Ulikereka nini hadi ukamuombea mgomvi wako afe? Tushirikishane ilikukuwaje

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
habari zenu!
Yapo matukio kadhaa ambayo hukera na kuudhi sana kiasi kwamba hadi watu hutengeneza uhasama maisha yao yote;
Uhasama huo unaweza ukawa we we na ndugu,mke,Mme, jilani, mfanyakazi mwenzio au mwanasiasa!
Ni jambo gani baya ulilowahi fanyiwa hadi ukatamani adui yako afe au umroge awe taahira?
Je, nikusalitiwa au nini? Tushirikishane hapa!!!!!
Maana kuna baadhi ya watu huombea hata wake/waume zao wafe!!!!!!!
 
Bado sijakerwa viwango vya kumuombea mtu mabaya au akumbwe na umauti...naah!!!

Na hata ikitokea nikakerwa kwa viwango vya kimataifa ninalo neno moja toka kwa Bwana wa Majeshi nalo ni hili "wapenzi,msijilipize kisasi,Bali ipisheni ghadhabu ya Mungu;maana imeandikwa kisasi ni juu yangu Mimi;Mimi nitalipa,anena Bwana"
Warumi 12:19
 
hilo andiko mbona gwajima halitambui alipotajwa kwenye madawa, anasema pambambana
 
Mimi sijawahi kufikiria kumuombea mabaya mtu aliyenikera kupita kiasi.
Ila mbwa na paka ninao fuga nimewapa majina ya walionikera .
 
Kipindi niko darasa la kwanza mpaka la pili nilikuwa naongoza wajinga darasani,tulipofika la tatu akahamia jamaa mmoja kwa sasa ni marehemu r.i.p bro.basi jamaa akawa anatuoshea balaa,yaani akipiga hesabu 99%nafuatia mimi ambaye nilikuwa nawakimbiza nina 66%.halafu wengine ndio wanafuatia.masomo yote ni hivyo.

Aisee kile kitendo kilinivuruga sana nikawa naomba hata jamaa atangulie mbele ya haki(akili za kitoto).ila nilipofika darasa la tano nikaanza kufikiri tofauti,kwamba natakiwa nisome nilikuwa naongoza wajinga tu.

Nikabadili mfumo wa maisha,ila jamaa alianza kutekwa na michezo sana,ingawa hakuwa anapoteza mimi ndio nilimfata aliko kule kwenye 98% nikawa namuongoza mpaka yeye.

Baada ya shule nilihama mkoa,miaka 6 baadae nakuja kuambiwa jamaa aliishafariki.nilisikitika sana.
 
noma sana
 
Back
Top Bottom