Ulichotegemea ndicho ulichokikuta ndani ya ndoa yako?

mbenda said

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,019
1,945
Asalam alaykum mabibi na mabwana, poleni kwa majukumu ya kazi za kila siku na kulea watoto.

Je, wewe ni mke au mume?

Je, umeoa au kuolewa?

Ndoa yako bado ina Furaha na amani?

Unaishi vile ulivyotegemea kalba ya ndoa?

Haya ni baadhi ya maswali muhimu kujiuliza ikiwa upo ndani ya ndoa. December 12 mwaka uliopita tulipeleka barua ya posa kwa familia fulani hukoo Sinza sasa wakati tunarudi mtu niliengozana nae akaniambia hivi.

Wanawake wengi wanategemea kupata raha ndani ya ndoa zao. Ikiwa imetokea tofauti hapo kuna uwezekano mkubwa sana WA ndoa kuyumba au kuachana kabisaaaaa.

Siku moja nikamuuliza Bi harusi wangu mtarajiwa unagemea nini ndani ya ndoa yako? Akanijibu, AMANI, FURAHA, KUSIKILIZANA NA UPENDO. Kiufupi nilifarijika sana kwa majibu haya.

Swali linakuja, Je watu wote wanaishi vile walivyotegemea ndani ya ndoa zao?
 
Hakuna kiumbe stressful kama mwanamke.. ukishampatia ndoa ndio umempa nafasi ya kuonyesha makucha yake.. zile jeuri.. viburi alizo zificha ndio utaanza kuziona. Nakwambia hakuna rangi utaacha kuiona hasa ukikosa pesa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hakuna kiumbe stressful kama mwanamke..ukishampatia ndoa ndio umempa nafasi ya kuonyesha makucha yake..zile jeuri..viburi alizo zificha ndio utaanza kuziona..nakwambia hakuna rangi utaacha kuiona hasa ukikosa pesa.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Hapa ndio wasiwasi wangu, kuumwa au kokosa hela watakukimbia tu, wengi wanapokuona una muelekeo wa kimaisha utaskia nitakua na wewe kwenye shida na raha sasa njoo ukose hela hata miezi mitatu tu uone huo urongo unapojidhihirisha.
 
Hapa ndio wasiwasi wangu, kuumwa au kokosa hela watakukimbia tu, wengi wanapokuona unamuelekeo wa kimaisha utaskia nitakua na ww kwenye shida na raha sasa njoo ukose hela ata miezi mitatu tu uone huo urongo unapojidhihirisha
Maisha sio kupata tu kuna kukosa, kuna kulala na njaa kuna raha na karaha kuna amani na vurugu.

Ndoa inahitaj uvumilivu, kuvumiliana madhaifu yenu, kuyabeba madhaifu ya mwenzio kama yako, kustiriana kwa kila hali, kusikilizana, kuheshimiana, kuthaminiana kwa ufupi ndoa ni full package.

Usikatishwe tamaa na watu waliokata tamaa, kaa tulia tafuta mke anaejua thamani yako, yake na ndoa kwa ujumla.

Usisahau ukiwa mwema utapata mwema, ukiwa kiruka njia utapata wa kufanana nawe.

Cha mwisho omba sana Mungu akupe macho ya moyoni uweze kumtambua na kumpata mke mwema, hakika ndoa njema ni ile yenye amani na kuridhika na kila hali.
 
Kiukweli maisha ya ndoa ni vaisi vesa, unategemea furaha ukiwa nje ukioa au kuolewa furaha ni uamue iwepo, ukubali kudhalilika, ukabali kejeli hasa kama pesa imeyumba, lakini yote yanawezekana. Niliwahi mfungulia mke wangu biashara ya m15 mi nikabaki natafuta vibarua vya kawaida, dharau zilianza hadi kufikia kuchit hapo tukiwa na watoto wawil, Nilivumilia kwa sababu ya watoto ila majuzi maji yamenifika pabaya nimeamua kuwa bachela.

So ushauri wangu tegemea yote, hakuna kiumbe dhaifu duniani kama mwanamke, hata umpe roho yako haridhiki, kama nilivyosema awali furaha ni uchague, upokee madhaifu yote yatakayotokea kwenye ndoa ikiwa ni kuvumilia usaliti, kuvumilia viburi, kuvumilia kejeli, kuvumilia kila aina ya uchafu maana mtu anapoingia kwenye ndoa anajua kila kitu amemaliza kwa kuwa anajua atakuwa happy, atakula kila aina ya raha, out nyingi, sex kibao, picnic za kutosha.

Wasijue ukiwa ndani majukumu yanaongezeka, unaweza uhamishwe kibarua uende Bukoba na we uliishi Dar, muda huo watoto wapo shule mama yao nae ana kibarua hapo ndo tutaomba Mungu asimamie ndoa maana uvumilivu wa mwanamke kwa tendo la ndoa ikizidi miezi mitatu bahati, so karibu ndoa ni kamari, sorry kwa uandishi usiopangilika, nawasilisha.
 
Ndoa ni sehemu ya maisha, kama yalivyo maisha kwenye nyanja zingine

Wewe huna gari, unapanda daladala, mwenzio anaendesha gari ya millioni 600!

Wewe Kodi ya nyumba unalipa 100K, mwenzio analipa 1000K!

Wewe umejenga nyumba kwa miaka 10, mwenzio ana nyumba 20 na anajenga kila siku.

Hata kwenye ndoa, zipo zenye visirani, michepuko, ngumi kila siku.

Zingine ni Kama upo peponi vile
 
Maisha sio kupata tu kuna kukosa, kuna kulala na njaa kuna raha na karaha kuna amani na vurugu.

Ndoa inahitaj uvumilivu, kuvumiliana madhaifu yenu, kuyabeba madhaifu ya mwenzio kama yako, kustiriana kwa kila hali, kusikilizana, kuheshimiana, kuthaminiana kwa ufupi ndoa ni full package.

Usikatishwe tamaa na watu waliokata tamaa, kaa tulia tafuta mke anaejua thamani yako, yake na ndoa kwa ujumla.

Usisahau ukiwa mwema utapata mwema, ukiwa kiruka njia utapata wa kufanana nawe.

Cha mwisho omba sana Mungu akupe macho ya moyoni uweze kumtambua na kumpata mke mwema, hakika ndoa njema ni ile yenye amani na kuridhika na kila hali.
Umemaliza kila kitu
 
Asalam alaykum mabibi na mabwana, poleni kwa majukumu ya kazi za kila siku na kulea watoto.

Je, wewe ni mke au mume?

Je, umeoa au kuolewa?

Ndoa yako bado ina Furaha na amani?

Unaishi vile ulivyotegemea kalba ya ndoa?

Haya ni baadhi ya maswali muhimu kujiuliza ikiwa upo ndani ya ndoa. December 12 mwaka uliopita tulipeleka barua ya posa kwa familia fulani hukoo Sinza sasa wakati tunarudi mtu niliengozana nae akaniambia hivi.

Wanawake wengi wanategemea kupata raha ndani ya ndoa zao. Ikiwa imetokea tofauti hapo kuna uwezekano mkubwa sana WA ndoa kuyumba au kuachana kabisaaaaa.

Siku moja nikamuuliza Bi harusi wangu mtarajiwa unagemea nini ndani ya ndoa yako? Akanijibu, AMANI, FURAHA, KUSIKILIZANA NA UPENDO. Kiufupi nilifarijika sana kwa majibu haya.

Swali linakuja, Je watu wote wanaishi vile walivyotegemea ndani ya ndoa zao?
Ngoja nitulie kwanza nisubirie mrejesho wa walioko kwenye ndoa.
 
Hongera sana, uzi mzuri sana. Ambao hatupo kwenye ndoa tunasikiliza walotangulia ili tusiwe waongo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom