Ulimwengu na elimu ya Namba

bonvize

JF-Expert Member
Feb 4, 2010
323
233
Habari wana JamiiForums

Karibuni katika uzi maalum ambao utakuwa unaelezea kwa kuna elimu ya Namba(Numerology). Michango yenu ni muhimu sana wadau wote wenye uelewa wa elimu ya namba maana humu JF nimekuwa napata wakati mgumu kutafuta haya maarifa, niliwahi weka huu uzi katika majukwaa mengine lakini muitikio wake haukuwa mzuri. Kwa upande wangu nitaaanza kwa kuelezea tarehe ya kuzaliwa

Tarehe ya kuzaliwa huwa inabeba taarifa zote muhimu kuhusu maisha ya muhusika na hii ni kwa mujibu wa elimu ya namba(Numerology). Katika hatua ya mwanzo nitaanza kwa kuzungumzia kitu muhimu ambacho kinapatikana kwa kukokotoa tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa, kitakachopatikana katika ukokotozi huo kitaitwa Mzunguko wa maisha (Tafsiri Binafsi). Kuna mambo muhimu ya kuzingatia katika ukokotozi wa mzunguko wa maisha ambayo ni namba mama na namba kiongozi.

Namba Mama
Namba mama ambazo zitakuwa zikitumika katika uchambuzi ni 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9 namba yoyote baada ya 9 inaweza kurudiswa katika namba mama. Zingatia mfano unaofuata
10=1+0= 1
27= 2+7= 9=
389= 3+8+9=20=2+0=2

Kila namba mama kuanzia namba 1 hadi 9 inakuwa imebebe nguvu maalum na hiyo nguvu inakuwa imegawanyika katika pande mbili, nguvu chanya na nguvu hasi.

Namba Kiongozi
Namba kiongozi ni namba ambazo zina sifa maalumu, nazo ni 11 na 22, namba hizi zinapojitokeza wakati wa kukokotoa huwa zinabaki kama zilivyo, zingatia mifano ifuatayo;
155= 1+5+5=11
949=9+4+9=22

Namba hizi zinakuwa zimebeba sifa za Namba Mama na Namba Kiongozi, zingatia mfano ufuatao;

155= 1+5+5=11=1+1=2
949=9+4+9=22=2+2=4

Wakati mwingine hizo Namba Kiongozi huwa zinaandikwa 11/2 na 22/4.

Mzunguko Wa Maisha
Mzunguko wa maisha ni funguo ya kufungua kile ambacho mwenyezi Mungu amekiweka ndani yako wakati wa kukuumba. Hii ni namba ya kudumu katika kipindi chako chote cha uhai, daima haitabadilika kwa kuwa inatokana na tarehe yako ya kuzaliwa.

Mzunguko wa maisha utakuwezesha kutambua mambo unayotakiwa kuyatimiza katika kipindi chako cha uhai kwa kuzingatia fursa na vipaji ambavyo Mungu amekuumba navyo. Mzunguko wa maisha utakuwezesha kwa urahisi kufanya maauzi kuhusu;
  • Uelekeo wa maisha
  • Kupanga na kutimiza Malengo
  • Mahusiano
  • Mipango ya mbeleni
  • Kazi ambayo itakufikisha katika kilele cha mafanikio
Hivyo basi Mzunguko wa maisha utatuwezesha kutambua mazingira ambayo yataambatana na fursa ambazo Mungu ameziumba kwa ajili yako.

Mzunguko wa maisha ni namba inayopatikana kwa kuzipunguza tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa hadi kufikia katika Namba Mama au Namba Kiongozi, mfano wa kwanza unahusu Namba Mama na wa pili unahusu Namba Kiongozi

Mfano wa kwanza 21/04/1990
Tarehe 21= 2+1 = 3
Mwezi 04= 0+4= 4
Mwaka 1990=1+9+9+0=19=1+9=10=1+0= 1

Baada ya kupata hizo Namba Mama kutoka katika tarehe ya kuzaliwa, mwezi na mwaka unazijumlisha zote;
3+4+1=8

Mfano wa pili 14/01/1985
Tarehe 14= 1+4 = 5
Mwezi 01= 0+1= 1
Mwaka 1985=1+9+8+5=23=2+3=5

5+1+5=11
Mada iliendelea hapa
 
pich

Picha ndio limeisha au?
 
Mkuu natumaini umejielezea vizuri
1. ni inausiana na namba mama
2 .na 11 na 22 ni namba tawala
Sasa mnataka amalizie nini?
 
Insatiable knowledge!
Unawaonjesha wenzio utamu!

Nitawaletea hili somo mshibe, Niko busy kwa sasa , achaneni na huyu muhuni.
 
Mkuu natumaini umejielezea vizuri
1. ni inausiana na namba mama
2 .na 11 na 22 ni namba tawala
Sasa mnataka amalizie nini?
Wewe umeelewa nini sasa hapo. Ukishapata jibu la namba mama au namba tawala then what next hapo ndiyo hajamalizia
 
Insatiable knowledge!
Unawaonjesha wenzio utamu!

Nitawaletea hili somo mshibe, Niko busy kwa sasa , achaneni na huyu muhuni.
Habari, muhuni nimekuja, mbona ujaendeleza somo tena?
 
Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom