Ulimwengu uliofichika (Mungu hajui nini hatima ya maisha yako)

KijanaHuru

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
1,822
2,290
Habari yenu ndugu zangu
Naamini muwazima wa afya njema pia poleni na majukumu yaa kila siku

Naomba sana tena sana Ndugu moderator uzi huu hauna nguvu zaidi katika dini hivyo naomba usipelekwe katika jukwaa la dini.

NIlipenda sana niweze kuuweka katika jukwaa lile lingine sema zinachelewa sana kuwa approved ndio maana nauweka hapa,Naombeni tena uzi huu naomba ubakie hapahapa.

Niukweli usiopingika (MUNGU HAJUI NINI HATIMA YA MAISHA YAKO) japo wanadamu tunashindwa kutambua kwasababu ya kutokuelewa nini ile nguvu iliyoko ndani yetu.
Watu wasema Mungu ni muweza wa yote anajua mawaazo yetu anajua haja zetu yaani kila kitu kuhusu sisi wanadamu anajua na kila mtu ataweza kuthibitisha kwa namna yake ya vitabu vyake ama misingi ya dini yake au Imani yake.

Kabla sijawez akukupa sababu za hoja zangu kwanza nakuomba uelewe jambo moja huenda hki nakuambia leo ni jambo jipya kabisa wala haujawahi kulisikia mahali lakini zaidi ya yote unaweza ona kama mim na kufuru ila ukweli unabakia palepale Mungu hajui wew ni wamotoni niwapeponi kesho utafanya nini yain anything about you hajui kabisa.

Sasa nakuomba usipaniki kwanza sababu ya kauli za hapo juu ila nakuomba tulia kidogo umbuza jazba uweze kunielewa sasa.

Kuna baba mmoja anampa mwanaye Shilingi laki moja kwakuwa ameweza kufaulu mtihani wake wa mwisho na kuna mwingine anampa elfu hamsini kwakuwa hakufanya vizuri sana katika mtihani wake wamwisho.

Kesho yake aliyefaulu anachukua marafiki zake wanaenda kufurahia maisha japo kwa mda kuondoa zile stress za kusoma lakini na kufurahia mafanikio yao

Aliyepewa 50 anajisikia mnyonge kidogo japo ajapo anajipa moyo anayonafasi nyingine ya kutetea heshima yake anaenda kwa baba yake akimuomba amuongezee hela kidogo ili aweze kufanya biashara zingine baba anamuongeza huyu mtoto tena laki mbili sababu ya kuona amefanya maamuzi mema japo mtihani wake wa mwisho hakufanya vyema.

Sasa sikia jambo moja hivi kama Mungu anajua wewe ni wamotoni kwanini aendelee kukuletea wahubiri kila siku kwa ajili ya kukubadirisha wakati anaelewa hatima yako ni ya motoni?

Ingekuwa anajua kweli na anakuletea habari hiyo Naweza sema Huyu Mungu ni Mnafiki, Sio uungwana kabisa najua wewe tumeazimia kukunyonga lakini nakusumbua tu kuendela kukuambia leta utetezi wako, yaani nakutengenezea zengwe ushindwe kujitetea? hapana Mungu hawezi fanya hivyo kama hawezi fanya hivyo Hajui hatima ya maisha yako.

Rudi kidogo katika mwanzo wa uumbaji pale Edeni, Utaona yakuwa mwanadamu Alikwisha pewa mamlaka ya maisha yake yeye mwenyewe binafsi katika mikono yake, Yaani wewe mwanadamu ndio uamue nini utafanya

Ndio maana Mungu hakujua kama Eva angekula tunda hata walipokula pamoja na Adam bado alipofika akaanza kuita hakujua wako wapi hawa Adamu na Eva Kumbuka Mungu unayesema anajua Kila kitu amejua mwanadamu anafanya jambo linalomgarimu na kuugalimu ulimwengu mzima na hajalizuia sasa tutaamini vipi wakati ameshindwa kulizuia?

Kumbuka hata shetani unapoambiwa alikuwa malaika kule Mbinguni yeye pia alipoanza kuasi Mungu hakujua kabisa
Kumbuka Hata Wale watoto wa Adamu walipouana Mungu anamuuliza Kaini ndugu yako yuko wapi? Ukiendelea mbele utaona Mungu anadai Sauti ya Kaini anaisikia ikimlilia lakini hajui yuko wapi
Vipi umeanza kuja kidogo?

Kwa ufupi hapo totally unaweza kujua yakuwa Mungu mambo mengi hayajui kuhusu Mwanadamu kesho yake hatima yake nk

Nikukumbushe tu kitu kimo kabla sijaendelea kumbuka Shetani hana nguvu ya kumshinda mwanadamu mapepo,majini,vinyamkela nk havina hata uwezo wakupambana na mwanadamu ila sasa mwanadamu kuna kitu umefichwa haujafundishwa ama haujaelezwa na ndio maana unaogopa hata bundi tu likilia kwako.

Sasa NINI NAFASI YA MUNGU KAMA UMEONA HAJUI WALA KUTAMBUA HATMA YA MAISHA YAKO?

Kwanza ule udini na ulokole wako weka pembeni kwanza ili uweze kunielewa vyema usipouweka pembeni utabakia na udini waoko tu.

Wanadamu wote duniani ni watumwa yaani kila mwanadamu ni mtumwa vivyo hivyo kwa viumbe vingine nk
Hakuna mwanadamu aliyehuru kila mtu ni slave to something,someone nk
Ila tumetofautiana jambo moja tu who is your master?
Yule MKubwa wako ndiye anakufanya uonekane jinsi ulivyo sasa

Sasa Nafsi ya Mungu ni ipi?
Mungu anakuhitaji wewe kwa namna hii wewe ndio umpe kibali cha kuongoza your next step, yaani hatua yako inayofuatia ndio ambayo wewe unapaswa kumpa Mungu uhuru na maisha yako

Mungu hawezi kukuingia utaratibu wa maisha yako wakati hata haujampa kibali, kumbuka yule mtoto ambaye hakufanya vyema shule anapewa elfu hamsini lakini anarudi kwa baba kumwelezea juu ya biashara yake ndipo sasa Baba anamuongezea kiasi kikubwa zaidi ya kile hata alichopew aaliyefauli sababu tu Kamruhusu Baba yake na yeye kuwa kitu kimoja katika mipango yake,

Yaani Kama Mungu hua anakuandikia kila kitu sasa wewe leo unaenda bar unaenda kuchepuka unataka kusema Mungu amekuandikia wewe uende bar?

Amekuandikia wewe uende kwa mchepuko? amekuandikia wewe ujinyonge? amekuandikia wewe uanze kupakuliwa? Hapana ni uongo mkubwa hakuna kitu kama hicho

Ila wewe ndio mwenye hatima ya maisha yako uaanamua wewe uwe mtumwa wa nani Unapompa nafasi Mungu ndio unajua anaanza sasa kuangalia hata kesho yako, ndio anawez akakuambia hapo usiende hapo nenda.

Ukielewa Kitu Karma, Ukielewa Sheria na Kanuni za Ulimwengu hili jambo hata sio gumu kulielewa, nakosa lugha rahisi zzaidi ya kueleza ila nikwamba Mungu ni hadi umruhusu wewe aweze kuwa controller wa maisha yako, Usipo mruhusu hata haiwezi kuwa hivyo.

Kwa Mkazo
-Mungu alitupa wanadamu uwezo hata wakujiongoza sisi wenyewe pasipo kuwa chini ya mtu yeyote(Ila kumbuka yeye ndio top anaweza fanya lolote)
-Yaani kuna mfumo ukiweza kuuishi na kuufuata utashangaa hata haulijui kanisa wala msikiti ila siku ya kiama upo vip peponi(kiding)
-Ushawahi jiuliza kabla ya hizi dini kusambaa kote wale wa zamani watahukumiwa na nini? ukiwaza hilo ndio unarudi hapo juu sasa kupata mrejeo kuwa kuna mfumo ambao wanadamu tunapaswa kuufuata.

Kuna mtoto toka amezaliwa yeye hajawahi kwenda sehemu yoyote kuabudu wala kusali ila amekuwa akiishi vizuri na jamii inayomzunguka kadri anavyoendelea kukua jamii nzima inakuwa inamuangalia kwa namna ya pekee kutokana na jinsi anavyoishi na jamii yake vizuri hivyo inapelekea kuishi maisha ya Baraka kubwa mno kutoka kwa watu japo wale wasioelewa wanasema Mungu kambariki no Hapana nikwamba katumia uhuru wake vyema ila sasa anapoenda na kwa Mungu wawe pamoja ndio anafanikiwa zaidi ya hapo awali.

Nitakuja siku nyingine kuelezea uhuru wa mwanadamu ulivyo namna ambavyo unaweza kusihi pasipo kuingiliwa na tawala yoyote uelewe yale mamlaka uliyonayo,
Nikwamba mwanadamu unaweza ukatawala anything and more kuna mengi sana usiyoyajua kuhusu wewe mwenyewe soon or later nitakuja

Pia kitabu soon kinakamilika nilichoelezea kwa upana Mipaka Iliyopo Kati ya Mwanadamu na Mungu namna gani mwanadamu umepewa kuishi mfumo wa kiutawala kutoka kwa Mungu hadi kakiumbe ka mwisho
wewe mwanadam upo kundi gani wapi upo una nguvu gani una nini?

Nimeshindwa kuendelea kuandika sababu ya mda ila next time nitakuja kuongezea nyama kidogo, hapa nimejaribu kuelezea kwa lugha rahisi ambayo walau kila mtu anaweza kuelewa pasipo shida kubwa sana ila ukiwa na swali usisite unaweza kuuliza hapo chini

SEE You Next Time
 
Haya nadhani ni mawazo yako.
Labda tupate reference ya kwenye maandiko
Madhara yanayotokea sasa ni sababu ya Anguko la pale bustani ya edeni unadhani Mungu kama alikuwa anajua kwanini hakumzuia mwanadam? kwanini Mungu anamuuliza Adamu uko wapi?kwanini ?

Pia nimeongea tayari mengi hapo ndani unaweza ukapitia ukasoma acha uvivu
 
Sasa sikia jambo moja hivi kama Mungu anajua wewe ni wamotoni kwanini aendelee kukuletea wahubiri kila siku kwa ajili ya kukubadirisha wakati anaelewa hatima yako ni ya motoni?
Ingekuwa anajua kweli na anakuletea habari hiyo Naweza sema Huyu Mungu ni Mnafiki, Sio uungwana kabisa najua wewe tumeazimia kukunyonga lakini nakusumbua tu kuendela kukuambia leta utetezi wako, yaani nakutengenezea zengwe ushindwe kujitetea? hapana Mungu hawezi fanya hivyo kama hawezi fanya hivyo Hajui hatima ya maisha yako.
Hapo unamaanisha Mungu ameshatuhukumu ingali bado tu hai hapa duniani,siyo kweli kabisa. Duniani bado tuna nafasi ya kubadili nyendo zetu na ndio maana kwa kuwa Mungu anatupenda hutuletea waubiri ili tumrudie yeye.
 
MKuu naomba usome andiko zima suicomment tu naomba usome tena na hilo unalolisema ndio linawapoteza wengi sana wanaishia kukata tamaa na kutokojua nini maisha yana maanisha
mnakamezeshwa tu pasipo kuelewa maarifa kuyasoma ni bure ila kufuata ama kuacha ni maamuzi yako binafsi
 
asante kwa somo zuri bt subiri wafia dini waje
Na ndio wanapotea sana kwa kutokuelewa wakati Mambo yote yapo wazi kabisa, wanashindwa kuelewa mfumo unataka nini wao wanatengeneza sheria na kanuni zao za kidini tu
 
Kwahiyo wanaomba kwa mungu na wanafanikiwa ni personal mind set ndo hutoa nguvu au ni mungu ndo anatenda?

Pili ushasikia nakala za DNA cloning then hhuman ndo kama product

NB
Not easy as u think about!
 
Mwenyezi Mungu alituumba, akatukadiria maisha yetu(kuanzia mwanzo mpaka mwisho wetu). akatufundisha mema na mabaya, akatupa Uhuru was kufanya mambo yetu huku akitupa hukmu ya Kila tendo utakalofanya, na akatufundisha jinsi ya kufanya ili kubadirisha kadar alizotupangia Kama ni mbaya(Dua)...hivyo ni juu yetu kuchagua njia tunayoitaka following the consequences
 
Uksoma vizuri Yesu alikua anajua wanadamu wanawaza nn ndio maana hata yeye alojua kesho yake itakua nn maka kifo msalabani.
Na ukisoma kitabu cha ufunuo utaona kuna idadi ya watakao ingia mbguni kama waizrael makabila 12 na ujumla wao
Sasa naomba hapo udadavue vzr
KWahiyo kamandio hivyo kwanini unahubiriwa wakati Mungu anajua unaenda motoni?
 
Madhara yanayotokea sasa ni sababu ya Anguko la pale bustani ya edeni unadhani Mungu kama alikuwa anajua kwanini hakumzuia mwanadam? kwanini Mungu anamuuliza Adamu uko wapi?kwanini ?

Pia nimeongea tayari mengi hapo ndani unaweza ukapitia ukasoma acha uvivu

Ah ww bwana so do you think Mungu alikuwa hajui Adam yuko wapi wakati anamuuliza alipo? Kwa akili yako ya kawaida ww unaweza kuwa mhandisi wa kutengeneza kitu ambacho utakuwa unakijua kwa 98% tu?
 
Kwahiyo wanaomba kwa mungu na wanafanikiwa ni personal mind set ndio hutoa nguvu au ni mungu ndo anatenda?

Pili ushasikia nakala za DNA cloning then hhuman ndio kama product

NB
Not easy as u think about!
MKuu naona haujasoma mpaka mwisho hoja yangu hapo juu ngoja nikupe mambo ya nyongeza uelewe

Kufanikiwa sio lazima Mungu akuwezeshe wala sio lazima uweze kupitia Mungu, kuna kitu kinaitwa Balance of nature hii sio kama ile uliyosoma katika mashule hapa tunaikazia kidogo na kuita Balance Of Law Of The Universe hii kitu ni kubwa mno kuzidi unavyofikiria hii kitu ukiielewa ndio uatajua kwanini kuna masikini wakati huohuo kuna matajiri kwanini sio wote wanaoomba Mungu hufanikiwa na kwanini wengine hufanikiwa pasipo kuroga wala kuomba Mungu, ila watu wa dini mnaishia tu kusema ni Neema Za Mungu.

Mfano ukiwa unaishi viuri na jamii inayokuzunguka na unashirikiana vizuri na watu ni rahisi kufaniiwa katika mambo mbalimbali kuliko ungekuwa unaishi vibaya na jamii yako.

Mungu hakupi wewe kuishi vizuri na jamii bali wew endio jukumu lako kuamua njia ipi utaipitia mwisho wasiku sasa ndio unapotambua yakuwa Ili uweze kuwa na faida zaidi nilazima uwe chini ya kitu au mtu fulani nk

Hapo ndio wengine huchagua ulozi na wengine huenda kwa Mungu

Sasa master wako ndio atakuongezea katika kufanya guidance ya maisha yako, kulingana na jinsi utakavoishi naye na huyo master yaweza kuwa nguvu yoyote ile unayoiamini kama Mungu, Shetani nk

Nimekuambia kitu kikubwa sana hapa Nakuombea tu ukielewe

Ila rudia tena kusoma hoja yangu
 
Mimi wanaponiachaga hoi ya kuwa yesu ni MUNGU alafu hapohapo unaona huyo yesu anaomba tena msaada wa baba yake
Sijaandika hoja kuhusu Yeni Mungu au lah lakini jua jambo moja muhimu hiliMungu kama anauwezo kuliko vitu vyote jua bas anaweza kufanya jambo lolote lile na likawa mfano wanaoamini Yesu ni Mungu wanakuambia jambo kama hili

Mungu Pekee ndiye husamehe dhambi mwanadamu hawezi kumfutia mtu madhambi yake lakini Yesu alifanya kwanini alifanya jambo ambalo ni la Mungu pekee?
sikushawishi bali ni maswali ya kujiuliza tu anyway tuendelee na hoja ya pale juu
 
Ah ww bwana so do you think Mungu alikuwa hajui Adam yuko wapi wakati anamuuliza alipo? Kwa akili yako ya kawaida ww unaweza kuwa mhandisi wa kutengeneza kitu ambacho utakuwa unakijua kwa 98% tu?
Asilimia 2 ulizoacha ndio hoja yangu ndugu
 
Mwenyezi Mungu alituumba, akatukadiria maisha yetu(kuanzia mwanzo mpaka mwisho wetu). akatufundisha mema na mabaya, akatupa Uhuru was kufanya mambo yetu huku akitupa hukmu ya Kila tendo utakalofanya, na akatufundisha jinsi ya kufanya ili kubadirisha kadar alizotupangia Kama ni mbaya(Dua)...hivyo ni juu yetu kuchagua njia tunayoitaka following the consequences
Hakika na ndio maana katika uhuru huo Mungu huwa hawezi kukuingilia unapaswa wewe kumruhusu aweze kutawala uhuru wako usipotaka basi hawezi fanya hivyo ndio hapo hoja yangu inaposimamia
 
MKuu naona haujasoma mpaka mwisho hoja yangu hapo juu ngoja nikupe mambo ya nyongeza uelewe

Kufanikiwa sio lazima Mungu akuwezeshe wala sio lazima uweze kupitia Mungu, kuna kitu kinaitwa Balance of nature hii sio kama ile uliyosoma katika mashule hapa tunaikazia kidogo na kuita Balance Of Law Of The Universe hii kitu ni kubwa mno kuzidi unavyofikiria hii kitu ukiielewa ndio uatajua kwanini kuna masikini wakati huohuo kuna matajiri kwanini sio wote wanaoomba Mungu hufanikiwa na kwanini wengine hufanikiwa pasipo kuroga wala kuomba Mungu, ila watu wa dini mnaishia tu kusema ni Neema Za Mungu.

Mfano ukiwa unaishi viuri na jamii inayokuzunguka na unashirikiana vizuri na watu ni rahisi kufaniiwa katika mambo mbalimbali kuliko ungekuwa unaishi vibaya na jamii yako.
Mungu hakupi wewe kuishi vizuri na jamii bali wew endio jukumu lako kuamua njia ipi utaipitia mwisho wasiku sasa ndio unapotambua yakuwa Ili uweze kuwa na faida zaidi nilazima uwe chini ya kitu au mtu fulani nk
Hapo ndio wengine huchagua ulozi na wengine huenda kwa Mungu
Sasa master wako ndio atakuongezea katika kufanya guidance ya maisha yako, kulingana na jinsi utakavoishi naye na huyo master yaweza kuwa nguvu yoyote ile unayoiamini kama Mungu,Shetani nk
nimekuambia kitu kikubwa sana hapa Nakuombea tu ukielewe

ila rudia tena kusoma hoja yangu
Sio nirudie kusoma coz najua n utakuja andika
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom