Ulifanya kosa gani mpaka ukapewa suspension shuleni?

Mwalimu aliuliza kati ya jiwe na Nazi vikigongana je nini kitapasuka

Kwa ujasiri Mimi nikainuka na kumjibu" jiwe litapasuka kwa sababu now days mawe ni mabovu ". Darasa lote vicheko

Ticha akavimba ......chaap nikapelekwa ofisin sper ya wiki tatu

.Tafsir.......kumbe swali sikuelewa ..alivyosema jiwe ...alimaaniesha yeye ni mwamba na sisi ni vifaranga wadogo .....so vikikutana nn kitatoke?

kwahiyo teacher wako mbovu

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Niliitwa ofisini kwa Headmistress Sasa ile ametoka Kidgo kama dk 1 mm nikatoa Pen nikaweka A.KA Yangu kweny Meza yake. Ilikuja kutafutwa kweny A.K.A ile mpka ikagundulika ni mm naitumiaga nikapewa adhabu ya kukaa nyumbn miezi 3 na kuja na Mzazi na meza mpya
 
Mimi nilipewa nikiwa form 4 nikakaa nyumbani nikarudi siku ya mtihani wa mwisho.

1.Kosa lilikuwa ni kuvaa sketi fupi.
2. viatu ambavyo havina kamba.
3. Sikuchomeka shati.
4. Nilijiremba.
Wakaniambia nivue viatu niwape nikawapa, wakaenda kunisimamia ninawe uso, nikanawa, halafu wakataka nikavue sketi niwape na mimi sikupeleka. Hili ndio lilikuwa kosa.
alafu ukivua sketi, walitaka waone nini wakati ulikuwa hauna taiti?😆😆😆
 
Mimi nilikula mkong'oto na kupigwa Suspension
kutokana na kosa la lililotengenezwa na mwalimu wa B/K & Michezo KIGONG'OTA SEC SCH.
Kabinti kazuri nilikatongoza,kakaingia ktk 18 zangu nikawa nakafinya taratibu.
Kumbe ticha wa BOOK/K alikuwa anakanyengea kwa siri ila kadent kanamtolea nje.
Ticha akapewa nyepesi na wakuda kuwa kademu kapo na mimi.
Ticha akaja class kwetu akiwa mbogo vibaya mno, akatema cheche na mikwala kibao, kuwa siku akimkamata mzizi hapo sch. atajuta kuzaliwa.
Ilikuwa msala siku hiyo saa nane mchana, naitwa mbele ya alaiki kujibu mashtaka ya kuiba daftari la mdada mmoja na kufuta jina lake kisha kuandika jina langu.
Daftari likatembezwa kwa wanafunzi, wote wakasema jamaa mwizi. nilaambwa za matako kisha nikapelekwa ofisini kuchukua barua ya kutimuliwa.
Sasa nikiwa pale Ofisini, yule mwalimu wa BK akaja na kunishauri, kama nataka msaada ili nisifukuzwe,
nikubali kumuacha yule demu, na kumshawishi amkubali ticha wa BK then atalilekebisha swala langu kwa Mkuu wa shule na kwa Malole.
Akasema yeye ndiye aliyefanya mchezo huo wote ili ampate demu. hakika ticha Mtamb___, sitamsahau.
Mimi nilikataa kwakuwa niliisha aibishwa, so nikatimuliwa kwa miezi 2.
zinaa mbaya sana.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom