Ulianzaje kujenga?

airwing

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
306
397
Habari za mda huu, Wana jamvi wenzangu

Kama uzi unavyojielezea, kuna watu wengi wanatamani kumiliki mjengo mjini lakini hawajui, waanzie wapi, wapitie wapi, wafanye Nini, watililike vipi hatua kwa hatua za ujenzi na hivyo kukamilisha Ndoto zao.

Kwa wewe mwenye uelewa, au ulifanikisha katika hili tunaomba tips zako, na vile ulivyofanikisha kusimamisha mjengo mjini.

NB: Mimi bado sijafanikisha Ila naamini Kuna vitu vingi nitajifunza hapa, Karibuni.
 
Nyumba ya Kwanza unajifunza mengi. Zinazofuata hamna wa kukudanganya.
Ni sawa na kumiliki gari, gari la kwanza linapurusa sana ila yanayofuatia unakuwa unajua mengi sana.

Kwenye nyumba yangu wakati wa kujenga kilitokea alichosema mdau hapo, mimi nyumba mpaka usawa wa kupaua ilipofikia ikawa imenila sana pesa wakati kuna mambo kibao ambayo nikitazama sasa ninaona ningeyaokoa, nitatumia akili hizo kwenye nyumba inayofuatia baada ya kujifunza.
 
Siku moja rafiki yangu alinitembelea nilipokuwa nimepanga one bedroom apartment. Akaniuliza Kodi bei gani nikamjibu. Akaniambia kwenye kile kiwanja chako hii unajenga Kwa 10m! Jamaa ni mkandarasi mkubwa.

Nikamwambia unatania akaniambia hii ndio kazi yangu najua ninachosema. Nikamuuliza ya vyumba viwili he? Akasema inaongezeka kidogo labda 15m!

Tangu siku hio nikaamua kujenga hio ya vyumba viwili and the rest is history. Apart kuwa na kipato pia unahitaji information na kufanya maamuzi nyingine mbwembwe.

Btw nilinogewa nikajikuta najenga hio ya vyumba viwili Kwa bajeti mara mbili ya makadirio alionipa!
Sio mbaya ulidhubutu,mbaya ungekata tamaa
 
Sio lazima ukubaliane na ninachoandika. Nilifikiri unauliza ili upate chochote kaa na negativity yako. I deleted all my posts
Hapana umenitafsiri negatively.. Wala sijadharau ulichokipost ndg,!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom