Ulimboka adakwa kwa kutaka kumhonga Kado | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulimboka adakwa kwa kutaka kumhonga Kado

Discussion in 'Sports' started by Fidel80, Sep 29, 2010.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Waandishi Wetu, Dar na Morogoro

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe amekamatwa na polisi mkoani Morogoro akihusishwa na njama za kuhujumu mchezo wa Ligi Kuu baina ya Simba na Mtibwa uliopangwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri.Mshambuliaji huyo aliyetemwa na mabingwa hao wa soka wa Tanzania Bara msimu uliopita alikamatwa juzi na kuachiwa kwa dhamana jana asubuhi baada ya kuhojiwa na polisi wa kituo cha Manungu.

  Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa Ulimboka alikamatwa akiwa na Sh400,000 na alipohojiwa alidai kuwa alikuwa akienda kumlipa deni kipa wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kado.

  Polisi walithibitisha kukamatwa kwa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa, lakini wakasema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo unaendelea.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye aliliambia Mwananchi jana kuwa uongozi wa Mtibwa wilayani Mvomero ulimfikisha Ulimboka kituo cha polisi kwa tuhuma za kutaka kutoa hongo ya Sh400,000 kwa Kado ili acheze chini ya kiwango kwenye mechi ya leo.

  "Ni Kweli tumepokea taarifa hizo kuwa Ulimboka alifikishwa kituoni Mtibwa baada ya kujaribu kumpa Kado fedha kiasi hicho ili aachie mabao katika mchezo wao wa kesho [leo] dhidi ya Simba," alisema Kamanda Andingenye.

  ‘’Hata hivyo, Ulimboka amekana kuwa hakutaka kumrubuni kipa huyo na kusema ni kweli alikwenda Mtibwa akiwa na kiasi hicho cha fedha kwa lengo la kumlipa deni mchezaji huyo kwa sababu (Kado) ni rafiki yake ndani na nje ya mpira.

  "Alitwambia kwamba anachofahamu katika siku za nyuma yeye alimwazima Kado kiasi hicho cha fedha na alifika Mtibwa kwa kuwa wakati huo ulikuwa muda sahihi wa kwenda kumlipa kwa kuhofia kuwa kama angechelewa, angeweza kumuudhi."

  Kado amekuwa mmoja wa wachezaji nyota walioibukia katika siku za karibuni na alionyesha kiwango cha juu wakati Taifa Stars ilipolazimisha sare ya bao 1-1 na Algeria mjini Blida.

  Kipa huyo anatarajiwa kusimama langoni Oktoba 9 wakati Stars itakapoikaribisha Morocco kwenye mechi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2012.

  Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Mtibwa Sugar ziliarifu Mwananchi jana kuwa walipokea taarifa kutoka kwa Kado akieleza kuwa Ulimboka alikuwa akitaka kumpatia fedha ili aiachie Simba katika mchezo wa leo na ndipo wao wakamshauri ampe muda ili wafike mahali (Manungu) wakiwa na polisi na ndivyo alivyofanya.

  Alipoulizwa kuhusu suala hilo, afisa habari wa klabu ya Simba, Clifford Ndimbo alikana klabu yake kuhusika na tuhuma hizo na kudai kuwa kuna watu wanataka kuwavuruga ili wafanye vibaya katika mchezo huo.

  ''Sisi hatuhusiki na tuhuma hizo... kwanza Ulimboka aliondoka Simba kwa ugomvi, iweje leo uongozi wetu umtume atoe rushwa? Habari si za kweli,'' alisema Ndimbo.

  Lakini tangu habari hizo zilipofumuka jana asubuhi wadau mbalimbali wa Simba, wakiwemo waandishi watano wa habari za michezo walikuwa wakipiga simu kujaribu kushawishi habari hiyo isichapishwe na Mwananchi kwa madai kuwa itashusha heshima ya klabu hiyo.

  Tukio hilo limetokea wakati Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiwa limetangaza kuwafungia waamuzi wanne kwa makosa ya kuvurunda mechi walizochezesha za Ligi Kuu Bara zinazoihusisha Simba, Yanga, Azam na Kagera. Klabu za Azam na Arusha FC ziliwahi kulalamikia uamuzi wa mechi zao dhidi ya Simba na Yanga zikidai uamuzi ulilenga kuzibeba timu hizo kongwe nchini.

  Ulimboka adakwa kwa kutaka kumhonga kipa
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Dah hii imeishushia hadhi Simba mwaka jana gemu nyingi walikuwa wanafanya hivi
   
 3. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  Hii habari imekaa ki-majungu-majungu na kuichafulia hadhi klabu yetu...mkuu unaanzisha thread na kuwa wa kwanza kuichangia huku ukuwa na muelekeo wa ki-komandoo wa jangwani...anyway..SIAMINI KAMA TIMU YA SIMBA INAWEZA KWENDA KUMUHONGA MTU KAMA KADO NA KWA KUPITIA ULIMBOKA AMBAYE ALIKUWA MCHEZAJI WA SIMBA....katika dunia ya utandawazi ya leo ni kazi ndogo sana kumpa mtu pesa..kuna ZAP, M-PESA, TIGO PESA NA BANK ACCOUNTS...kwa hiyo ilikuwa ni suala la mtu kuongea na kado na kumtumia pesa kwa njia hizo walla haihitaji mtu kusafiri kilomita 1000 kumpelekea tshs 400,000/=...HAYA NI MAJUNGU NA UPUUZI...kwa hiyo tuamini kila timu inayoshindwa na simba wamehongwa?...therefore hata polisi dodoma walimuhonga kipa wa simba??.... na azam wanavyofungwa nao kipa wao anakuwa amehongwa??....BUSARA ZICHUKUE MKONDO WAKE
   
 4. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ndiyo maana mpira wa tz hauendelei!!
   
 5. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Unamsakama bure Fidel80! Hajaanzisha yeye thread hii bali ame-quote Mwananchi. Kwa hiyo ana haki ya kuijadili. Usitetee uozo, hata kama ww ni simba. Nyie ndiyo mnadumaza mpira wa tz
   
 6. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa huwa yuko so pumbadi sana ni bora umesema wewe
   
 7. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  nadhani huelewi hata mpira..kwa taarifa yako duniani kote rushwa zimejaa michezoni...ila cha msingi ni kuwa habarii hii ni "fabrications" za kipuuzi na u-simba na yanga usiokuwa na msingi....

  Je ulimboka anasema ametumwa na simba??...je simba hawana jinsi nyingine ya kumpatia kado pesa mpaka wamtume ulimboka?...je kila mechi waliyofungwa mtibwa alihongwa kado?...je kila mechi waloshinda simba walihonga magolikipa wa timu pinzani?....baada ya hayo..je mechi zote wanazoshinda yanga tuamini walitoa hongo??...

  Tuache upuuzi tuangalie mambo yanayorudisha nyuma soka letu ...na rushwa sio moja ya vitu vinavyorudisha nyuma mpira...ingekuwa ndivyo basi juventus ya italy ingekuwa marehemu kaburini na soka la italy lingekuwa limekufilia mbali...lets tok senses now we r big boys n girlz here

   
 8. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  hapa hatujadili "watu"..tunajadili issues... jaribu kuonyesha "UKOMAVU WA AKILI YAKO" atlest ujipatie heshima kwa jamii
   
 9. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  ofcuz haundelei kwa sababu wachezaji hawalipwi vizuri na wanakopeshana viji-pesa na kulipana kabla ya mechi...ila kama unamaanisha rushwa michezoni...naomba kupingana na wewe...rushwa ilikuwapo, ipo na itaendelea kuwapo popote pale duniani penye ushabiki na ushindani katika michezo yote... rushwa zipo hadi kwenye boxing, basketball, etc...ila uendelevu wa michezo unatokana na "proper training" na "personal/individual talent development"...chini ya hapo michezo itakufa na kutoendelea duniani kote... ni maoni tuu wadau
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Kwa watu waelewa kama sisi, tumeshakuelewa sana mheshimiwa....Thibitisha kwa hapa chini:  The Following User Says Thank You to Who Cares? For This Useful Post:

  Asprin (Today) ​
   
 11. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
   
 12. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
   
 13. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  WRONG. Rushwa ni moja ya vitu vinavyorudisha mpira nyuma na miongoni mwa culprit wakubwa kwa mpira wetu wa hapa nchini ni hivi vilabu vinasemekana kuwa 'vilabu vikubwa vya soka nchini' vikishirikiana na Marefa kutaka ushindi hata pale wasipokuwa na uwezo. Ndio maana wanapokwenda nje hawafiki mbali kwa sababu hapa nyumbani ushindi waomara nyingi unatokana na fitna za soka na sio uwezo wao wakutandaza kandanda.
  Afadhali ungesema tuwe wavumilivu na tusubiri 'gemu' hili litakavyoendelea. Kado amedai kuwa Mwakingwe alikuwa anamletea Laki 400,000/= ili acheze chini ya kiwango watakapocheza na Simba. Mwakingwe amedai kuwa Kado ni rafiki yake alikuwa anamrudishia hela aliyomkopa!! Hivirafiki yako asijue kuwa unamrejeshea hela yake nabadala yake akurupuke kudai kuwa unampelekea rushwa???
  Ingekuwa vyema sana kama Mwananchi ingetaja majina ya hao waandishi watano wanaodaiwa kulipigia simu gazeti hilo ili kuomba story hiyo isitoke kwa sababu 'itaidhalilisha Simba'! Wawataje. Sio vizuri kuficha ugonjwa.
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,770
  Trophy Points: 280
  kama ushachana passport chungulia basi hata kwenye website za magazeti ya nyumban usikimbilie kulaumu
   
 15. s

  smp143 Member

  #15
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  uwongo huo
   
 16. K

  King kingo JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duh kweli siku za mwizi arobaini....kila siku kuhonga leo wamebambwa kazi kweli kweli....
   
 17. K

  King kingo JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kama unakubali rushwa zimejaa michezoni mbona hii unataka kuikataa..?????
   
 18. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  kumbe ngebe zoote zile ndani yake kuna rushwa?
  sasa hizo hela si mngetumia kuzibua vyoo vya jengo lenu kariakoo ambalo kwa sasa watu wamekuwa wakinya kwenye mifuko na kutupa hovyo kutokana na uchakavu wa vyoo vya jengo?
   
Loading...