Ulikuwa wapi kabla haujaja duniani kama kiumbe hai? Umewahi kutaka kujua ulipotoka?

Kabla ya kuzaliwa wewe hukuwa mwanadamu bali ulikuwa mbegu, nusu kwenye korodani za baba yako na nusu kwenye ovari za mama yako.

Baada ya tendo la ndoa kufanyika ndipo hizo mbegu mbili zikaungana na wewe ukatengenezwa tumboni mwa mama yako.

Hii maana yake ni kwamba kama baba yako angelala na mwanamke mwingine basi wewe usingekuwepo kabisa hapa duniani.
Jibu konki kabisa hili
 
Tunatokea tumboni baada ya spend kukutana na yai, Sasa je, Kama utapata memory za nyuma , Basi ujue umepewa nafsi ya mtu aliyewahi kuishi hapo kale
 
Yoda naomba nikuulize swali ukijibu ndio naweza kuendelea na mjadala.

Unapata hasara gani usipojua ulikotoka? Kwanini uumize kichwa wakati hakuna adhabu utakayopata usipojua mwanzo wako?

Unachopaswa kuhangaikia kwa sasa ni mwisho wako tu. Sababu ndio una maumivu
 
Kuna adhabu utakayopata usipojua mwisho wako?
Kwa nini watu wanaumiza vichwa vyao kutaka kujua watakapokwenda baada ya kufa?

Ulipomalizia mwishoni nimecheka sn..kuna Mwamba somewhere anakucontrol km tu vile wewe unavyolicontrol GTA 🤔🤔

Lakini game mbn haliko autopilot km the way Mimi na wewe tulivyo? Consciousness yetu Sisi inatoka wapi mkuu Stephen Chelu

Mkuu, haya mambo kuna kipindi niliyawaza sana hadi nikahisi naweza kurukwa na akili, yanavuruga sana ubongo, anyway turudi kwenye mada maana hakuna namna, inabidi tufikiri ili kuutafuta ukweli.

Umesema kuwa sisi hatoko auto piloted kama ambavyo ‘tunahisi’ ma-gemu yalivyo kwa kuwa sisi tuna consciousness, hivyo umehoji consciousness yetu inatoka wapi. Hii hoja yako naweza kujaribu kuijibu katika namna mbili. Namna ya kwanza ni kwa kutumia key term uliyoitumia (consciousness) na namna ya pili ni kuangalia miktadha wa hoja yako kwa kulinganisha uhuru katika utendaji kati ya sisi binadamu na ma-gemu. Na pia nisisitize kuwa huu ni mtazamo binafsi tu.

CONSCIOUSNESS

Kama sote tujuavyo kuwa consciousness ni hali ya kujitambia au kuhisi uwepo wetu na vitu vinavyotuzunguka. Kwa maana hiyo naamini mimi Stephen Chelu nipo duniani kwa kuwa najihisi kuwa nipo, lakini je, mimi stephen chelu nipo kweli?

Twende kidogo kidogo kujaribu kuling’amua hili..

Kwa mfano nikienda sehemu ambayo watu hawanifahamu, watu wataniona lakini hawatanifahamu mimi ni nani na hivyo pengine nitatakiwa kujitambulisha. Hivyo nitasema; “Jina langu ni Stephen Chelu” au “Mimi ni Stephen Chelu”.

Sentensi hizi mbili hazifanani kabisa kwa kuwa zinamaanisha vitu viwili tofauti. Sentensi ya kwanza inaonyesha mimi ni huyu ambaye natumia utambulisho wa Stephen Chelu kwa maana ya kwamba, mimi nipo ila natumia jina la Stephen Chelu kutambulisha uwepo wangu kwa hiyo mimi si jina langu.

Sentensi ya pili inaonyesha kuwa mimi ni Stephen Chelu kwa maana ya kwamba jina langu ndiye mimi. Lakini je, jina langu ndiye mimi? Jibu ni hapana kwa sababu mimi naweza kuamua kujiita Idd Suleyman na bado nikaendelea kuwa mimi yule yule. Kwa hiyo ni wazi kwa kuwa mimi si jina langu, naweza kubadili jina ila mimi nikabaki kuwa mimi yule yule.

Mfano mzuri ndugu yangu wa Jf, the big superstar in town Don Nalimison, hapo mwanzo alikuwa anaitwa Deogratius Kisandu, lakini baadae akaenda mahakamani kubadili jina sasa hivi anatumia jina la Don Nalimison lakini yeye ni yule yule, anaendelea kutoa mapini makali kama kipindi kile anaitwa Deogratius Kisandu.

Tunaendelea..

Kwa kuwa tumegundua jina siyo mimi bali ni utambulisho wangu mimi, tunaendelea kutafuta huyo mimi mwenyewe ni yupi. Wakati najitambulisha nilitoa sauti, kwa hiyo pengine sauti yangu ndiye mimi mwenyewe. Je, ni kweli sauti yangu ndiye mimi? Sauti hii niliyoitoa ina sifa Fulani ambazo zinatofautiana na sauti nyingine zote kiasi watu wakiisikia tena watajua ni mimi ndiye ninayeonygea na si mtu mwingine yeyote.

Lakini fikiri, labda nimepata ugonjwa ambao umeathiri mfumo wa sauti na kufanya sauti ibadilike, je kubadilika kwa sauti kutafanya mimi niwe mwingine? Jibu ni hapana, mimi nitaendelea kujihisi ni mimi yuleyule niliyebadilika sauti. Na hata watu wakinisikia naongea watasema “Chelu, sauti yako imebadilika sana” Kwa hiyo sauti yangu siyo mimi bali ni kitu ambacho mimi nakitoa ili tuweze kuwasiliana.

Lakini kwa kukazia zaidi kuwa sauti siye mimi, naweza nisijitambulishe kwa sauti bali nikaamua kuchukua karatasi na peni na nikaandika jina langu. Kwa hiyo pasipo sauti yangu, watu watasoma ile karatasi na kutambua mimi ni nani.

Sasa kama mimi si jina langu wala si sauti yangu, mimi ni nini? Labda kwa kuwa sauti niliyoitoa ilitoka baada ya mimi kufikiri, labda mimi ni fikra zangu. Kama tujuavyo fikra huzaa mitazamo mbalimbali ambapo mitazamo hiyo hupelekea kufanyika kwa maamuzi mbalimbali pia. Sasa katika mitizamo mingi niliyonayo hebu tunyofoe mtazamo mmoja ili tuone kama mimi ni hizi fira zangu.

Mimi ni shabiki wa Yanga na watu wangu wa karibu wote wanajua hivyo. Kwa hiyo moja ya utambulisho wangu ni kuwa mimi ni shabiki wa vyura fc aka utopolo. Je, ikitokea nikabadilika kifikra na kupata mtazamo ambao utafanya nibadilishe maamuzi yangu na kuwa shabiki wa Simba; je, nitakuwa nimebadilika na kuwa mimi mwingine? Jibu ni hapana, mimi nitaendelea kuwa yuleyule ila nitakuwa nimetoka utopoloni na kwenda kwenye wa kimataifa. Kwa hiyo mimi si hizi fikra zangu, naweza kubadilika kifikra na nikabaki kuwa mimi yuleyule.

Sasa mimi ni nini? Labda kwa kuwa wakati najitambulisha nilitumia mdomo ambao ni sehemu ya kichwa ambacho kimeungana na sehemu nyingine za mwili na pia kwa kuwa jina niliandika kwa kutumia vidole vilivyopo mkono, ambao mkono huo nao umeunganika na sehemu nyingine za mwili na pia kwa kuwa fikra zinatoka kwenye ubongo ambao upo ndani ya kichwa ambacho kama nilivyosema hawa mwanzo, kimeungana na sehemu nyingine za mwili, Labda basi mimi ni huu mwili unaoonekana.

Je, ni kweli mimi ni huu mwili?

Tukuchukulie labda kuna siku nikaanza kuumwa. Nitasema “Mwili wangu unauma” au nitasema “Najihisi kuumwa”.

Sentensi hizo mbili hazifanani kabisa kwa kuwa zinamaanisha vitu viwili tofauti. Sentensi ya kwanza inaonyesha kuwa huu mwili si mimi bali mimi ni yule mwenye huu mwili hivyo inakanusha kuwa mimi si huu mwili unaoonekana. Sentensi ya pili inaonyesha kuwa mimi ni huu mwili na ndiyo maana nikasema ‘najihisi kuumwa’. Basi tuchukulie kuwa sentensi ya kwanza si sahihi na tukubaliane na sentensi ya pili inayosema mimi ni huu mwini unaoonekana.

Basi ikatokea mimi nikazidiwa na ugonjwa, nikafa. Taarifa zitakuja humu Jamiiforums kuwa ‘Member mwenzetu Stephen Chelu amefariki dunia’. Kauli hiyo bado inakubali kuwa mimi ni ule mwili, na kwa kuwa mwili hauna tena sifa za kuwa hai basi ni mimi huyo ndiye niliyefariki dunia. Kwa hiyo hadi hapo bado tunakubali kuwa mwili wangu ndiye mimi.

Taratibu za mazishi zinaanza, nawekwa kwenye jeneza, watu wanapiga picha na kuzipost humu Jamiiforums kuleta update ya kinachoendelea kwenye mazishi yangu. Caption ya chini ya picha ya jeneza langu itaandikwa “Jeneza lenye mwili wa Stephen Chelu”. Utata unaanzia hapa, kumbe kilichomo ndani ya jeneza si mimi, bali mwili wangu, kwa hiyo mimi siyo huo mwili. Kama kilichopo ndani ya jeneza siyo mimi bali ni mwili wangu, ina maana mimi bado nipo.

Sasa kama mimi siyo jina langu, kama mimi siyo sauti yangu, kama mimi siyo mwandiko wangu, kama mimi siyo fikra zangu na kama mimi siyo mwili wangu; je, mimi ni nini na nipo wapi?

Hivyo utagundua kuwa mimi sipo popote bali mimi najihisi nipo kwa sababu ya vitu mbalimbali (mwili, sauti, fikra nk) ambapo kwa pamoja vinatengeneza illusion ya kufanya nijihisi kuwa nipo lakini kiuhalilia mimi sipo kabisa. Kwa hiyo mkuu Satoh Hirosh, consciousness ni kama software ambayo imekuwa programed na kuwekwa ndani ya miili yetu na kutengeneza illusion ambayo inatujifanya tujihisi tupo ila mzee baba sisi hatupo, hata hii jf haipo, ni maluweluwe tu. Yaani sisi ni GTA iliyochangamka 😂😂😂😂

Hapo nimejaribu kujenga hoja kwa kutumia mtazamo wa kwanza katika hoja yako kwa kuangalia hiyo key term ya consciousness, baadae nitakuja na hoja katika upande muktadha mzima wa hoja yako kujaribu kusisitiza ni kwa jinsi gani haya maisha ni illusion tu.

Sema kimeumana…😂😂😂😂😂
 
Habari yako muungwana.
Sidhani kama kuna ugumu sana kuhusu hicho unachojiuliza.Ninachoona ni kwamba ugumu upo kwenye namna unavyojiuliza.
Hebu tugeuze kwanza shilingi upande wa pili na tuangalie habari za kifo kisha tuludi kwenye habari za kuzaliwa.
Kwa kawaida mtu akifa huwa tunasema" MWILI WA MAREHEMU UTAZIKWA SIKU FULANI,MWILI WA MAREHEMU UTASAFIRISHWA,MWILI WA MAREHEMU UTA..........NK).
Kuna tofauti kubwa sana kati ya MAREHEMU na MWILI WA MAREHEMU,yaani ni kama ng'ombe na maziwa ya ng'ombe au ng'ombe na nyama ya ng'ombe.
Kwa kawaida maziwa ya ng'ombe sio ng'ombe mwenyewe ila ni sehemu ya ng'ombe na ndo mana hata yakikamuliwa na kutoka ng'ombe huendelea kuwepo.Hata tunapokula nyama ya ng'ombe hatusemi kuwa tunamla ng'ombe ila tunakula nyama ya ng'ombe.Hii ni kumaanisha kuwa kuna tofauti kati ya ng'ombe na nyama ya ng'ombe na ndo mana hata ukimchinja ng'ombe,huwezi kumla ng'ombe ila unachoweza kula ni nyama yake tu(steki,kongoro)
Hiki kinachotokea kwa ng'ombe ndo kinachotokea kwa mwanadamu,kwa kuwa hata baada ya kufa mwanadamu huwa hazikwi ila kinachozikwa ni mwili wake tu( MWILI WA MAREHEMU).
Kwakuwa kinachozikwa ni mwili wa marehemu,
ushawai kujiuliza huyu marehemu mwenyewe huwa anaenda wapi?
Muungwana,mwanadamu sio mwili tu,mwanadamu ni ROHO+NAFSI+MWILI.
Hivyo basi,unaposikia fulani kafa/kafariki jua kuwa kinachokufa/kufariki ni mwili tu ila ROHO+NAFSI bado huendelea kuwepo na unaposikia flani kazaliwa jua kuwa kinachozaliwa ni MWILI TU,ila ROHO+NAFSI huwa vipo tu.Swala la vinakuwa wapi au vinaenda wapi ni swala ambalo linakosa majibu si kwa sababu hakuna majibu bali kwa sababu limekosewa kuulizwa.
Swali hili huwa linakosewa kuulizwa kwa sababu neno wapi hutumika kuuliza sehemu vilipo vitu au viumbe vyenye miili tu.

Maelezo ya ziada.
Ikitokea umeulizwa fulani yuko wapi na ukasema yupo kariakoo,hapa unakuwa umemaanisha kuwa katika sehemu zote zilizopo duniani,muhisika hayupo sehemu nyingine yoyote ila kariakoo tu.
Hii ni kwa sababu miili yetu haiwezi kuwa maeneo tofauti tofauti kwa wakati mmoja,kwa hiyo ili uwe kariakoo maana yake haupo sehemu nyingine yoyote duniani kwa muda huo.
Sasa ROHO zetu zinauwezo wa kuwa sehemu tofautitofauti kwa wakati mmoja pindi zikiwa peke yake( bila ya mwili).Ila inapotokea ROHO inaingia kwenye MWILI ( pindi tukiwa hai)uwezo wa ROHO kuwa sehemu tofautitofauti kwa wakati mmoja unapotea mana ikifanya hivyo, ROHO itauacha MWILI kwani MWILI/MIILI yetu haina uwezo huo na ndo mana ROHO huchagua kufuata kanuni za MWILI katika kipindi cha uhai wetu.
Sasa sisi ambao TUNAMIILI huwa tunaitazama ROHO na kufikiri kuwa uwezo wa ROHO zetu ni mdogo kama ilivyo MIILI yetu na kupelekea kujiuza hayo tunayojiuliza.
Hivyo basi,nirudie tu kusema kuwa kujiuliza ROHO ilikuwa wapi au itaenda wapi ni kuikosea heshima ROHO kwa sababu neno WAPI linaelezea uwepo wa vitu au viumbe wenye miili tu katika eneo fulani.
Oooh.. Uko deep sana Chief.
 
Kwanza kabisa tumeumbwa siku moja ile siku ya sita ambayo Mungu alifanya uumbaji wa kumbe ambacho kitaitawala dunia na vitu vyake.

"Na tumfanye mtu kwa Mfano wetu"
Kuna mstari unasema: Nilikujua kabla ya mimba yako kutungwa, nalikujua ungali tumboni mwa mama yako
Kwa mujibu wa bible.

MAELEZO
Kwa sababu Mungu hana mawili wa nyama kama tulivyo sisi, sasa alipo sema kuwa ametufanya kwa Mfano wake inamaanisha kuwa sisi ni roho.
Ndiyo maana fulani akifa tunasema tunaenda kuaga mawili wa fulani (yaani hiyo fulani hayupo Bali ule ni mwili wake tu).

Nadhani, tukiwa tunachokuwa hatuna ni ile hali ya utambuzi/ufaham (konshaziness). Hii ni same applied kabla hatujaja duniani, nafsi/roho zetu zinakuwa unknown na miili yetu inakuwa katika state ya mbegu (me+ me) wakikutaba ndo tunatokea.
 
Yeah. breath in and out, mmmmmmmmmmmhhhh huuuuauauuuuuauuu.how can species like you able to ask a question like that?😅😅. Then if you Do that is another case which raise another questions, How? and why
What i know is. we are all one, that is am another of yourself. Big bang theory is beautful truth
 
mara kadhaa nimekuwa najiuliza hili swali.
roho yangu kabla mimi sijazaliwa na kuwa binadamu, ilikuwa inaishi wapi. nakosa jibu. sikubaliani na hoja za wafuasi wa imani za kidini.

labda roho yangu ilikuwa sayari nyingine au pengine ilikuwa inarandaranda hapa duniani ikiwa imejihifadhi kwa wanyama kama kuku, ngo'mbe au mbwa.

kiukweli kuna siri nzito sana inayohusu uumbaji wa mwanadamu, sidhani kama yupo anayeweza kuielezea kwa usahihi akaeleweka.

labda huku tulipo(duniani), tupo gerezani kutumikia adhabu baada ya roho zetu kutenda makosa kwenye universe nyingine.

labda kifo ni portal(mlango) ya kurudisha roho zetu kwenye universe yake ya awali baada ya kumaliza kutumikia adhabu hapa duniani(gerezani).

najiuliza maswali haya kwasababu sayari tuliyopo haina usawa, ina watu wanyonge sana, watu makatili sana, watu matajiri, watu masikini, watu wenye madaraka, wasio na madaraka na kadhalika.

ni kama tupo kwenye uwanja wa vita vile.

Umekuja vizuri sana mzee..! Maswali yako pia namimi huandama nafsi kichwa Changu.!
 
Kabla ya kuzaliwa wewe hukuwa mwanadamu bali ulikuwa mbegu, nusu kwenye korodani za baba yako na nusu kwenye ovari za mama yako.

Baada ya tendo la ndoa kufanyika ndipo hizo mbegu mbili zikaungana na wewe ukatengenezwa tumboni mwa mama yako.

Hii maana yake ni kwamba kama baba yako angelala na mwanamke mwingine basi wewe usingekuwepo kabisa hapa duniani.

Sentensi ya mwisho ina jibu la kile huwa nakiwazia wakati fulani.! Kuna wale wanaosemaga mzee asinge nizaa mama angeenda kurutubishwa nikazaliwa kwa Baba Mwingine wanasahau kwamba kila mbegu inayoungana na Yai inakuwa na mtoto wa tofauti. SitaweZa kudadavua sana ila tu ninachokijua hapo ni kwamba Mimi zao la Mbegu ya kiume ya siku hiyo iliyotoka na yai la siku hiyo hiyo lililotoka labda kama lile ya lisingerutubisbwa huenda nisingekuwepo.!
 
Mkuu, haya mambo kuna kipindi niliyawaza sana hadi nikahisi naweza kurukwa na akili, yanavuruga sana ubongo, anyway turudi kwenye mada maana hakuna namna, inabidi tufikiri ili kuutafuta ukweli.

Umesema kuwa sisi hatoko auto piloted kama ambavyo ‘tunahisi’ ma-gemu yalivyo kwa kuwa sisi tuna consciousness, hivyo umehoji consciousness yetu inatoka wapi. Hii hoja yako naweza kujaribu kuijibu katika namna mbili. Namna ya kwanza ni kwa kutumia key term uliyoitumia (consciousness) na namna ya pili ni kuangalia miktadha wa hoja yako kwa kulinganisha uhuru katika utendaji kati ya sisi binadamu na ma-gemu. Na pia nisisitize kuwa huu ni mtazamo binafsi tu.

CONSCIOUSNESS
Kama sote tujuavyo kuwa consciousness ni hali ya kujitambia au kuhisi uwepo wetu na vitu vinavyotuzunguka. Kwa maana hiyo naamini mimi Stephen Chelu nipo duniani kwa kuwa najihisi kuwa nipo, lakini je, mimi stephen chelu nipo kweli?

Twende kidogo kidogo kujaribu kuling’amua hili..

Kwa mfano nikienda sehemu ambayo watu hawanifahamu, watu wataniona lakini hawatanifahamu mimi ni nani na hivyo pengine nitatakiwa kujitambulisha. Hivyo nitasema; “Jina langu ni Stephen Chelu” au “Mimi ni Stephen Chelu”.
Sentensi hizi mbili hazifanani kabisa kwa kuwa zinamaanisha vitu viwili tofauti. Sentensi ya kwanza inaonyesha mimi ni huyu ambaye natumia utambulisho wa Stephen Chelu kwa maana ya kwamba, mimi nipo ila natumia jina la Stephen Chelu kutambulisha uwepo wangu kwa hiyo mimi si jina langu.
Sentensi ya pili inaonyesha kuwa mimi ni Stephen Chelu kwa maana ya kwamba jina langu ndiye mimi. Lakini je, jina langu ndiye mimi? Jibu ni hapana kwa sababu mimi naweza kuamua kujiita Idd Suleyman na bado nikaendelea kuwa mimi yule yule. Kwa hiyo ni wazi kwa kuwa mimi si jina langu, naweza kubadili jina ila mimi nikabaki kuwa mimi yule yule.
Mfano mzuri ndugu yangu wa Jf, the big superstar in town Don Nalimison, hapo mwanzo alikuwa anaitwa Deogratius Kisandu, lakini baadae akaenda mahakamani kubadili jina sasa hivi anatumia jina la Don Nalimison lakini yeye ni yule yule, anaendelea kutoa mapini makali kama kipindi kile anaitwa Deogratius Kisandu.

Tunaendelea..
Kwa kuwa tumegundua jina siyo mimi bali ni utambulisho wangu mimi, tunaendelea kutafuta huyo mimi mwenyewe ni yupi. Wakati najitambulisha nilitoa sauti, kwa hiyo pengine sauti yangu ndiye mimi mwenyewe. Je, ni kweli sauti yangu ndiye mimi? Sauti hii niliyoitoa ina sifa Fulani ambazo zinatofautiana na sauti nyingine zote kiasi watu wakiisikia tena watajua ni mimi ndiye ninayeonygea na si mtu mwingine yeyote.
Lakini fikiri, labda nimepata ugonjwa ambao umeathiri mfumo wa sauti na kufanya sauti ibadilike, je kubadilika kwa sauti kutafanya mimi niwe mwingine? Jibu ni hapana, mimi nitaendelea kujihisi ni mimi yuleyule niliyebadilika sauti. Na hata watu wakinisikia naongea watasema “Chelu, sauti yako imebadilika sana” Kwa hiyo sauti yangu siyo mimi bali ni kitu ambacho mimi nakitoa ili tuweze kuwasiliana.
Lakini kwa kukazia zaidi kuwa sauti siye mimi, naweza nisijitambulishe kwa sauti bali nikaamua kuchukua karatasi na peni na nikaandika jina langu. Kwa hiyo pasipo sauti yangu, watu watasoma ile karatasi na kutambua mimi ni nani.
Sasa kama mimi si jina langu wala si sauti yangu, mimi ni nini? Labda kwa kuwa sauti niliyoitoa ilitoka baada ya mimi kufikiri, labda mimi ni fikra zangu. Kama tujuavyo fikra huzaa mitazamo mbalimbali ambapo mitazamo hiyo hupelekea kufanyika kwa maamuzi mbalimbali pia. Sasa katika mitizamo mingi niliyonayo hebu tunyofoe mtazamo mmoja ili tuone kama mimi ni hizi fira zangu.
Mimi ni shabiki wa Yanga na watu wangu wa karibu wote wanajua hivyo. Kwa hiyo moja ya utambulisho wangu ni kuwa mimi ni shabiki wa vyura fc aka utopolo. Je, ikitokea nikabadilika kifikra na kupata mtazamo ambao utafanya nibadilishe maamuzi yangu na kuwa shabiki wa Simba; je, nitakuwa nimebadilika na kuwa mimi mwingine? Jibu ni hapana, mimi nitaendelea kuwa yuleyule ila nitakuwa nimetoka utopoloni na kwenda kwenye wa kimataifa. Kwa hiyo mimi si hizi fikra zangu, naweza kubadilika kifikra na nikabaki kuwa mimi yuleyule.
Sasa mimi ni nini? Labda kwa kuwa wakati najitambulisha nilitumia mdomo ambao ni sehemu ya kichwa ambacho kimeungana na sehemu nyingine za mwili na pia kwa kuwa jina niliandika kwa kutumia vidole vilivyopo mkono, ambao mkono huo nao umeunganika na sehemu nyingine za mwili na pia kwa kuwa fikra zinatoka kwenye ubongo ambao upo ndani ya kichwa ambacho kama nilivyosema hawa mwanzo, kimeungana na sehemu nyingine za mwili, Labda basi mimi ni huu mwili unaoonekana.
Je, ni kweli mimi ni huu mwili?

Tukuchukulie labda kuna siku nikaanza kuumwa. Nitasema “Mwili wangu unauma” au nitasema “Najihisi kuumwa”.
Sentensi hizo mbili hazifanani kabisa kwa kuwa zinamaanisha vitu viwili tofauti. Sentensi ya kwanza inaonyesha kuwa huu mwili si mimi bali mimi ni yule mwenye huu mwili hivyo inakanusha kuwa mimi si huu mwili unaoonekana. Sentensi ya pili inaonyesha kuwa mimi ni huu mwili na ndiyo maana nikasema ‘najihisi kuumwa’. Basi tuchukulie kuwa sentensi ya kwanza si sahihi na tukubaliane na sentensi ya pili inayosema mimi ni huu mwini unaoonekana.
Basi ikatokea mimi nikazidiwa na ugonjwa, nikafa. Taarifa zitakuja humu Jamiiforums kuwa ‘Member mwenzetu Stephen Chelu amefariki dunia’. Kauli hiyo bado inakubali kuwa mimi ni ule mwili, na kwa kuwa mwili hauna tena sifa za kuwa hai basi ni mimi huyo ndiye niliyefariki dunia. Kwa hiyo hadi hapo bado tunakubali kuwa mwili wangu ndiye mimi.
Taratibu za mazishi zinaanza, nawekwa kwenye jeneza, watu wanapiga picha na kuzipost humu Jamiiforums kuleta update ya kinachoendelea kwenye mazishi yangu. Caption ya chini ya picha ya jeneza langu itaandikwa “Jeneza lenye mwili wa Stephen Chelu”. Utata unaanzia hapa, kumbe kilichomo ndani ya jeneza si mimi, bali mwili wangu, kwa hiyo mimi siyo huo mwili. Kama kilichopo ndani ya jeneza siyo mimi bali ni mwili wangu, ina maana mimi bado nipo.
Sasa kama mimi siyo jina langu, kama mimi siyo sauti yangu, kama mimi siyo mwandiko wangu, kama mimi siyo fikra zangu na kama mimi siyo mwili wangu; je, mimi ni nini na nipo wapi?
Hivyo utagundua kuwa mimi sipo popote bali mimi najihisi nipo kwa sababu ya vitu mbalimbali (mwili, sauti, fikra nk) ambapo kwa pamoja vinatengeneza illusion ya kufanya nijihisi kuwa nipo lakini kiuhalilia mimi sipo kabisa. Kwa hiyo mkuu Satoh Hirosh, consciousness ni kama software ambayo imekuwa programed na kuwekwa ndani ya miili yetu na kutengeneza illusion ambayo inatujifanya tujihisi tupo ila mzee baba sisi hatupo, hata hii jf haipo, ni maluweluwe tu. Yaani sisi ni GTA iliyochangamka

Hapo nimejaribu kujenga hoja kwa kutumia mtazamo wa kwanza katika hoja yako kwa kuangalia hiyo key term ya consciousness, baadae nitakuja na hoja katika upande muktadha mzima wa hoja yako kujaribu kusisitiza ni kwa jinsi gani haya maisha ni illusion tu.

Sema kimeumana…
Naomba nikupe heko mkuu, lakini hoja yako hii kidogo kuingia akilini anahitajika nguvu ya ziada.
 
Kwa hiyo mkuu,ili kusherehesha mada yako ukaona kuna ulazima wa kuchomekea jina la Don Nalimison 🤣

Anyway mkuu,haya mambo yanapasua sn kichwa..hata usije tena kuendelea yashanichosha kuyajadili😁....hebu rudia Kusema kimeumana🤣
 
Roho ya mtoto inapatikana muda gani baada mbegu kurutubisha yai? Hiyo roho huwa inatoka wapi?

Nilitaka kuuliza swali hili hili yaani..! Jana nikianza kuusoma huu uzi muda wa saa saba usiku so baadae nikapitiwa na usingizi na nimerudi sasa..! Ngoja tusubiri Waungwana waje watujuze
 
Umejuaje roho itatoweka sehemu isiyojulikana?

Kwani hayo maneno yako yana uhakika gani na sio siasa tu pia?

Mkuu alichoandika jamaa ni Science na Mambo ya Dini zetu za kikristo yanakulazimisha uamini kwanza ndio uelewe na sio uelewe kwanza ndipo uamini. Kwa watu wanaofikiria sana ni mkangayiko
 
Dini zote duniani zina nadharia na mafundisho tele kuhusu maisha baada ya kifo. Kila dini ninayoifahamu imelizingumzia suala la maisha ya baada ya safari ya uhai wa binadamu kufika mwisho kwa undani sana tofauti na suala la alipotoka binadamu.

Japo kuna mjadala mkali kwa mafundisho na nadharia hizo lakini hakuna ubishi kwamba zipo, hii ni tofauti sana na mafundisho kuhusu alipotoka binadamu

Sehemu kubwa ya dini ninazozijua hazizungumzii alipokuwepo binadamu fulani kabla hajazaliwa na kuanza kuishi duniani.

Je mtu huwa anakuwa wapi kabla ya kuzaliwa kwake hapa duniani?

Kwa nini binadamu wengi pia hawahangahishwi na kutaka kujua walipokuwa kabla ya kuzaliwa?
Njia nyingine ya kuuliza swali lako ni hii: (1) ukifa mwili wako unakwenda wapi? (1) ukifa roho yako unakwenda wapi?

Kuhusu swali la kwanza, ukifa mwili wako unarudi ulikotoka. Kwa wanasayansi, hapa naongelea miduara ya bayo-jio-kemia, yaani, bio-geo-chemical cycles, ndio kusema biological, gelogical and chemical cycles.

Miduara hii ni mbinu ya kisasa kuelezea kile kitu baadhi ya wanateolojia wanaita miduara ya umwilisho (re-incarnation cycles).

Unakufa, unaoza, mime inapata mbolea, wanyama wanakula mimea, watoto wako wanakula mimea, elementi zilizokuwa katika mwili wako zinaingia katika miili ya watoto/wajukuu wako. Na hivyo bio-geo-chemical cycles zinadelea milele!

Utetezi wake kimetafizikia ni kwamba, tangu dunia iwepo miaka mabilioni, pamoja na viumbe wote waliomo, ina uzito ule ule. Kinachoendelea ni kama recycling kwa njia ya bio-geo-chemical cycle.

Kuhusu swali la pili sijakamilisha utafiti. Kuna hoja moja inaitwa "an argument from consciousness" kama njia ya kutetea uwepo wa Mungu. Sijamaliza kuisoma. Nitarudi baadaye.
 
Kuna adhabu utakayopata usipojua mwisho wako?
Kwa nini watu wanaumiza vichwa vyao kutaka kujua watakapokwenda baada ya kufa?
Lazma ujue mwisho wako sababu utalipwa kulingana na jinsi ulivyoishi,lakini hakuna haja ya kujua mwanzo
 
Back
Top Bottom