaka umekuwa kisiwa
Niliona clip moja Dubai wametengenezewa robot zinazokusanya plastics.
Kuna nchi zinajitahidi lakini bado wanatumia, yaani ni kutwanga maji tu.

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Ni kweli kabisa mkuu. Plastiki zinamadhara makubwa sana katika mazingira yetu ya asili, tofauti kabisa na watu wanavyochukulia kirahisi kirahisi tu. Hiyo hapo chini ni video clip inayoonyesha aina za plastiki mbalimbali zilizokutwa ndani ya mwili wa Nyangumi (Whale) na Wanasayansi wa University of Bergen, Baada ya kupigwa risasi na watu wa Fire Department waliojaribu kumfukuza kutoka ufukweni. Kila walipojaribu kumfukuza kutoka ufukweni aligoma kuondoka kutokana na kumeza plastiki nyingi sana ndani ya mwili wake, mpaka walipoamua kumpiga risasi kwa ajili ya usalama. Ndipo Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Bergen walipokuja kufanya utafiti wakagundua kumbe alikuwa amemeza kilogramu za plastiki za kutosha.
 
Attachments

  • OCEAN POLLUTION_ This Whale Had A Message From The Deep.mp4
    6.3 MB · Views: 59
Ni kweli kabisa mkuu. Plastiki zinamadhara makubwa sana katika mazingira yetu ya asili, tofauti kabisa na watu wanavyochukulia kirahisi kirahisi tu. Hiyo hapo chini ni video clip inayoonyesha aina za plastiki mbalimbali zilizokutwa ndani ya mwili wa Nyangumi (Whale) na Wanasayansi wa University of Bergen, Baada ya kupigwa risasi na watu wa Fire Department waliojaribu kumfukuza kutoka ufukweni. Kila walipojaribu kumfukuza kutoka ufukweni aligoma kuondoka kutokana na kumeza plastiki nyingi sana ndani ya mwili wake, mpaka walipoamua kumpiga risasi kwa ajili ya usalama. Ndipo Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Bergen walipokuja kufanya utafiti wakagundua kumbe alikuwa amemeza kilogramu za plastiki za kutosha.
Inasikitisha sana, hapo ni viumbe wangapi wanakufa baharini maana hizo plastics mwisho hukatika katika mpaka zinakuwa particles kiasi ambacho kila kiumbe atameza.
Madhara yake mwanadamu hayaoni kama ni mabaya ila ni baadhi ya vikundi ndio wanapigania

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Naangalia RT wanaongelea kuhusu Coca-Cola na uharibifu wao ni hatari kwa kweli wanavyochafua bahari

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Inasikitisha sana, hapo ni viumbe wangapi wanakufa baharini maana hizo plastics mwisho hukatika katika mpaka zinakuwa particles kiasi ambacho kila kiumbe atameza.
Madhara yake mwanadamu hayaoni kama ni mabaya ila ni baadhi ya vikundi ndio wanapigania

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Viumbe wengi wa baharini hivi sasa wakipimwa wanakutwa na kiwango cha plastiki ndani ya miili yao. Kwa sababu ya ocean waves na decomposition processes zinazotokea ndani ya bahari zinafanya Macroplastics (Plastiki kubwa) kuwa disintergrated kwenda kwenye mesoplastics na microplastics. Hizi microplastics ni vipande vya plastiki vidogo vidogo sana ambavyo kwa macho ya kawaida ya mwanadamu vinaweza visionekane. Microplastics zinaingia kwenye miili ya viumbe hai wa majini kwa njia mbalimbali, Kwa mfano samaki zinaingia kwa kupitia matamvua (fish gills) na ingestion process.
 
Na wanakufa wengi sana
Binadamu hatujali na ni wwchache wa kuwasemea hawa viumbe
Nawahurumia sana kwa kweli

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Na wanakufa wengi sana
Binadamu hatujali na ni wwchache wa kuwasemea hawa viumbe
Nawahurumia sana kwa kweli.
Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Ni kweli kabisa mkuu, kwa sasa tupo katika ulimwengu mwingine kabisa kila mtu, shirika, kampuni na taifa linatazama maslahi yake binafsi kwanza na sio madhara yatokanayo na shughuli au uzalishaji wa bidhaa fulani katika mazingira.
 
Aisee makampuni wameanza kubadili straws zimekuwa za karatasi badala ya plastics safi sana

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Uchafuzi wa mazingira kupitia mifuko ya plastiki ni tatizo kubwa sana...

Suluhisho lake ni gumu sana, kwa sababu katika maisha yetu ya kila siku haswa mijini plastic zinatumika na zinahitaji sana...

Cc: mahondaw
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom