Ulimi Mbona Umenisaliti? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulimi Mbona Umenisaliti?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by X-PASTER, Sep 25, 2008.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Sep 25, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Salaam nawatumia, wa bara na visiwani,
  Mwenzenu nimeumia, ulimi umenihaini,
  Tamko limetimia, kutenda naona soni,
  Ee wangu ulimi, mbona umenisaliti?

  Nilisema kwa dhihaka, nakutaka mwafulani,
  Naye akaniitika, kasogea barazani,
  Neno liliponitoka, hakuwa na ukinzani,
  Ee wangu ulimi, mbona umenisaliti?

  Mwili ulinitetema, joto kapanda mwilini,
  Natikisika kwa homa, palepale barazani,
  Bint akinitazama, huku atweta moyoni,
  Ee wangu ulimi, mbona umenisaliti?

  Sikuweza kuthubutu, kumkaribu chumbani,
  Akili ikawa butu, kama mfu kuzimuni,
  Rijali sikuwa kitu, macho kitazama chini,
  Ee wangu ulimi, mbona umenisaliti?

  Binti kazidi sogea, karibu na mlangoni,
  Macho akikodolea, wanaopita njiani,
  Pale alipokolea, akanisukuma ndani,
  Ee wangu ulimi, mbona umenisaliti?

  Nilitamani kulia, ili waje majirani,
  Naye akanitishia, nisilie asilani,
  Na ndani akaingia, akanivuta chumbani,
  Ee wangu ulimi, mbona umenisaliti?

  Nilishikwa na butwaa, hakika sikuamini,
  Ilikuwa ni fadhaa, kubwa iso na kifani,
  Binti yule akakaa, uchagoni kitandani,
  Ee wangu ulimi, mbona umenisaliti?

  Namshukuru Rabbuka, Rabbi aso na kifani,
  Binti aloyatamka, ni mambo mema ya dini,
  Kaka mimi nakutaka, tuwe sote maishani,
  Ee wangu ulimi, mbona umenisaliti?

  Hii kwenu changamoto, naomba yenu maoni,
  Nipeni mawazo moto, mwenzenu nifanye nini,
  Binti kwa kweli ni moto, tena msomi wa dini,
  Ee wangu ulimi, mbona umenisaliti?
   
 2. H

  Haika JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kiushairi siwezi kukujibu,
  Ila pole kwa ulimi, ulimi unaendelea kutusaliti wote siku kwa siku.
  siku hizi na vidole vya kubofya.
   
 3. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #3
  Sep 25, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Eksipasta tulia jukwaani umefika
  kilio kimesikika, wako ulimi ullivyokutenda
  Majuto kuendeleza, simanzi kukaribisha
  Ulimi hadaa, wengi umewagharimu

  Hisia kuzitoa, hukufanya baya jambo
  Binadamu kueleza, moyoni yanayowasibu
  Binti kumwona, moyoni uliguswa
  Ulimi hadaa, wengi umewagharimu.

  Kosalo ulielewe, dhihaka ulitumia
  Japo hisia ulijenga, za kupita kama moshi,
  Mzuka ulikupanda, ghafula ukaropoka,
  Ulimi hadaa, wengi umewagharimu.

  Ushauri nakupa, binti usimkwaze,
  Kwako amefika, hasilani hatanii,
  Nafasi anaitaka, upweke kuumaliza
  Ulimi hadaa, wengi umewagharimu.

  Kwako kashaingia, hapo amefika,
  Mlotenda chumbani, wazi hujayaweka,
  siri baki nayo, ila huyo usimmwage,
  Ulimi hadaa, wengi umewagharimu.

  Ukweli kuukabili, mkeo umempata,
  Ustaarabu kaonesha, mapepe hakutanguliza,
  Ukweli kauonesha, kwako katia nanga,
  Ulimi hadaa, wengi umewagharimu.

  Angekuwa mapepe, uchagoni asingekaa,
  Kanga moja kuja nayo, kitovu kukuonesha,
  Kitandani angefika, kihasara angekaa,
  Ulimi hadaa, wengi umewangarimu.

  Umrio waruhusu, shemeji kutupatia,
  Huyo mkubalie, maisha myapange,
  Hadaa ya ulimi, igeuke ngekewa,
  Huyo kwako amefika, mkeo twamwita.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Sep 27, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nashukuru muungwana, kwa pole kunipatia
  Ila mwezenu nanena, kauri ilinipotea
  meno yaliumana, ububu ukaniingia
  Mtoto ameumbika, tasema malaika

  Kila ninapo muona, maungo yananilegea
  akinikaribia sana, naishia kumwamkia
  maneno nakuwa sina, kauri inanipotea
  Mtoto ameumbika, tasema malaika

  Mzee wa Gumzo sikiza, si zihaka kutumia
  Binti kimuona kapendeza, hakika ninakwambia
  hakuna anaye mbeza, kila mtu amsifia
  Mtoto ameumbika, tasema malaika

  Mtoto kwa hakika, sifaze nitawambia
  hakika kakamilika, Mungu amependelea
  Ni zaidi ya malaika, umbo na yake tabia
  Mtoto ameumbika, tasema malaika

  Kiuangalia mwendo, anapo kukaribia
  Kama aso na fundo, Maungo memlegea
  pole pole mwendo, kwa pozi atakujia
  Mtoto ameumbika, tasema malaika

  Ananukia na udi, Kila anapo nipitia
  Udi wa mawardi, ndio anao tumia
  Nikimpata nitafaidi, Hakika nawambia
  Mtoto ameumbika, tasema malaika

  Nalipenda umbo lake, kama nyuki na maua
  Kamuumba Mola wake, kiwa mgonjwa upoa
  Nyororo ngozi yake, nikimpata tatulia
  Mtoto ameumbika, tasema malaika

  Naomba nimalizie hapa mbele sito endelea
  Msije mumzengee, Risasi nitawafyatulia
  Wala msimsogelee, onyo nisha waandikia
  Mtoto ameumbika, tasema malaika

  Ewe kiumbe wa shani, Nalipenda umbo lako
  Kila chozi machoni, laandika jina lako
  Maua bustanini, yanatoa harufu yako
  Naomba sinizaini, niurumie mwenzako

  Moyo wangu unadunda, kila uendako
  Mwenzio nakupenda, naomba niwe wako
  Ona nilivyo konda, kwa fikra zako
  Mungu anijaalie, niwe wako peke yako

  Kama mapenzi wazimu, mi sitaki nitibiwe
  Bora niwe chakalamu, nipige watu mawe
  Nipo ndani maamumu, tabibu wangu ni wewe
  Nipo naangamia, Kimuona napata kiwewe
   
Loading...