Ulimwengu awananga vikali viongozi wa CCM, asema wanahatarisha amani ya Watz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulimwengu awananga vikali viongozi wa CCM, asema wanahatarisha amani ya Watz

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Nov 3, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Fujo hizi za ‘wanasiasa’ zinatuhatarisha sote

  Jenerali Ulimwengu

  NIMEJARIBU kwa njia kadhaa kuonyesha ni kwa nini kizazi cha sasa cha watu wanaojiita wanasiasa hakina uwezo wa kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mojawapo ya sababu za hali hii ni kwamba wanasutwa na dhamira zao.

  Ukiwaangalia wengi wa wanasiasa waandamizi waliomo ulingoni hadi leo, utagundua kwamba ni watu waliofanya kazi karibu na Mwalimu. Baadhi yao walikuwa karibu sana na wengine walikuwamo, japo hawakuwa karibu kiasi hicho. Lakini wengi sana walikuwamo ndani ya mifumo ya kisiasa na kiutawala wakati Mwalimu akiwa ni kiongozi wa chama chake na mkuu wa serikali yake.

  Hawa ni watu waliokuwa wamezoea kuitikia kila kitu alichosema Mwalimu, wakati mwingine wakiwa hawakubaliani naye lakini hawathubutu kusema mawazo yao hadharani kwa kuhofia “kumwaga unga.”

  Walikuwa ni waoga na wanafiki waliokuwa tayari kusema lo lote walilodhani lingemfurahisha Mwalimu alimradi wabakie na nafasi zao, au wasogezwe juu kidogo. Baadhi yao walifanikiwa kuingia katika nafasi za juu kabisa kupitia unafiki wao huo. Leo tunao na tunaona sura zao halisi.

  Baada ya Mwalimu kuwa ameondoka duniani wanafiki hawa wamepata nafasi ya kufanya kile walichokuwa wakitamani kukifanya lakini wakiogopa. Hivi sasa hakuna tena mtu anayeweza kuwaonya, kuwaasa, kuwakemea, kuwakaripia au kuwarudi. Wanaweza kufanya vile watakavyo bila hofu ya lo lote. Kwao, kuondoka kwa Mwalimu imekuwa ni faraja kubwa.

  Ndiyo maana wanaendesha chama alichokiasisi Mwalimu mwenyewe kama kijiwe cha wahuni wasioisha kulumbana. Inastaajabisha kwamba chama ambacho kinaweza kujinasibu kama chama alichokiasisi kimekuwa ni kituo cha fujo na vurugu ambamo watu wanaojiita viongozi wanazozana kama madalali wa mnada wa samaki, wakirushiana kila aina ya kashfa, vijembe, ubeuzi na matusi.

  Ni kama vile kijiwe hicho kimejibanza katika kona ambako wazee wa kijiji hawapiti, kwani ingekuwa vinginevyo angalau mzee mmoja angekuwa amekwisha kuwatia bakora wahuni hawa na kukomesha ghasia zao.

  Nimekuwa nikisikiliza matamko ya baadhi ya “wanasiasa” ndani ya chama hiki, nami napata woga mkubwa. Mambo kama yanayotokea Arusha, ambayo hayapishani sana na kile kilichotokea miaka ya karibuni ndani ya jumuiya ya wanawake ya chama hicho, mwanzoni yalionekana kama mambo ya aibu yanayofanywa na watu wasiokuwa na haya, lakini sasa ni dhahiri kwamba ni mambo ya hatari kwetu sote.

  Hiki ni chama kilichobeba dhamana ya kuendesha serikali yetu na nchi yetu kwa ujumla, na wao hujinadi kwa mbwembwe kama chama-tawala. Aidha ni chama ambacho kinaendeshwa na watu wasiochoka kutuhubiria kile wanachokiita “amani na utulivu,” kana kwamba hiyo inaweza kuwa sera ya chama cho chote.

  Lakini ndicho chama hicho hicho kinachofanya vurugu na kusababisha fujo ndani ya chama chenyewe kutokana na kugombea ngawira.

  Ningependa kusisitiza kwamba chama-tawala kimebeba dhima nzito ambayo inakitaka kiwe na uangalifu mkubwa sana. Katika mpangilio wa kifamilia chama hicho ndiye mwana mkubwa wa kwanza ambaye anatakiwa kuwalea, kuwalinda, kuwatetea na kuwaongoza wadogo zake huku akiwaonyesha namna ya kuishi kama ndugu.

  Iwapo wakati baba wa kaya ameondoka na kijana wa kwanza akajenga tabia ya fujo nyumbani kwake, akipigana na mke wake na kunyang’anya chakula cha watoto, kaka kama huyo atashindwa kuwaongoza wadogo zake. Hafai.

  Nimekuwa nikikiangalia chama-tawala kikiserereka kutoka mserereko mmoja hadi mwingine huku kikionyesha wazi wazi kwamba ni mithili ya motokari isiyo na breki na ambayo usukani wake unagombewa na madereva saba, kila mmoja akiwania kuielekeza katika njia anayoijua yeye. Hilo gari halifiki ko kote salama.

  Tunavyo vyama vichanga, ambavyo katika mfano wangu ni wadogo wa chama-tawala. Watajifunza nini kutoka kwa kaka kama huyu? Vurugu, fujo, ghasia, zogo. Ni dhahiri vyama vidogo hivi navyo vitataka kufanya yale vinayoyaona kwa kaka mkubwa, kwanza ndani ya vyama hivyo vyenyewe, lakini zaidi katika ushindani kati ya hivyo vyama na chama-tawala.Vitajifunza kushindana kwa vurugu na fujo.

  Ni hivi: Iwapo kila mtu anaona yanayotokea ndani ya chama-tawala, uhuni na ukora wa kusikitisha, iwapo watu wanaona kwamba wakubwa wa chama hicho wako tayari kufanyiana kila aina ya hila – hata kuuana – ni nani katika chama cha upinzani anaweza kuamini kwamba watu kama hao watamtendea haki katika ushindani baina ya chama chake na chama-tawala? Hakuna.

  Haiingii akilini na wala haiwezekani kwamba wale wasiotendeana haki nyumbani kwao, watu wanaoparurana kila siku huko huko kwao, watakuja kuwatendea haki watu baki, washindani wao rasmi. Hata mtoto mdogo ataliona hili.

  Kwa kasi hii tunayosafiri nayo kwenda katika vurugu, siku moja tutafika huko. Tusijidanganye hata siku moja kwamba vurugu zinaowakumba wenzetu katika bara hili ni mahsusi kwao tu na sisi haziwezi kutukumba. Kwa kweli zikitokea zitakuwa wala hazikutukumba bali zitakuwa zimetukumbatia tu, kwani tutakuwa tumejipeleka huko sisi wenyewe. Ikija kutokea hivyo tusianze kuulizana ni nini kimetusibu. Hiki ndicho ninachokieleza katika makala hii.

  Ingekuwa inawezekana kwa ‘wanasiasa’ kufanya vurugu, wakatukanana, wakasutana, wakabezana, wakazomeana, wakakashifiana, wakasimangana, wakang’ong’ana, wakazodoana, kisha wakapanda chati, wakachapana makonde, wakatiana bakora, wakachomana moto, wakatoboana macho, wakakatana miguu, wakanyweshana sumu, wakakatana shingo.... na bado wengine tukabaki salama, tungekuwa na ahueni.

  Tungewaacha hao “wanasiasa” wakamalizana huku sisi tukishika majembe yetu kuelekea kondeni. Lakini kwa bahati mbaya haiwi hivyo. Vurugu zao zinahitaji mtaji wa wananchi wa kawaida ambao ndio watekelezaji wa vururgu hizo wakati zinaenezwa nchi nzima. Wananchi wa kawaida ndio wapiganaji-wahanga, chakula cha makombora, wanaoteketea ili “wanasiasa” wapate wanachokitaka.

  Mwaka 1997 tulikaa na Mwalimu Nyerere hotelini kwake mjini Kinshasa tukiangalia ng’ambo ya pili ya mto Kongo, mji wa Brazzaville, ambako makombora yalikuwa yakirushwa kutoka upande mmoja wa mji hadi upande mwingine, yakisababisha miale ya moto, mawingu ya moshi, mitikisiko ya majumba na miti na maangamizi ya mamia ya wananchi. Yote hiyo kwa sababu “wanasiasa” hawakuelewana.

  Mwalimu aliangalia sinema hiyo kwa muda, kimya, akiwa ameshika kichwa chake mkononi, na kisha akauliza: “Hivi hawa ni watu wa nchi moja, na ule ni mji wao wote?” Swali hilo halikuhitaji jibu. Halafu akasema: “Hizo silaha kubwa namna hiyo wanazipata bila matatizo, lakini ukiwaambia kujenga shule watakuambia wanahitaji mfadhili.”

  Silaha watazipata kwa urahisi kwa sababu wanao “wafadhili” walio tayari kutoa silaha za kila aina, (tena kwa pande zote zinazokinzana) wakijua kwamba kuna maslahi mbele ya safari kutoka kwa ye yote atakayeshinda. Kongo Brazza ni mafuta; hapa kwetu itakuwa dhahabu, na labda uranium, na mafuta pia. “Wanasiasa” wanapozodoana hawatakosa watu wa nje wa kuunga mkono upande huu na upande ule, kwa sababu ya maslahi ya hao “wafadhili.” Watakaoumia ni wananchi wa kawaida, si “wanasiasa” hao wala “wafadhili” wao.

  “Wanasiasa” wa aina niliyoina nchini Sierra Leone (na ninayoiona katika chama-tawala leo hii) watachochea fujo hadi fujo ikolee, lakini mlipuko wa kwanza unapotokea, wataondoka na kwenda kuishi uhamishoni milipuko ikomeshwe na majeshi ya nchi za nje (kwa Sierra Leone yalikuwa majeshi ya Uingereza na Nigeria); kisha, hali ikirejea kuwa shwari, watarejea na kugawana nafasi za utawala, na kuendelea kana kwamba hakuna kilichotokea.

  Hawa ni watu wa hatari sana, na ni watu wa kuwaepuka kwa kila njia inayowezekana. Nimekuwa nikiweka neno wanasiasa katika alama za nukuu, kwa sababu kimsingi hawa si wanasiasa kwa sababu hawafanyi siasa, bali wanachofanya, kinachowashughulisha hasa hata hawalali, ni MIPANGILIO NA ‘DILI’ itakazowawezesha kuchota mali za nchi kwa maslahi yao na hao ‘wafadhili’ wa ndani na nje.

  Hawa si wanasiasa, ni wana-dili; hawafanyi siasa, wanapangilia mambo, wanasuka mipango.  Chanzo: Raia Mwema
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ulimwengu sio raia wa Tanzania, yeye aende akayaseme haya huko kwao burundi , kongo anatusemea watanzania km nani ?
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  kuna kila dalili ya wehu ktk kichwa, sio bure!
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tyipical magamba! Mkibanwa kwa hoja mnakimbilia uraia, udini - so sad!
   
 5. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulimwengu ameongea kama Mtanzania MZALENDO. Kama hoja ni uraia hata mafisadi unaowatumikia ni raia wa Tanzania.
   
 6. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Chama cha kila mtu na kamhogo kake!
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  labda hukusoma sawasawa... Ameyataja ya kongo pia.tena akaenda mbali zaidi mpaka siera leone,soma tena!
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Bashe raia wa Tanzania? hadi anawaongozea kamati ya kuratibu muundo mpya unaofaa ndani ya ccm?
   
 9. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  ..........yale yale Bashe type! hovyoo!
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  masaburi at work
   
 11. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mamako anahasara.
   
 12. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Kimekuingia eenh... Malaria sugu huyu aka Topical....hahahhhahhh Astaghafirulah...
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ulimwengu anayo point

  Lakini hayo mambo ya kumsifia nyerere yanaharibu utamu wa habari yake..

  Tumechoka na upuuzi wa nyerere..tumwache babu wa watu apumzike ametuachia watu wajinga mwenyewe tena kwa kuiba kura na kuchezea demokrasia nchini..kabla ya kifo chake..
   
 14. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kama umeamua kumwaga 'ugali' sasa mwaga na 'mboga'. Weka hadharani majina ya hao unaowajua na kuwaita 'wahuni' tuwajadili hapa na ikibidi tuwaepuke, au sivyo?
   
 15. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Hata kama Ulimwengu anatoka sijui unakojua wewe yeye ni mzalendo zaidi kuliko hao wahuni wa magamba,ni mzalendo zaidi kuliko hao waliopata uongozi kwa kupitia njia za panya(wana mtandao),ni mzalendo zaidi kuliko hao miungu wako walioiingiza nchi gizani,ni mzalendo zaidi kuliko hao waliouza NBC,ni mzalendo zaidi ya wale wanaopewa mamlaka ya kuwa ndio wasimamizi wa tozo za kesi za Dowans.ni mzalendo zaidi ya wale wanaoficha vijisenti vyao nje vikiwanufaisha wazungu ilihali ndugu zao hata majosho ya kuoshea vijing'ombe vyao hawana,Ulimwengu ni mzalendo zaidi kuliko wale wanaoenda kwenye kampeni na bastola ni mzalendo zaid kuliko hata huyo Bashe ambaye amejifanya ndie alfa na omega wa UVCCM wakati hata historia ya UVCCM haijui anachojua ni kuwa loud speaker ya mafisadi.
  Uone aibu kwa kujifanya wewe ndio mtanzania zaidi wakati nawe ni mamluki

  Je Bashe anayeendesha UVCCM tumrudishe Somalia?mbona hujamwambie arudi kwao acha unafiki magamba weye
   
Loading...