Ulikuwa wapi wakati kifo cha Mwalimu Nyerere kimetangazwa?

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
7,442
10,233
Wakuu Salaam:

Leo Oktoba 14 inatimia miaka 21 tangu muasisi wa Taifa hili atutoke duniani.

Wakati kifo chake kimetangazwa, binafsi mimi sikua na uwelewa kuhusu hilo hivyo sijukujua chochote kinachoendelea. Mwaka wa 2000+ ndiyo naelewa sasa.

Kuuliza uliza, kipindi kile tulikua Moshi wakati hiyo taarifa imetoka na ilitangazwa usiku.

Ulikuwa wapi ulipopata habari hizi?
 
Nilikuwa darasa la tatu, Ngarenaro Primary School Arusha.

Eti walimu wakawa hawafundishi, tukawa tunaimba tu nyimbo za mamombolezo. ilinishangaza sana kwa kweli. Nilivopata akili vizuri ndo nikajua kumbe ulikuwa ni upumbavu wa aina yake, yaani mtu kufa inahusika vipi na walimu kutokuongia darasani karibu mwezi mzima?
 
Nilikuwa Breki ya nanunua barafu/icecream. Muuza icecream ambaye had I juzi namuona akiwa anaziuza alisikia kwenye redio yake akatuambia.

Shule ilifungwa tukaenda kwa Mzee kolo kuangalia maombolezo. Nililia mno japo nyerere nilikuwa sina ABCD zake sana
 
Siku kama ya leo marehemu Ben alitangaza, saa nne asubuhi kuwa Mwalimu ametangulia. Tulikuwa darasani, radio ya mchoma chipsi pembeni ya darasa letu ndo ilitupasha habari, kipindi kile ukisikia wimbo wa Taifa unapigwa redioni, mnakuwa shupavu kutaka kujua nini kimetokea, hivyo tulivyosikia tu huo wimbo, wote kimyaaa kusikiliza.

Ila wengi tulioishi maeneo ya karibu na kwa mwalimu tulishajua mambo yameharibika kule kabla ya tarehe tajwa, barabara ya kwenda kwa mwalimu ilikarabatiwa, walianza kukarabati nyumbani kwake, magazeti nayo yakiripoti; "Kawawa arudi na siri nzito" akitoka kumuona mwalimu St Thomas, mara Mwalimu apumulia mashine kwa 100%, magazeti ya Alasiri na Dar Leo yakiripoti hivyo, mara mortuary ya Muhimbili inakarabatiwa. Yote hayo yalikuwa kati ya tarehe 1 na 10 mwezi wa 10.

Nilikuwa darasani
 
Nilikuwa darasa la tatu, Ngarenaro Primary School Arusha.

Eti walimu wakawa hawafundishi, tukawa tunaimba tu nyimbo za mamombolezo. ilinishangaza sana kwa kweli. Nilivopata akili vizuri ndo nikajua kumbe ulikuwa ni upumbavu wa aina yake, yaani mtu kufa inahusika vipi na walimu kutokuongia darasani karibu mwezi mzima?
Yule si alikua na hadhi ya kipekee hapa kwetu, walivyosimamisha masomo ilikua sawa...

Ila maisha yako kasi, Mkapa kaondoka kumekua tofauti, maisha yamebadilika.
 
Siku kama ya leo marehemu Ben alitangaza, saa nne asubuhi kuwa Mwalimu ametangulia. Tulikuwa darasani, radio ya mchoma chipsi pembeni ya darasa letu ndo ilitupasha habari, kipindi kile ukisikia wimbo wa Taifa unapigwa redioni, mnakuwa shupavu kutaka kujua nini kimetokea, hivyo tulivyosikia tu huo wimbo, wote kimyaaa kusikiliza.

Ila wengi tulioishi maeneo ya karibu na kwa mwalimu tulishajua mambo yameharibika kule kabla ya tarehe tajwa, barabara ya kwenda kwa mwalimu ilikarabatiwa, walianza kukarabati nyumbani kwake, magazeti nayo yakiripoti; "Kawawa arudi na siri nzito" akitoka kumuona mwalimu St Thomas, mara Mwalimu apumulia mashine kwa 100%, magazeti ya Alasiri na Dar Leo yakiripoti hivyo, mara mortuary ya Muhimbili inakarabatiwa. Yote hayo yalikuwa kati ya tarehe 1 na 10 mwezi wa 10.

Nilikuwa darasani
Mkuu kweli wewe ulishuhudia mengi wakati ule.
 
Kwa yanayoendelea nchini chini ya CCM wala sina haja ya kukumbuka chochote ndani ya watu wa CCM.

Uwe muasisi, uwe kada, uwe shabiki n.k

Twende na Lissu.
 
Wakuu Salaam:

Leo October 14 inatimia miaka 21 tangu muasisi wa Taifa hili atutoke duniani.

Wakati kifo chake kimetangazwa, binafsi mimi sikua na uwelewa kuhusu hilo hivyo sijukujua chochote kinachoendelea. Mwaka wa 2000+ ndiyo naelewa sasa.

Kuuliza uliza, kipindi kile tulikua Moshi wakati hiyo taarifa imetoka na ilitangazwa usiku.

Ulikuwa wapi ulipopata habari hizi?
Nashukuru nilikuwa napenda kusikia taarifa ya habari itv iliyokuwa ikitangazwa kwa lugha ya kiengereza kuhusu afya ya babu kule alikokuwa uingereza.
Ni Langfered masako na sijui yuko wapi kwa sasa.
Utasikia.
The condition of mwalimu julius kambarage nyerere who has been hospitalised at st Thomas is said to be bad since today evening.
He has been head operated in order to restore his health condition with negative success.
All the people are ordered to pray for Mwalimu as ordered by President Mkapa.
Tommorow evening our president will fly to London to see his condition.
Oooh hazikuisha siku babu huyooo katembea.

Rip Our babu Nyerere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu Salaam:

Leo October 14 inatimia miaka 21 tangu muasisi wa Taifa hili atutoke duniani.

Wakati kifo chake kimetangazwa, binafsi mimi sikua na uwelewa kuhusu hilo hivyo sijukujua chochote kinachoendelea. Mwaka wa 2000+ ndiyo naelewa sasa.

Kuuliza uliza, kipindi kile tulikua Moshi wakati hiyo taarifa imetoka na ilitangazwa usiku.

Ulikuwa wapi ulipopata habari hizi?
Shule,darasa la 4.
 
Nilikuwa wakati huo nina umri wa miaka 44 tumekaa na mzee mmoja wakati huo alikuwa na umri wa miaka 55 bar tunakunywa baada ya kusikia tu yule mzee alilia kama mtoto mdogo unavojua Konyagi ukilewa kisawasawa mtu akikuambia tu wewe mpumbavu unaweza lia machozi sasa mimi japo nilikuwa nakunywa beer niliingiwa na simanzi pia nikalia.
MUNGU AMUWEKE PEMA RAISI WETU BABA WA TAIFA
pia mungu amuweke pema yule mzee niliyekuwa naye maana naye alifariki mwaka huu January akiwa na 76
 
Back
Top Bottom