Ulimwengu wa giza na uchaguzi wa tanzania

  • Thread starter MWANA WA UFALME
  • Start date

MWANA WA UFALME

MWANA WA UFALME

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2010
Messages
578
Likes
0
Points
0
MWANA WA UFALME

MWANA WA UFALME

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2010
578 0 0
Waumini wanaoadiwa kuwa ni wa imani ya Freemasons inayosemekana inatumia nguvu za giza, mwishoni mwa wiki iliyopita walifanya sherehe ya kufuru nchini ambapo Risasi Mchanganyiko lilifuatilia matukio yote yaliyokuwa yakijiri na hii ndiyo ripoti kamili.

Tukio hilo lililoshuhudiwa hatua kwa hatua na paparazi wetu lilichukua nafasi yake Oktoba 31, siku ya Uchaguzi Mkuu ndani ya jengo maarufu la kibiashara lililopo pembezoni mwa barabara ya Old Bagamoyo Kinondoni jijini Dar.

Paparazi wetu ambaye awali alikuwa hajui chochote, alialikwa kwenye shughuli hiyo na rafiki yake wa karibu (jina tunalo) baada ya kumdanganya ishu inayofanyika.

Paparazi huyo aliingia kwenye hoteli hiyo mida ya saa nne usiku na kushuhudia matukio ya ajabu na kutisha likiwemo watu waliohudhuria sherehe hiyo kuvaa mafuvu ya binadamu na wengine kuonekana kama vinyago.

Ukumbi huo pia ulipambwa kwa mafuvu ya binadamu na sehemu nyingine kulikuwa na popo huku vitambaa vyeusi vikiwa vimezungushwa kuziba eneo kubwa la kuta.

Aidha, katika lango la kuingilia ukumbini humo kulikuwa na bango lenye ujumbe uliosomeka ‘Don’t Mess With Me’ na kwamba baadhi ya masharti yaliyokuwepo ndani ni pamoja na mtu kuvaa vazi lisilofanana na mwenzake.

Ili kuufikia ukumbi huo ilikuwa ni lazima uvuke mapazia matatu mpaka la nne na kuna sehemu kulikuwa na kaunta yenye kuuza tiketi na pembeni yake kulikuwa na jeneza lililokuwa wazi.
Ishu hiyo ilianza kujaza watu majira ya saa 6 usiku ambapo katika lifti kulikuwa na baunsa ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kufungua na kufunga mlango wa usafiri huo wa kwenda juu.

Hakuna mtu aliyeingia ukumbini humo bila kusachiwa na chombo maalumu cha usalama na kisha kusindikizwa na ‘askari’ maalum waliokuwa wamevalia vinyago vya kutisha.

Inasemekana kadri muda ulivyozidi kwenda, mambo yalizidi kupamba moto ambapo katika jeneza lile aliwekwa binadamu na damu nyingi ambapo kila mdau aliyekuwemo ndani alilazimika kumwagiwa na wengine kuilamba.

Zoezi hilo liliendelea hadi mwandishi wetu alipoondoka eneo hilo ambapo nje kwenye maegesho (parking) aliyakuta magari mengi ya kifahari.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliohudhuria mkutano huo walionekana ni wenye uwezo wa hali ya juu, wakiwemo raia wa kizungu.

Mmoja wa watu waliohudhuria sherehe hiyo, alisema hufanyika kila mwaka katika majira kama haya.

Source: Global publishers 3-November-2010.
 
Joss

Joss

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2009
Messages
729
Likes
1
Points
35
Joss

Joss

JF-Expert Member
Joined May 28, 2009
729 1 35
Hiyo tar 31 October ni Hollowing day husheherekewa sana kwenye nchi za magharibi kwa kuvaa vinyago vya kutisha.
Historia yake inahusiana na majini(ghost), kwa hiyo wao wanasema kuwa siku hiyo huvaa vinyago vya kutisha ili kuyatisha hayo majini .

Kwa baadhi ya nchi za Asia kama Vietnam siku hiyo hutumiwa kuwaombea marehemu waliokufa na huwa ni siku ya huzuni.

Kwa hiyo nafikiri raia wa nje hususani hao wazungu waliokuwepo hapo walikuwa wanaisheherekea siku hiyo kwani kwao ni disko,vinywaji kwa kwenda mbele.
 

Forum statistics

Threads 1,250,281
Members 481,278
Posts 29,726,972