Ulimboka alikuwa akamatwe na polisi kabla ya kutekwa

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
Ulimboka alikuwa akamatwe
na polisi kabla ya kutekwa

* Polisi walijipanga kumkamata kwa kudharau mahakama
* Walikuwa wanasubiri ‘arrest warrant’ toka mahakamani
* Wanaharakati wasema usalama walihusika na tukio

WAANDISHI WETU
Dar es Salaam

TUKIO la kinyama alilofanyiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari
Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, limeelezwa kuwachanganya polisi baada
ya kuwapo taarifa kwamba alitekwa wakati kukiwa na maandalizi ya
kukamatwa kwake na polisi kwa kukiuka amri ya mahakama.

Habari za ndani ya serikali zimeeleza kwamba, wakati polisi wakizubiri
amri ya mahakama ya kumkamata Dk. Ulimboka na wenzake, ndipo taarifa
za kutekwa kwake zikiwa zimeifikia polisi kabla ya kuokotwa porini
akiwa amejeruhiwa vibaya.

Uchunguzi wa KULIKONI umebaini kwamba kulikuwapo mpango wa kumkamata
Dk. Ulimboka na wenzake na kuwafikisha mahakamani kwa kukiuka amri ya
mahakama iliyozuia mgomo, lakini mpango huo ulikuwa ukisubiri kutolewa
kwa hati ya mahakama (arrest warrant).

"Baada ya madaktari wakiongozwa na Dk. Ulimboka kuendelea na mgomo
huku serikali ikisisitiza kwamba kulikuwa na amri ya mahakama ya
kuzuia mgomo huo, kulikua na maelekezo ya kutaka kukamatwa kwa
viongozi na kuwafikisha mahakamani lakini ikawa inasubiriwa hiyo
arrest warrant," anaeleza ofisa mmoja wa serikali aliyefahamu mpango
huo.

Hata hivyo, baada ya kutekwa kwa Dk. Ulimboka, vyombo vya dola na
serikali vimepata wakati mgumu kuunganisha hasa nini kilichotokea
kabla ya kutolewa kwa amri ya mahakama na nani amehusika na kitendo
cha kumkamata ama kumteka daktari huyo na kwa malengo gani.

Mkanganyiko na lawama umeelekezwa zaidi kwa vyombo vya dola kwa baadhi
ya watu kuvihusisha moja kwa moja na tukio hilo, huku ofisa mmoja
mstaafu serikalini aliyetumikia vyombo nyeti vya dola akisema:

"Hata kama (serikali) haijahusika moja kwa moja, itapaswa kulaumiwa
kutokana na uzembe wa kushindwa kumpa ulinzi ama kumfuatilia kwa
karibu Dk. Ulimboka hasa wakati huu ambako mgomo wa madaktari ulikuwa
katika hatua mpya na mbaya zaidi na inayohatarisha amani.

"Kwanini vyombo vya dola visimfuatilie Ulimboka popote alipo? kwanini
visimpe ulinzi kwa maana hii ambayo sasa inatokea, kwa kuwa ameonekana
ni mwiba dhidi ya serikali, kwa hiyo kama kuna mtu anataka kuivuruga
serikali ni nafasi nzuri ya kuitumia kwa kufanya yaliyotokea."

Tayari baadhi ya watu wakiwamo wabunge, wameanza kuhusisha tukio la
utekwaji wa Ulimboka na hujuma dhidi ya serikali, wakirejea baadhi ya
kauli za wanasiasa kwamba 'nchi haitatawalika', lakini ofisa huyo
mstaafu, alizidi kuvilamu vyombo vya dola kwa kutokuwa makini kutambua
na kuchukua hatua kabla ya jambo lolote kutokea.

"Sisi wakati wetu, tulikua tunapata taarifa ama kupata hisia kabla ya
tukio na tulikua tunachukua hatua, lakini kwa sasa wenzetu wako busy
na kutafuta fedha na kuhangaika na wanasiasa badala ya kufanya kazi za
kitaaluma. Kwa kweli hili ni janga la kitaifa maana kila taaluma
imepoteza uadilifu na umakini, si eneo moja tu," anasema mstaafu huyo
wa serikali.

Wakati hayo yakiendelea, kumeibuka tuhuma za vitendo vya 'kimafia'
vikiwagusa baadhi ya watumishi serikalini wakiwamo wale wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii na wizara nyingine.

Habari zimeeleza kwamba wakati bado uchunguzi wa nani hasa wanahusika
na unyama dhidi ya Dk. Ulimboka ukiendelea, kumekuwapo na hofu ya
kuwapo mipango ya 'kimafia' dhidi ya madaktari iliyokuwa ikiandaliwa
na watu ndani ya Wizara ya Afya wakishirikiana na wafanyabiashara na
watumishi kutoka idara nyingine.

Hata hivyo, hakuna aliyekuwa tayari kuzungumzia kwa kina kuhusu
mipango hiyo yua 'kimafia' baada ya mtoa habari wetu kusema hizo ni
taarifa za awali wakati uchunguzi wa kina ukiwa umeanza kwa kasi.

"Ni kweli kuwa kuna taarifa za kuwa baadhi ya watu ndani ya Wizara ya
Afya, waliopo sasa na walioondoka ambao wana chuki na madaktari na
ambao wana mikono mirefu hadi nje ya nchi ambao wanaweza kuhusishwa,
lakini kwa sasa kuna mambo mengi yanayochunguzwa kuhusiana na tukio
hilo. Tusubiri tusihukumu kabla," anasema mtoa habari wetu ndani ya
serikali.

Dk Steven Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na
kujeruhiwa sehemu kubwa ya mwili wake, kabla ya kutupwa katika msitu
wa Pande, nje kidogo ya jiji Dar es Salaam, msitu ambao ulipata
umaarufu mkubwa baada ya kuhusishwa na mauaji yaliyofanywa na polisi.

Daktari huyo ambaye amekuwa kiongozi wa mgomo wa madaktari unaoendelea
na ambao umeitikisa serikali, aliokotwa akiwa amefungwa mikono na
miguu akiwa katika hali mbaya na baadaye kukimbizwa Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili, katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI).

Dk. Ulimboka alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatano
katika klabu ya Leaders jijini Dar es Salaam, alikokuwa na wenzake
wawili na ilikuwa baada ya kukaa kwenye baa hiyo kwa muda, alianza
kujisikia vibaya tofauti na siku zingine.

Imeripotiwa kwamba daktari huyo aliteswa vibaya, ikiwamo kuumizwa
sehemu za siri, kuvunjwa meno kadhaa, mbavu na miguu.

Msitu wa Pande ulioko wilayani Kinondoni, ndiko wafanyabiashara watatu
wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva teksi wa Manzese Dar es
Salaam waliuawa na polisi mwaka 2006, mauaji ambayo yalimhusisha
aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Jinai Mkoa wa Dar es Salaam (RCO),
Abdallah Zombe.

Tayari Jeshi la Polisi limeunda jopo kuchunguza tukio hilo na Kamishna
wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova awaambia
waandishi wa habari kwamba tukio hilo ni la aina yake kutokea nchini
na kueleza kwamba jopo hilo ambalo linaongozwa na Mkuu wake wa
Upelelezi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ahmed Msangi.

Tayari suala hilo limeibua mjadala mara kadhaa ndani ya Bunge, huku
serikali kupitia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikisita kutoa tamko kama
ilivyoahidi, baada ya kuhofia kuingilia uhuru wa mahakama, huku baadhi
ya wabunge wakihusisha suala hilo na hujuma dhidi ya serikali.

Pinda alitangaza Bungeni jana kuwa serikali imesikitishwa na tukio
hilo na kuwa imeagiza ufanyike uchunguzi wa haraka kubaini
waliohusika.

Nao wanaharakati wa haki za binadamu wamesema kuwa tukio hilo lina
kila dalili ya kuwa na mkono wa serikali, kwani ni dhahiri kuwa
maafisa wa usalama wa serikali walikuwa wanafuatilia kila nyendo ya
Ulimboka na wangeweza kuzuia tukio hilo lisitokee kama wao
hawakuhusika.
Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Helen
Kijo-Bisimba, alisema kuwa ni vigumu kuamini kuwa maafisa usalama wa
serikali (state agents) hawakuhusika kwenye tukio hilo kubwa.

KULIKONI Ijumaa, Juni 29, 2012
 
Uongo mtupu, huu...!
Akamatwe kwa mlipi ?
Mbona mnajitahidi kujisafisha,
Acheni tume huru iundwe na ifanye kazi kiimpatially ndio tutajua mbivu.
ni zipi na mbichi ni zipior
Mtaunda story humu weee but ukweli utasimama!
 
...ni harakati za kuficha ukweli !! Hawa wanafikiri kila mtu ni masaburi kama wao...
 
Mafisadi hawana jipya la kuwaambia Watanzania tena.


MUNGU WETU! Tupe uongozi mwingine mbadala wa huu tulionao Mungu! Usitupite Mwokozi,badilisha mioyo ya hawa mafisadi waikimbie hii Nchi wenyewe!
 
Uongo mtupu, huu...!
Akamatwe kwa mlipi ?
Mbona mnajitahidi kujisafisha,
Acheni tume huru iundwe na ifanye kazi kiimpatially ndio tutajua mbivu.
ni zipi na mbichi ni zipior
Mtaunda story humu weee but ukweli utasimama!
Tume huru ipi mkuu? Hakuna tume huru iliyoundwa, tume iliyopo ni ya polisi ambao nao wanatuhumiwa kushiriki.
 
Tume huru ipi mkuu? Hakuna tume huru iliyoundwa, tume iliyopo ni ya polisi ambao nao wanatuhumiwa kushiriki.

Nimesema tume huru iundwe si hii ya polisi, ya polisi tayari watu wamekosa imani nayo.
 
magamba ni kiboko! sijawahi kupiga kura maishani! but 2015 mpaka last born wa mdogo wangu wa mwisho atapigia cdm! bora waje wengine! ccm hatuwataki tena! i hate this government jamani! wanachanganya maneno ili waonekane sio wao waliomteka na kumsulubu dr wa watu! pathetic!
 
"Walinipiga mateke ya mbavuni, wakati mwingine walitumia vitako vya bunduki, kila nilipokuwa najaribu kuangalia ninapokwenda nilishindwa," alisimulia Dk Ulimboka.

Alisema kuwa watu hao walimpeleka katika nyumba moja ambayo hakujua iko sehemu gani ambapo walimshusha na kuanza kumshambulia kwa mateke mfululizo kila sehemu ya mwili.
Wakati huo, wote walimshinikiza awaambie nani yupo nyuma ya mgomo wa madaktari.

"Tangu saa sita usiku mpaka saa 9:00 alfajiri walikuwa wananipiga tu, kuna wakati nilijaribu kukimbia wakapiga risasi juu nikasimama na sikuweza kukimbia tena," alisema Dk Ulimboka

Kila kitu kipo wazi.
 
mxxii napinga huu upuuzi kwa nguvu zangu zote, wanataka kujisafisha, hakuna hapa serikali imehusika moja kwa moja wala wasianze kutuletea uongo wa kitoto. Serikali mlitaka kumuua dr ulimboka full stop!
 
They r using much effort to cover it ... BUT simply that is the law of reversed effort ...!! Through it they will lead us to what they r trying to HIDE ...The hell will open loose .. No escape... much shame!!!
 
kwa kupigwa kwake cc sote tumepona

Umepona nini? wewe ni Pinda? Wewe ni Kikwete? wewe ni Riz moja?

Kama ni mtu wa Manzese utaponaje leo hii. Kweli Daktari anaweza kukuandikia dawa ya ugonjwa kwa kulazimishwa? Akiandika wewe utaaamini hiyo ni dawa?

Tusiige upuuzi wa wanasiasa ambao Rufaa yao iko India.
 
Kama nyumba hazijabadilika mimi nazifahamu nakumbuka tukiwa chuoni tulikuwa tunapelekwa huko na washikaji wa TISS,viongozi wakuu serikalini kujichana mikuku na mipombe unakuta jumba kubwa halina mtu kunawafayakazi tuu,wiki hii wanakupelekeeni nyumba hii mwezi ujao nyumba ile zipo nyingi tuu nazinafahamika

JK kabla hajaisambalisha nchi kuwa majivu akubali kuondoka madarakani serikali ya mpito iwekwe mpaka 2015 nchi imesambaratika na yeye kila siku inavyokwenda anazidi kuwa dictator poor him
 
Back
Top Bottom