Ulimwengu wa FTA Satellite TVs

Nimeipata vizuri tu ila signal sio kubwa kama ilivyokuwa kwenye sat ya zamani.Pia mfumo haujabadilika hata wenye Mediacom wanaweza kuzipata.
Mkuu umepata na channel gani za ziada tofauti na ITV, Chan 5 na Capital tv?
 
Nimeipata vizuri tu ila signal sio kubwa kama ilivyokuwa kwenye sat ya zamani.Pia mfumo haujabadilika hata wenye Mediacom wanaweza kuzipata.
Natumia hiyo Receiver ya Mediacom naona ITV, EATV na CAPITAL wamebadilisha satellite na frequency zao, naomba maelekezo ya kuingiza hayo mabadiliko kwenye receiver.
 
Naombe kujuzwa hii kitu
IMG_20191010_110712_595.jpeg
 
- Kuna Qsat model Q15, Q23, Q26 nk. Hizi bei zake zinaanzia 150,000/- kupanda juu kulingana na model. Hizi ni FTA (HD) lkn Uzuri wake ni kwamba ina unscramble channels zote zilizofungwa kwa PowerVU na BISS key. Hawa hawana decoder feki sokoni.

- Kuna Mediacom 940+, hii nayo ni FTA (HD) na ni nzuri pia, ingawa haina uwezo wa kufungua channels zilizofungwa kwa kwa BISS na PowerVU. Bei zake zinaanzia 95,000/- .

- Kuna Strong SRT 49 series (HD). Hizi ndio baba lao, na ni wakongwe sokoni kuliko hao hapo juu. Bei zao zmeshiba, na zinaanzia 250,000/- ingawa zipo feki nyingi sana. Hizi hufungua channels za FTA na zile zilizofungwa kwa BISS na PowerVu.

- Kuna Azsky G6 (HD), hii nayo inafungua FTA na zilizofungwa kwa BISS. Ni chache sana sokoni, ila bei inaanzia 200,000/-
- Kuna Astrovox (HD), nazo zipo sokoni ingawa sio pupular. Bei zake zinaanzia 80,000/-
- Kuna Starsat 2000 (HD) extreme, bei yake inaanzia 230,000/-.
- OnSat receiver inafungua FTA na canal 22w kwa account. Inauzwa kuanzia 190,000/-.
- Freesat v7 (HD) nayo inafungua FTA. Bei zake zinaanzia 100,000/-.
- OpenBox (HD) hii na yenyewe ina PowerVu,bisskeys, RF na be yake inaanzia 90,000/-.
- Digisat 9800 yenye rf, bisskey nk na bei yake inaanzia 85,000/-.

Nadhani kwa kuanzia unaweza kucheki hizo. Bei zinatofautiana kati ya duka na duka na namna unavyojipeleka.
Please naomba ushauri wako kuhusu hii fta decoder!
Shukran.
 

Attachments

  • Screenshot_2019-11-29-09-37-10-1.png
    Screenshot_2019-11-29-09-37-10-1.png
    115.1 KB · Views: 8
  • Screenshot_2019-11-29-09-37-03-1.png
    Screenshot_2019-11-29-09-37-03-1.png
    37.3 KB · Views: 8
Back
Top Bottom