Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 14,969
- 10,462
- Kuna Qsat model Q15, Q23, Q26 nk. Hizi bei zake zinaanzia 150,000/- kupanda juu kulingana na model. Hizi ni FTA (HD) lkn Uzuri wake ni kwamba ina unscramble channels zote zilizofungwa kwa PowerVU na BISS key. Hawa hawana decoder feki sokoni.
- Kuna Mediacom 940+, hii nayo ni FTA (HD) na ni nzuri pia, ingawa haina uwezo wa kufungua channels zilizofungwa kwa kwa BISS na PowerVU. Bei zake zinaanzia 95,000/- .
- Kuna Strong SRT 49 series (HD). Hizi ndio baba lao, na ni wakongwe sokoni kuliko hao hapo juu. Bei zao zmeshiba, na zinaanzia 250,000/- ingawa zipo feki nyingi sana. Hizi hufungua channels za FTA na zile zilizofungwa kwa BISS na PowerVu.
- Kuna Azsky G6 (HD), hii nayo inafungua FTA na zilizofungwa kwa BISS. Ni chache sana sokoni, ila bei inaanzia 200,000/-
- Kuna Astrovox (HD), nazo zipo sokoni ingawa sio pupular. Bei zake zinaanzia 80,000/-
- Kuna Starsat 2000 (HD) extreme, bei yake inaanzia 230,000/-.
- OnSat receiver inafungua FTA na canal 22w kwa account. Inauzwa kuanzia 190,000/-.
- Freesat v7 (HD) nayo inafungua FTA. Bei zake zinaanzia 100,000/-.
- OpenBox (HD) hii na yenyewe ina PowerVu,bisskeys, RF na be yake inaanzia 90,000/-.
- Digisat 9800 yenye rf, bisskey nk na bei yake inaanzia 85,000/-.
Nadhani kwa kuanzia unaweza kucheki hizo. Bei zinatofautiana kati ya duka na duka na namna unavyojipeleka.