Ulikuwa wapi siku kifo J. Nyerere (baba wa Taifa) kinatangazwa?

Safety last

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
4,227
1,389
Nakumbuka ilikuwa siku ya jumanne niko kidato cha pili majira ya saa 4:30 tuko darasani na mwl wa Archtectural drawing ,ilikuwa ni mlinzi wa shule ndio alikuwa anazunguka kwenye corridor za madarasa na kusema nyerere ameaga duniani huku yuko na redio ikipiga wimbo wa taifa then akaja mkapa kulìhutubia taifa. Wewe ulikuwa wapi wakati huo ?
 
Kunatakiwa kuwe na jambo la kitaifa ambalo litafanyika kote nchini kumuenzi nyerere kama kusafisha mazingira au kupanda miti.
 
Umenikumbusha mbali sana! Nilikuwa chuoni mwaka wa pili. Tulikuwa tunafanya test ya Construction Technology kwenye darasa ambalo lilikuwa karibu na Laboratory ya Soil ambapo pana TV. Mwalimu aliyekuwa anasimamia mtihani alitoka nje kwa dk kama tano hivi. Alirudi ghafla na kutuambia Nyerere kafariki. Wote tulitoka fasta utadhani tuliambiwa jengo linaungua tukaelekea Lab tukakuta wimbo wa Taifa unapigwa ndio Mkapa akatutangazia kifo huku machozi yakimtoka! Mtihani uliahirishwa automatically tukaufanya baada ya wiki!
 
Yeah ,kweli umekumbuka mbali.
 
Kwakuwa kwangu Nyerere alikuwa mtu wa kawaida, sikuhifadhi kumbukumbu za kifo chake kwenye kichwa changu.
 
nilikuwa shule nakumbuka kama sikosei ilikuwa lunch time mara wimbo wa taifa wanafunzi tukatega masikio ikafatiwa na sauti ya mkapa hakika ilikuwa ni vilio kwani tuliamini ilikuwa mwisho wa tanzania..
 
Nilikuwa form 2 na siku hiyo kulikuwa na mahafari ya kidato cha nne nilikuwa mwanakamti na pia nilikuwa kwenye kwaya na maigizo, nakumbuka walimu hawakutuambia mapema ili mahafari isiahirishwe. Mara mwisho nilikuwa nimwona kwenye msiba wa Adam Sapi pale Kalenga. Nimekumbuka mbali sana.
 
Nilikuwa Form 3 sikumbuki sehemu niliyokuwa wakati huo, lakini kila mtu alisisimka kwa huzuni na kujaa uoga. Ulikuwa msiba wa kitaifa kweli, naweza haijawahi kutokea tena kwa watanzania kuungana kuomboleza kama kipindi hicho.
 
Dah umenikumbusha mbali sana mbali sana...miaka 12 iliyopita...nilikuwa kidato cha pili seminarini,tujiandaa kwa jiving na nyimbo za kuwaaga form four...mgeni rasmi mtarajiwa angekuwa Askofu TARCISIUS NGALALEKUMTWA(Jimbo katoliki Iringa),ghafla Gombera(Rector) wetu akaamuru kengele igongwe kitu ambacho ni adimu sana,ukiona ivo ujue mtu anafukuzwa seminar kwa utovu wa nidhamu...na mim nilikuwa na kesi ya kuiba maparachichi na mapera bustanin kwa Masista Kamadolesi,nkajua ndo safari ya home....HP wetu ambaye sasa ni Padri wa kanisa katoliki uko Parelmo Italy akampa Rector nafasi...akatangaza kwa Huzuni kuondokewa kwa baba wa Taifa...wote tukapoa...huzuni ikatanda...Tulikuwa na Tv room inashka DSTV tu!Tukafunguliwa chanel ya SABC-AFRICA,Wakawa wanatoa wasifu,hstoria ya mwalimu..24hrs...na siku ya mazishi Tulitazama kupitia SABC-AFRICA ya South Africa...nakmbuka mengi sana,lakn nimewakmbuka zaid marafik zangu waloamua kuendelea na Upadri..weng wako nje ya nchi wakihubiri Injili...Ni mda mrefu!!R.I.P J.K.NYERERE
 
Nakumbuka nilikua darasa la5 shule moja ya boarding huko arusha.at that time tulikuwa porini tunakata kuni za shule,kuna baadh yetu walikuwa na viredio vidogo vile!ndo walitupa taarifa!it was so sad kwakweli.
 
mzee safety utakuwa my age mate! Nilikuwa kidato cha pili though sikumbuki mwalimu aliekuwa class. Wanafunz tulitoka kwenda kuchungulia kinachojir kwenye Tv pale staff room. Nilisikitika sana kwani tulikuwa tunasikia akifa nyerere kutakuwa vita! Lol, tulitaharuki kweli
 
Nakumbuka siku hiyo nilikuwa hospitali ya mount meru nimeenda kumuangalia mke wangu alikuwa kajifungua mtoto wangu wa nne.
Kwa kumbukumbu mtoto yule nilimwita Julius.
 
Nilikuwa Mikicheni B kwenye mabwawa ya maji machafu, nikasikia kale kamlio ka ajabu ka Redio Tanzania, ilikuwa mida ya saa nne, ndipo Mkapa akatangaza kifo cha Mwalimu
 
Kunatakiwa kuwe na jambo la kitaifa ambalo litafanyika kote nchini kumuenzi nyerere kama kusafisha mazingira au kupanda miti.

wazxo zuri sana, kwa jinsi tunavyoteketeza mit, bora tujikite kupanda miti kwani mwl. alisisitiza uhifadhi wa mazingira/rasimali za taifa kwa manufaa ya kizazi cha baadae.
 
kipindi anafariki, nilikuwa darasa la saba siku chache kabla ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi. Kifo chake
 
mzee safety utakuwa my age mate! Nilikuwa kidato cha pili though sikumbuki mwalimu aliekuwa class. Wanafunz tulitoka kwenda kuchungulia kinachojir kwenye Tv pale staff room. Nilisikitika sana kwani tulikuwa tunasikia akifa nyerere kutakuwa vita! Lol, tulitaharuki kweli

yeah bro inaweza ikawa we are age mate ,good and sad to remember!
 
wazxo zuri sana, kwa jinsi tunavyoteketeza mit, bora tujikite kupanda miti kwani mwl. alisisitiza uhifadhi wa mazingira/rasimali za taifa kwa manufaa ya kizazi cha baadae.

hakuna mwongozo wowote wa kitaifa nini kifanyike kama kumbukumbu ,watu wanakaa nyumbani au wanazunguka zunguka tu,at the end siku ya Nyerere itakosa mashiko sababu inamotivate uvivu.
 
Back
Top Bottom