Ulikuwa mgao feki wa umeme ili kula pesa za tanesco sasa naona deal imehamia vita na malawi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulikuwa mgao feki wa umeme ili kula pesa za tanesco sasa naona deal imehamia vita na malawi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DUNIANGUMU JR, Aug 8, 2012.

 1. D

  DUNIANGUMU JR Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ULIKUWA MGAO FEKI WA UMEME ILI KULA PESA ZA TANESCO SASA NAONA DEAL IMEHAMIA VITA NA MALAWI.


  Tanzania imekuwa ni nchi ya watu wajanja sana katika maisha yao ya kila siku, ndiyo maana inaitwa 'BONGO' Inaitwa bongo kwa vile kila mtu anajitahidi kutafuta mbinu ili aweza kuishi na kumudu maisha yake ya kila siku amabayo ni mbinde sana kuona unafikisha mwisho wa mwezi.
  Watu watajitahidi kutafuta mbinu hizi na zile ile wale hata kama mlo ule ni NAJISI lakini lazima wafaulu, rejea mgao wa umeme, watu wamebuni mgao feki ili kujipatia pesa hawajali hata kama shirika likifa au hawajali hata kama watu watakaa gizani, rejea pia rada, watu wameiuzia serikali rada kwa bei mara dufu ili kujitajilisha wao binafsi na siyo serikali ya nchi yao, UZALENDO ule tumekuwa tumuukuta sasa unatoweka nchini kwetu kila mtu anataka mshiko tena mshiko mnono na familia yake, rejea nyumba za serikali, watu wamedhurumu nchi yetu kwa kujiuzia nyumba za serikali kwa bei nafuu na hali wanajuwa wanahujumu nchi, rejea wanyama pori wetu wanavyosafirishwa nje za nchi wakiwa hai wengine wafu hii yote ni kujitajirisha binafsi si kwa ajili ya nchi yetu.
  Sasa hivi, watu hao hao wanaotaka kujinufaisha binafsi na familia zao wameanzisha DILI la mzozo FEKI na nchi ya malawi ili kupata uhalali wa kutafuna pesa ya watanzania, Ni lazima tuwe macho na njama hizi:-
  1. wataanza dili za kununua silaha feki za kupigana na malawi
  2. wataanza dili ya kukodi magari makubwa ya kusafirisha silaha feki kwenda mpakani
  3. wataanza dili ya kununua dizeli feki kwa ajili vita na malawi
  4. wataanza dili ya kununua mafuta mapesi feki ya kulainisha mitambo ya kijeshi
  5. wataanza dili ya kuajili wanajeshi feki wa kupigana malawi
  6. wataanza dili ya kununua sare za kijeshi feki kwa ajili vita na malawi
  7. wataanza dili ya masurufu feki ya kutembelea uwanja wa mapambano
  8. wataanza dili feki ya kuchangisha watanzania fedha kwa ajili vita na malawi
  9. wataanza dili za vikao feki kwa ajili kujadili vita na malawi
  10. wataanza dili feki ya propoganda ya vyombo vya habari ili kuhalalisha vita na ulaji
  Watanzania ni lazima tuwe macho na viongozi wa dili hizi ili kuendelea kuibia nchi kwa kuanzisha mzozo feki na nchi jirani ili waweze kunufaika kwa dili feki kama zile za TANESCO, RICHMOND, EPA, AIR TANZANIA, BANDARI, VITALU VYA WANYAMA!!!! Jamani tutafilisi nchi hii, ole wenu baba wa taifa, waziri mkuu sokoine na karume original wafufuke leo ninaimani matajificha ndani ya vyoo vya shimo wote mnao chongo MA-DILI ili kuifilisi Tanzania yetu yenye neema. SAA YA UKOMBOZI NI SASA
   
 2. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ukweli mtupu mkuu
   
Loading...