Ule uteuzi wa kupeana kishikaji kwenye nafasi nyeti za nchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ule uteuzi wa kupeana kishikaji kwenye nafasi nyeti za nchi!

Discussion in 'International Forum' started by The Quonquerer, Apr 9, 2010.

 1. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wabunge washtushwa ATCL kudaiwa 39 bilioni[​IMG]Sadick Mtulya

  WAJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, wameshutshwa na deni la Sh39 bilioni na gharama ambazo Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), zinalilipa Shirika la Ndege la Air Bus.

  Deni na gharama hizo zinatokana na ndege ATCL iliyopata hitilafu ya bawa, wakati ikitua mkoani Mwanza siku kadhaa zilizopita.

  Kutokana na hali hiyo, kamati hiyo imeitaka Bodi ya ATCL inayongozwa na Balozi Mustafa Nyang'anyi, kuwasilisha vilelezo vya mikataba kati ya Shirika la Ndege la Air Bus na ATCL.

  Mikataba hiyo inapaswa kuwasilishwa bungeni katika kikao kinachotarajiwa kuanza wiki ijayo.

  “Ni kweli ATCL inadaiwa Sh39 bilioni na kulipa gharama za ile ndege iliyopata hitilafu kule Mwanza. Fedha hizo zinalipwa Shirika la Ndege la Air Bus. Kutokana na hilo kamati imeiagiza bodi ya ATCL kuleta vielelezo vya mikataba iliyongia na shirika hilo katika Bunge la linaloanza Aprili mwaka huu,” alisema Mwenyekiti wa kamati hiyo Mohamedi Misanga.

  Misanga alisema kamati yake itatangaza msimamo wake baada kupitia vielelezo hivyo na kupata maelezo ya kina.

  Mapema, kamati hiyo ilikutana kwanza na wawikilishi wa wafanyakazi na kupokea mapendekezo yao.

  Baadaye ilikutana na bodi kwa ajili ya ufafanuzi wa mambo mbalimbali ya msingi.

  Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili, wameapa kuibana ATCL ili itoe taarifa za msingi kuhusu matatizo ya kimejimenti, tangu shirika hilo liliporejeshwe mikononi mwa wazalendo, baada ya kuvunjwa mkataba kati yake na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA). "Tuliwabana hadi wamevunja mkataba na SAA, tumewapa wazalendo wenzetu mambo bado hayaendi kabisa, mara unasikia ndege iliyonunuliwa bawa moja lina itilafu," alisema mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwa.
   
 2. M

  Mkora JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  What ?
  Mbona hizo pesa zinashinda hata thamani ya ndege, This is too much ni bora na nchi yenyewe tubinafsishe kila mtu apate chake
   
Loading...