Ulimboka apandishwa mahakamani na takukuru kwa kosa la rushwa

mopaozi

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
3,301
519
Wadau nimehabarishwa kuwa Taasisi ya rushwa imewanasa golikipa na meneja wa timu ya Simba ya dar es salaam na kuwaweka chini ya ulinzi mkali wa njagu hao kabla ya kupelekwa mahabusu. Mwenye habari zaidi atujuze
 
Habari niliyoipata leo, ni kwamba Ulimboka amepandishwa mahakamani kwa kosa la hongo kwa mchezaji wa Mtibwa. Amepandishwa leo mahakama ya mkoa wa Morogoro na TAKUKURU mkoa wa Morogoro.

Source: Mahakama ya Mkoa Morogoro.
 
Habari ya uhakika ni kwamba mchezaji mpira ULIMBOKA amepandishwa leo mahakamani na TAKUKURU kwa kosa la hongo kwa mchezaji wa timu ya Mtibwa. Kesi hiyo imefunguliwa mahakama ya mkoa wa Morogoro.



SOURCE: MAHAKAMA YA MKOA MOROGORO.
 
Hii issue mbona ya Longil sana??
Yaani kipindi Ulimboka anatuhumiwa kwa Rushwa! Shaaban Kado alikua kipa wa mtibwa!!
Ulimboka alikua mchezaji huru mwaka ukaisha,
Akaja akachezea majimaji nao mwaka ukaisha,
Kwa sasa yupo Simba, walikua wapi hao TAKUKURU???
Eti alikutwa na kama laki 3 hivi ambazo mwenyewe alidai anakwenda kumlipa deni lake Kado!!
Wanawaachiaje wala rushwa wa mabilioni wanaotanua tu mjini?
 
TAKOHURU oops!!TAKUKURU ni mapuuzi sana yakiongozwa na Mkurugenzi wao.Wakitaka tuwaamini waanze na kina EL,EC,RA,JAIRO,SHIMBO,JK etc.
 
Hii taasisi bila kuvunjwa sasa hivi itaendelea kutafuna kodi zetu bila sababu yoyote, TAKUKURU ni genge la wahuni ambao kazi yao ni kubuni kesi dhaifu ambazo wao wenyewe wanajuwa hazima maana na hawawezi kuwa na ushahidi wa kushinda mahakamni.
 
Hawa takukuru siwapende! Yani imekua taasisi ya kisiasa kabisa! 'wanashughulika na kesi za wizi wa kuku'. Mbona wale twiga waliopelekwa uarabuni kupitia KIA hatujasikia lolote? Mkurugenzi wa wanyamapori pale maliasili vp? Kwa kifupi, hii taasisi it needs major reform!
 
hizi taasisi vipi takukuru.ewura.sumatra ni wizi mtupu sijui tanzania tunaenda wapi vyombo tunavyo na matatizo ndo yanazidi je visingekupo ingekuwaje?jaribu tafakari vina saidia nini?
 
hizi taasisi vipi takukuru.ewura.sumatra ni wizi mtupu sijui tanzania tunaenda wapi taasisi tunazo na matatizo ndo yanazidi je zisingekupo ingekuwaje?
 
mi nadhani wamekosa cha maana cha kufanya haswa kujikita kwenye rushwa ambazo hazituathir kitaifa moja kwa moja na kuziacha rushwa za waheshimiwa ambazo zinatufanya tz tuwe nchi masikini huku gap la walionacho na hawana likiongezeka!mi nadhani hii taasis ingeitwa "ya wala rushwa" 'a sio kama inavyoitwa sasa!pole Ulimboka jamaa wanataka waonekane wapo serious na kazi yao wakati wananchi hatuna imani nao tena.
 
Back
Top Bottom