Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,298
- 45,585
Tukubali miaka mitano iliyopita kulikiwa na mwanaume mmoja aliyeweza kuwaweka wanaume na wanawake wote chini ya himaya yake bila kufurukuta. Wengine walikaa wakatulia kimya, wengine walibaki mashuja wa mitandaoni, wengi walimsifia na wote kwa pamoja tulimuogopa.
Wote walifanya hivyo kwa sababu nyingi. Wapo waliompenda kweli, wapo waliopenda maslahi yao tu na yeye aliwahakikishia hilo, wapo waliokipenda chama chao, wapo waliosema wana familia za kutunza, wapo walioogopa mkono wa chuma kupitia dola n.k
Wakati huu ambapo chuma hayupo na watu wanapokosa utendaji wa Serikali, Bunge, wanapodai Katiba Mpya, wanapohoji kuhusu muungano, wanapouliza kutenganisha kofia mbili n.k tusiwasakame sana na kuwabeza sana mbona hawakusema wakati wote.
Tuwaelewe na tujifunze kutokana na historia kwa sababu ambao hawajifunzi kutoka katika historia wana hatari ya kuirudia.