Ulikabilianaje na hali ya kuachwa na mtu uliyempenda?

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Mapenzi ni kama basi unaweza achwa stendi ili hali tayari umelipa nauli, kuna wakati unampenda mtu kwa moyo wako wote, unajiona kama vile umemaliza muda wote unamuwaza yeye lakini pia unajikuta umewekeza nguvu zako za hali na mali kwa huyo mtu lakini ghafla tu anakuacha na unasikia ana mwingine tena anataka kufunga ndoa.

Tena anakuacha kipindi ambacho wewe umekolea kwake huambiliki na husikii kuhusu yeye lakini yeye bila kujali hisia zako anakuacha, sasa unaweza/uliwezaje kukabiliana na hicho kipindi kigumu.
 
Zama za kupenda mwanamke (bila shaka wewe ni M) 100% zilishapitwa na wakati sahivi ni hamsini na hamsini unamwachia akiondoka maumivu hayawi makali sana.
 
Kiukweli inaumaa sana usiombe yakukute baki kuhadithiwa tu.
Buy the way ukiona mjinga umetendwa jua kuna fala kashapendwa. Mpnz hayana mwnyw.
 
Mchungaji Hizza wa pale cct udsm kila siku akihubiri kuhusu vijana miaka ile alikuwa anasema hivi

'" ukiachwa na mtu unaempenda Bila sababu yoyote Haina haja ya kulia wala kusononeka, nenda kanisan au nyumba ya ibada mshukuru Mungu kwa yote. Toa sadaka ya shukran mwachie Mungu songa mbele.....kwan hujui kusudi la Mungu juu ya hilo jambo"

Kwa wenye imani
 
Umenitonesa kidonda Dah, mapenzi ni kama siasa amanini hivyo wadau
 
Mapenzi ni "Pata Patia" au "Pata Potea". Ikiwa pata potea ndio ishatokea i.e ushaliwa, ushapoteza, kikubwa ni kukubali tu. Hakuna namna
 
Iliwai nitokea... Nilitamani nijichanjechanje mikono ili maumivu ya nje yachukue maumivu niliokua nayasikia ndani!!! Yaani mkaka tulikua vizuri ghafla akapotea tu!!! Akahama na kwenye simu hapatikani na chuo haendi!!! Jamani nikijifikiria saivi ndo naona jinsi nilivyochizika kipindi kile... Angalau angeniambia kua ananiacha!!!
Nikaanza kuwaogopa wanaume... Nilikaa mda sana kabla ya kumkubalia mwanaume mwingine... Although alikuja nitafuta baadae na kuleta story za ajabu nikamtolea nje... I was already over him. Na sikutaka maumivu yale ever again!
 
Daah pole sana...maisha hayana formula
 
Siku hizi mapenzi ya kweli hayapo...hata nikiachwa nasema afadhali nuksi imeondoka..kuachwa ilikuwa zamani..

BTW maumivu ya kuachwa na kutendwa nawaachia wavulana na wasichana wanaobalehe na kuvunja ungo RESPECTIVELY...am grown up now, i know how to handle and to deal with those kind of stuffs
 
Pole mkuu, kwa bahati sijawahi kuachwa hivyo siyajui maumivu hayo wenye uzoefu wa kuachwa watatueleza vzr
 
Ilinitokea, kwa jinsi alivyokuwa ananipenda niliamini yy ndio Mme haswaa. Kilichokuja kutokea sikuamini,nilikuwa nasikia maumivu mpk nikawa nahisi kufa. Lkn badae nikakaa nikatulia nikakubaliana na ukweli basi nashukru maisha yanaendelea mpk sasa.
 
Hayo ndo madhara ya kua na demu mmoja.me na mademu saba mmoja akizingua wala hainiathiri ndo kwanza nafanya usajiri wa kifaa kingine kuziba pengo.
 
Mi huwa natamani kuachika ili nipate kifaa kipya nikikaa na demu muda mrefu huwa naugua
 
Back
Top Bottom