Ulimtambua vipi kuwa huyu ndiye mwenyewe?

Mtihani na fimbo gumu kulifumbua Ruta. Tunajiingiza hivyohivyo na feki zetu, yote yatajulikana mbele kwa mbele.
How would I know? Ila najua with time I will know ukweli na feki.

Remmy mbona migongano ya kauli hapo...........huku unasema waenda mkichwamkichwa lakini bado unaamini maujanja unayo .......which is which............kama unayo hebu nifafanulie.....................nipo darasani nimetulizana vilivyo.............
 
Last edited by a moderator:
Hahaha...umejuaje Rutashubanyuma..namtafuta huyu tangu kipindi JF iko exile kwa ajili ya matengenezo...

Rogi ni kitu gani kilikufanya uvutiwe na Elizabeth Dominic? Haya matengenzo ya JF yaelekea yameibua mambo......................wengi hata FB walikuwa hawaijui sikuhizi naona ninajipatia marafiki kibao wa JF....something ought to yield now..................
 
Last edited by a moderator:
OOOOHHHHHHHH me sijampata ngoja nnikimpata ntakuja kusema nimempataje Rutashubanyuma

charminglady......kwa kuipima tu hiyo taswira ya avatar yako wewe siyo mtu wa kuhangaishwa na haya majambozi......tayari unaye ila umeamua kunificha tu..............................jinsi ambavyo magoti yalikugonga pale ulipomtia machoni..........................lol
 
Last edited by a moderator:
Rogi ni kitu gani kilikufanya uvutiwe na Elizabeth Dominic? Haya matengenzo ya JF yaelekea yameibua mambo......................wengi hata FB walikuwa hawaijui sikuhizi naona ninajipatia marafiki kibao wa JF....something ought to yield now..................

Yaani Rutashubanyuma ndio maana nikamwambia Rogi asubiri kwanza nitafakari maana naona naenda juu chini lakini sipati maana
 
Last edited by a moderator:
ULIMTAMBUA VIPI KUWA HUYU NDIYE MWENYEWE…..
(Getting to know her/him)

Hivi mwandani wako ulimtambuaje kuwa ndiye yeye?
Hivi ni maujanja yepi wewe uliyatumia kumpima yeye?
Ni vigezo vipi vilikutongoza hadi kujua umelamba dume?
Hivi ni vichocheo vipi vilikufanya uone ya kuwa umewasili?
Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu

Kauli yake mwenyewe huitia kitanzini na kuishibisha azma zake!
Aongeacho mara nyingi sicho kilichopo moyoni kwake wala!
Tabasamu lake lalenga kuijenga kauli ambayo si lazima iwe na kweli!
Kamwe kauli au hata tabasamu lake kuwa kioo cha moyo wake!
Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu

Kauli na taswira yake huoana na moyo wake masijala ya kukataa…
Pindi moyo wake umekuasi kata katu basi shabaha wewe hulengwa…
Bila haya au huruma jipu kukupasulia kuwa hakuhitaji nawe kulia..
Na kwa kufanya hivyo huwa kajitendea mwenyewe ubinadamu..
Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu

Ni mitihani ipi uliitumia kuupima moyo wake?
Hata kuridhia yeye ndiye na hakuna mwingineo?
Kama ulienda mkichamkichwa basi ilikula kwako!
Kama uliserereka na kauli au taswira basi wewe teja!
Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu

Dah mi labda ungeniuliza niliwatambuaje
 
Remmy mbona migongano ya kauli hapo...........huku unasema waenda mkichwamkichwa lakini bado unaamini maujanja unayo .......which is which............kama unayo hebu nifafanulie.....................nipo darasani nimetulizana vilivyo.............

Kimsingi sitajua, ila ndani ya mahusiano with time nitajua ukweli. At first naingia kichwakichwa, lol.
 
Ruta Mkuu, tunapokabiliana na wenzetu to be, hakuna fomula ya kuchanganya A+B+C+D= My real love. Mara nyingi sana kinakuwa kitu kimoja tu, tena kidogo sana, iwe kutoka pomaja kama KakaKiiza, iwe vidole kamacacico, iwe macho kamaFirstLady1, iwe si love at first sight kama decruca, iwe ujumbe tu kamakisukari.....hakuna formula, hakuna coat cut to fit all sizes. Binafsi siamini sana kwenye maneno mengi pekee, haya yanaweza kufurahisha masikio lakini sio moyo, moyo huguswa na cheche ya upendo ambayo hulipuliwa na hicho kitu kimoja kidogo ambapo kila shetani ana mbuyu wake.
 
i knw, i knw Rogi! i also like vidole virefu vya miguu kwa mwanaume, halafu avae sandles, looks mwahhhh! wacha nikutumie pic yangu ya vidole vya mikono kwa PM, subiri hapohapo usiende mbali, lolest!

Niasubir aise..ntafanayej jmn na mie nimeomba
 
Back
Top Bottom