Ulega atoa mwezi mmoja kwa TARURA kuhakikisha ujenzi wa barabara umekamilika

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo, Abdalah Ulega ametoa mwezi mmoja kwa tarura wilaya ya mkuranga kuahakikisha barabara ya vikindu sangatini ambayo inajengwa iwe imekamilika.

Ulega ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa Barbara hiyo katika kata ya vikindu wilayani mkuranga mkoani pwani na kuwasisitiza wakandarasi kutumia pesa za mradi vizuri katika malengo yaliyo kusudiwa.

Amesema kuanzia kesho mkandarasi hakikishe ananza kuchimba mitaro sambamba nakuweka mawe pembezoni mwakuta za barabara ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea mvua za masika zitakapoanza.

"Hapa mvua zikianza kunyesha kabla mitaro haijachimbwa hii barabara itakatika na nyumba zilizopembezoni zitaanguka, kwahiyo tarura shughulikieni ili suala haraka sambamba nakuweka barabara za mchepuko kwa ajili ya kupunguza msongamano wamagari." Amesema ulega

Aidha ulega ameongeza kuwa mkandarasi aliyekuwepo saiti alipewa miezi nane kazi iweimekamilika,lakini mpaka sasa ni miezi saba hakuna kilichofanyika hivyo ametaka kazi hiyo ikamilike ndani ya mwezi mmoja uliobaki.

Kwa upande wake Mhandis Bernard Mwita akizungumza kwa niaba ya meneja wa tarura mhandis Godfrey Mlowe amesema mkandarasi waliempa kazi ndiye aliyewakwamisha ila watahakikisha kazi hiyo inakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake diwani wa kata ya vikindu Mohammed Maundu amemshukuru mbunge wa jimbo hilo kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kutatua changamoto za wananchi.

Katika hatua nyingine ulega ametembelea ujenzi wa daraja la kifaurongo lilopo tambani mkuranga mkoani pwani na kumtaka meneja wa tarura kuhakikisha karavati linalojengwa linakamilika kabla ya mvua za masika kuanza ili kuondoa kero kwa wananchi.

Akizungumza mbele ya wananchi wakati wa ziara yake katika kata ya tambani ulega amemsisitiza meneja watarura kuhakikisha kunajengwa karavati kubwa litakalo weza kuhimili maji yanayopita kwa kasi.

Ujenzi wa daraja la kifaurongo ambalo linaunganisha mkoa wa Dar es salaam

Kwa wilaya ya temeke kupitia mbande, na mkoa wa pwani kwa wilaya ya mkuranga kupitia kata ya tambani, litawasaidia sana wananchi kwani kipindi cha mvua eneo hilo halipitiki hali inayopelekea wananchi kuvuka na madumu kitendo kinacho hatarisha maisha yao.

Hata hivyo serikali ya awamu ya tano ya Daktari John Pombe Magufuli kupitia mbunge wa jimbo la mkuranga ilijenga daraja la kifaurongo lililogharimu kiasi cha mil 200 lakini kwa bahati mbaya liharibiwa na mvua zilizopita, na imetoa mil 200 zingine kwa ajili ya ukarabati wa daraja hilo ili kufanya kero hiyo kuwa historia kwa wananchi wa kata ya tambani

Awali ulega alishiriki uchimbaji msingi wa ujenzi wa madarasa matatu kwa shule ya msingi shikizi ya mpera iliyopo kata ya vikindu wilayani mkuranga mkoani pwani, ambapo amekabidhi mabati 100 na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya kumalisha ujenzi huo.

Akikabidhi mabati hayo Abdalah Hamisi ulega ambaye pia ni naibu waziri wa habari sanaa utamaduni na michezo amesema ujenzi wa shule hiyo ni muhimu kwasababu itapungunza changamoto ya mrundikano wa wanafunzi katika shule ya msingi kisemvule.

Naye diwani wa kata ya vikindu Mohammed Maundu amesema shule hiyo shikizi ikikamilika itachukua watoto wa darasa la kwanza hadi la tatu kwa sasa ili kuwapunguzia changamoto vivuko na umbali.
 
Back
Top Bottom