Ulevi wa madaraka Vs Ulevi wa fedha, upi ni hatari?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,099
164,468
Sijawahi kumshuhudia mlevi wa madaraka ila mlevi wa fedha nimewahi kumuona.Huyu jamaa ktk miaka ya 90s alimiliki Hotel ikijulikana kama Three in One, yeye fedha ilipomzidia alifanya sherehe ya kuuaga umaskini.

Ilikuwa ni pale Iringa mjini na story zikavuma mji mzima hata zikawafikia watu wa kodi na mwaka mmoja baadaye Kalinga alionekana mtaani akibomu hata nauli ya kupandia Mnenge town bus.

Sasa ulevi wa madaraka ni kama nimeuhisi bungeni wiki hii pale wabunge walipotumia muda mwingi kumjadili mtu badala ya "swala" ila sina hakika kama huo ni ulevi.

Nimpongeze tu mh Bulaya kwa kutukumbusha uwepo wa mamlaka ya kupambana na kudhibiti matumizi ya mihadarati ila atusaidie pia kumshauri Mwenyekiti kwamba "mtu hakatai wito hukataa neno"
 
Ulevi wa madaraka ni mbaya zaidi kwa sababu watu huteswa na kunyanyaswa, wengine huuawa kimyakimya au kupotea katika mazingira yasiyoelezeka
 
Back
Top Bottom