Ulimpataje best friend wako?

Mimi nilikutana naye Jkt kwa mujibu wa sheria tulikuwa kombania moja sasa mbali na doso la Jkt bado kabla ya kuoga lazima nipige tizi boxer sasa yeye alikuwa anapenda sana hivyo akaomba niwe namfundisha fundisha ndio ikaanzia hapo.

Tukaja kukutana naye tena chuo tukawa washikaji hadi kuwa marafiki ambao tuko kindaki Ndaki sana hata baada kumaliza chuo licha ya umbali kidogo lakini bado tuko pamoja
Aluta Continua.
 
Just Mungu huleta watu kwako kwa kusudi. Huyu tulikutana chuo kikuu Na amekua ndugu yangu kabisa. Ukiacha wazazi Na ndugu zangu Wa damu ndo mtu anayenielewa Na harakati zangu.
 
Mimi tulikutana kwenye daladala tukiwa tunaenda interview basi la mwenge posta lilipofika moroco basi likaharibika na condakta akakimbia kurudisha nauli ilikuwa nipande likaharibikia kituoni.

Huyo kijana Akawa analia kuwa anaenda interview kule kule Mimi nlikuwa naenda kufanya interview hana nauli ingine nikambwambia usijali na mimi naenda nitakulipia. Kweli ikaja UDA tukapanda nikalipa

Tukafika posta tukashuka akasema nisubiri nakuja Toa photocopy za vyeti nipe nikatoa nikampa sikujali sababu muda wa interview ulikuwa bado sana na japo simjui sikujali sababu hakuchukua vyeti original

Baada ya muda akaja na mtu mzima pale nilikuwa akasema twende pembeni akaniambia maswali yote yatakayoulizwa interview na majibu

Kuingia nikamkuta nikajikausha kama simjui maswali yote nikakuta yaleyale nikayajibu vilevile nikapata kazi kumbe alikuwa mjomba wake

Hadi leo yeye simhesabu kama best friend bali ndugu
Mmmhh we jamaa muongo. Wewe siulipewa kazi na Kinana wewe?
 
Back
Top Bottom