nyamwingi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2016
- 933
- 863
*KCWW RAM/29 1438*
Darasa ya Ramadhani, Jumatatu tarehe 24 Ramadhani 1438, sawa na 19 Juni 2017
WAJIBU WA ZAKA YA FITRI
Zakatul-Fitr ni zaka/sadaka ya lazima inayotolewa baada ya kumalizika Ramadhani, na kuingia tarehe mosi, Shawwaal/Mfungo Mosi: mara tu baada ya kuandama mfungo wa Shawwaal, na hivyo kumalizika Mfungo wa Ramadhani.
Inaitwa Zaka ya Fitri, kwa sababu ni Zaka inayotolewa baada ya kufuturu/kumaliza Wajibu wa kufunga Ramadhani.
Kama ilivyokuwa Sijdatus-Sahw, inayo sujudiwa mwisho wa Swala–ni mfano wa raba au fidia ya kusahau kufanya Sunna maalum ndani ya Swala, basi na Zakatul-Fitri ni kitakaso cha vijimakosa vidogo vidogo vya Saumu, vilivyochumwa kwa kujua au kutokujua wakati wa kufunga Ramadhani. Yaani ni kirekibisho cha palipoharibika kidogo katika Swaumu.
Imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas رضى الله عنهما akisema: Amesema Mtume ﷺ,
زكاة الفطر طهرة للصائم من اللغو والرفث وطعمة للمساكين. فمن أداها فبل الصلاة فهي زكاة مفبولة ومن أداهابعد الصلاة فهي صدقة من الصدقات (رواه أبو داؤد ,ابن ماجه والدار قطنى)
“Zaka ya Fitri ni kitakaso cha aliyefunga kutokana na mambo ya upuuzi na maneno machafu, na ni lishe kwa masikini. Hivyo, atayeitoa kabla ya Swala, itapokewa kama Zaka, na atayeitoa baada ya Swala basi ni sadaka kama sadaka yoyote ile nyengine.”
Wanachuoni wa Fiqh, huielezea na Zaka ya Fitri kwamba:
زكاة الفطر: صدقة معلومة بمقدار معلوم، من شخص مخصوص، بشروط مخصوصة، عن طائفة مخصوصة، لطائفة مخصوصة، تجب بالفطر من رمضان، طهرة للصائم: من اللغو، والرفث، وطعمة للمساكين،
“ Zaka ya Fitri ni Sadaka ya wajibu maalumu, ya kiwango maalumu, kutoka kwa mtu maalumu, kwa masharti maalumu, kwa niaba ya watu maalumu, kupewa watu maalumu, kwa lengo maalumu, nalo ni Kikataso cha Swaumu na chakula kwa masikini.”
Zaka ya Fitri imefaradhishwa mwezi wa Shaabani, mwaka wa pili Hijriyya, kama kitakaso cha mwenye kufunga Ramadhani.
Zaka ya Fitri imethibiti kwa Qu’aani na Sunna ya kauli na vitendo.
Mwenyezi Mungu سبحانه وتعالى amesema, kwa wenye kujitakasa nafsi zao kwa kutoa sadaka:
قَدْ أَفْلَحَ مَنْ تَزَكَّى* وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّى * بل تؤثرن الحياة الدنيا * واللآخرة خير وأبقى
“ _Hakika amekwishafaulu aliyejitakasa na akakumbuka kutaja Jina la Mola wake na akaswali. Ila nyinyi mna hiari maisha ya dunia! Na ya Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi._” (Al-A‘la 87:14-15).
Wamesema Imam At-Tabari, Ibn Kathir na wengine, kuwa Sa‘id bin Al-Musayyib na ‘Umar bin ‘Abdul-‘Aziz (khalifa) na maswahaba wengine wamesema Aya hizo zinazungumzia Zakatul-Fitr. _Tafsir At-Tabari_ 24/374, pia _Muswannaf ‘Abdurrazaaq,_ Hadithi [HASHTAG]#5795[/HASHTAG].
Kwa upande wa Sunna:
Zimepokewa kutoka Mtume ﷺ Hadithi mbali mbali kuhusu wajibu wa Zaka ya Fitri. Miongoni mwa Hadithi hizo ni:
1. Imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Umar رضي الله عنهما akisema: Amefaradhisha Mtume ﷺ Zakatul-Fitr juu ya binaadamu, katika Mwezi wa Ramadhani. Nayo ni pishi moja ya tende au shayiri kwa kila mja, awe huru asiwe huru (mtumwa) mwanamume au mwanamke, miongoni mwa Waislamu.” _Muttafaq ‘alayhi_.
2. Imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Umar رضي الله عنهما akisema: Amefaradhisha Mtume ﷺ Zakatul-Fitr katika Mwezi wa Ramadhani, nayo ni pishi moja ya tende, au pishi moja ya shayiri, juu ya mja aliye huru, mwanamume au mwanamke, mkubwa au mdogo, miongoni mwa Waislamu. Na akaamrisha itolewe kabla ya watu kwenda kuswali Swala ya Idi.” Ameipokea Bukhari.
Hivyo, Zaka ya Fitri ni Zaka ya kiwiliwili SI zaka ya Mali. Inatolewa kutakasa nafsi ya mja na kuisafisha, hata kama haina makosa au uchafu. Na hiyo inamaanisha ni wajibu kutolewa kwa kila kiumbe Mwislamu, hata aliyezaliwa leo, mwamume au mwanamke, mdogo au mkubwa, muungwana au mtumwa.
3. Imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas رضي الله عنهما akisema: Amefaradhisha Mtume ﷺ Zakatul-Fitr kuwa ni kitakaso cha Swaumu kutokana na makosa madogo madogo na mambo machafu, na kuwa ni chakula kwa masikini. Hivyo basi, atayeitoa kabla ya Swala (ya Idi), Zaka yake ya Fitr itakubaliwa, lakini atayeitoa baada ya Swala (ya Idi) basi hiyo itakuwa ni sadaka tu kama sadaka yoyote nyengine.” Ameipokea Abu Daud.
4. Imepokewa kutoka kwa Abu Sa‘id Al-Khudriyy رضي الله عنه akisema: Tulikuwa tukitoa sadaka ya Zakatul-Fitr (wakati wa Mtume ﷺ) pishi moja ya chakula, au shayiri, au pishi moja ya tende, au pishi moja ya samli, au pishi moja ya zabibu.” _Muttafaq 'alayhi_. Na imepokewa vile vile na Tirmidhi, Nasaa'i, Ibn Maajah, Abu Daud na Ahmad.
*UFAFANUZI*
Zaka ya Fitri ni wajibu kwa kila nafsi ya Mwislamu anayetweta–yaani anaepumua. Ni Zaka ya kiwiliwili, si Zaka ya mali. Hivyo, midhali kiwiliwili kipo basi lazima kitolewe Zaka ya Fitri. Ni wajibu. Ni Faradhi. Haiepukiki, isipokuwa kwa yule ambaye hana uwezo kabisa. Hapo لايكلف الله نفسا إلا وسعها.
Ama mwenye kipato, au mwenye wajibu wa kumtunza mtu mwengine, kama mke, watoto, wazazi wake wawili wasiojiweza, watumishi wa nyumbani na kadhalika, na kipato chake kikawa kinazidi wajibu wake wa kuwatunza anaowatunza, basi ni wajibu KWAKE kujitolea yeye mwenyewe, kwanza, na kisha kuwatolea wote wale anaowajibika kuwatunza, kwa hali na mali. Yaani, lazima awe na chakula cha ziada ya kula yeye na familia yake, siku ya Idi. Hicho kitachozidi ndicho kinachotolewa Zaka ya fitri. Kikiwa hakitoshi kulisha familia yake hiyo siku ya Idi, basi hana jukumu la kutoa Zaka ya Fitri.
Kwa maneno mengine, iwapo baba mwenye nyumba ni masikini, hana cha kumtosha yeye na familia yake siku ya Idi, basi huyo hana wajibu wa kutoa Zaka ya Fitri. Wala hana wajibu wa kumtolea mkewe, hata kama mke huyo ni mwenye uwezo kutokana na kipato chake mwenyewe.
Lakini mke mwenye kipato chake mwenyewe, anaweza kujitolea kumtolea mumewe na watoto wake akipenda. Maana hana wajibu wa kujitunza, wala kumtunza mumewe wala watoto wake. Ni hiari yake, na ni fadhila kubwa, sana, kufanya hivyo. Ila SI wajibu juu yake.
Zaka ya Fitri ni chakula, SI pesa. Na kiwango cha kutolewa ni pishi moja ya chakula kinacholiwa sana katika jamii husika. Hivyo, vyakula vinavyoingia hapa ni nafaka zote, kuanzia ngano, shayiri, mchele, unga wa ngano, sembe, maharage, ulezi, nk. Ni chakula kinacholiwa sana na watu wengi katika jamii ya mtoa Zaka hiyo.
Kiwango cha Zaka ya Fitri ni pishi moja, ambayo ni sawa na kilo mbili na gram 400; kwa pishi ya Mtume ﷺ (ambayo ni sawa na vibaba vine vya Mtume ﷺ, na kibaba kimoja ni ujazo wa nafaka kwenye viganja viwili–kwa pamoja–vya mtu wa kawaida). Hivyo, ni kama kilo mbili na nusu za chakula kinachopendwa sana na jamii husika. Kiwango hicho ni kwa kila kiumbe chenye uwezo wa kujitolea chenyewe.
Iwapo hakina uwezo basi ni juu ya mwenye jukumu la kumtunza kiumbe huyo, ilimradi ana uwezo wa shibe yake na shibe za watoto wake wote, siku ya Idi. Kitachozidi ndicho kitachotolewa Zaka. Kama hakitoshi, basi akigawe kwa utaratibu aliouweka Mtume ﷺ kama ifuatavyo:
عن جابر رضي الله عنه قال قال رسل الله صلى الله عليه وسلم: ((ابدأ بنفسك فتصدق عليها، فإن فضل شيء فلأهلك، فإن فضل عن أهلك شيء فلذي قرابتك، فإن فضل عن ذي قرابتك شيء فهكذا وهكذا)) يقول: فبين يديك، وعن يمينك، وعن شمالك.(رواه مسلم)
“Anza kujitolea mwenyewe. Kikizidi kitu watolee watu wako wa nyumbani (anza na mke, kwanza, kisha watoto). Kikizidi kitu, watolee ndugu na jamaa zako (anza na ndugu na jamaa wa karibu, kisha wa mbali). Kikizidi basi watolee wa huku na huko, na kule na hapa (walio karibu zaidi nawe na ambao si watu wa ukoo wako, kama majirani wa karibu).” Ameipokea Muslim.
*SUNNA ZA KUTOA ZAKA YA FITRI*
a) Kuitoa mara baada ya kuandama mwezi wa Shawwaal–yaani usiku wa kuamkia Sikukuu, au kabla ya kwenda kuswali Swala ya Idi, au siku moja au mbili kabla ya kumalizika Ramadhani.
b) Kumtolea hata mtoto aliye tumboni, kama alivyokuwa akifanya Sayyidina ‘Uthman bin ‘Affaan رضي الله عنه. Ameipokea Ahmad na Ibn Abi Shayba.
c) Kuigawa kwa mikono yako mwenyewe, badala ya kuwapa watu wengine waitoe kwa niaba yako. Mtume ﷺ alikuwa akifanya hivyo, na kuwausia Maswahaba nao wafanye hivyo.
d) Ukiwapa watoto wako nyumbani kuitoa, ni sawa na kuigawa mwenyewe.
e) Kuwapa masikini jamaa zako, wenye kustahiki na ambao huna wajibu wa kuwatunza.
f) Kuigawa kwa masikini wa mahali ulipo, ila ikiwa kuna wanaohitaji zaidi, na ni jamaa zako, nchi nyengine.
g) Iwapo chakula unachotoa kina viwango mbali mbali, basi chagua kiwango cha juu: Mwenyezi Mungu amesema: _“Hamtaipata Pepo mpaka mtoe mnavyovipenda.”_
h) Kutoa nafaka kavu, inayoweza kuhifadhika kwa siku kadhaa bila ya kuharibika, ni bora kuliko chakula kisichoweza kuhifadhika kwa muda mrefu.
i) Kwa upande wa Wazazi wako wawili, ni Sunna kumtolea Mama mzazi kwanza, kisha ndiyo Baba mzazi–iwapo wanakutegemea kuwatunza.
j) Kuwapa majirani zako masikini, ni bora kuliko masikini wa mbali.
*YALIYOMO NA YATOKANAYO*
Kutokana na Aya za Qur’aani na Hadithi za hapo juu, maulamaa wema waliotutangulia wamefafanua YALIYOMO NA YATOKANAYO kama ifuatavyo:
1. Zakatul-Fitr ni wajibu, kwa kila mwenye kuweza, na ambaye ana chakula cha ziada ya chakula chake cha Sikukuu ya mwanzo.
2. Asiye na uwezo, na ambaye yumo chini ya kukimiwa na mtu mwengine, kama vile Baba mzazi, au hata mlezi wake tu, basi wajibu wa kutolewa upo juu ya mabega ya mwenye kumkimu. Kwa maana hiyo, Mume anamtolea mkewe, watoto wake, wazee wake–iwapo wamo chini ya himaya yake–mtumishi au watumishi wake, bila ya kujali umri au jinsia. Hata mtoto aliyezaliwa saa moja kabla ya kuandama mwezi wa Shawwaal, anapaswa kutolewa sadaka ya Zakatul-Fitr.
3. Zakatul-Fitr ni Zaka ya kutakasa mwili wa aliyefunga, kwa upande mmoja, na hata asiyekuwa na wajibu wa kufunga, kwa upande wa pili, ilimradi umeingia Mwezi wa Rehema na yeye yupo hai. Kwa maana hiyo, Zakatul-Fitri ni Zaka ya NAFSI, SI ZAKA ya mali. Ndiyo maana inampasa kila mtu, mwanamume kwa mwanamke, mdogo kwa mkubwa, muungwana na asiye muungwana.
4. Zakatul-Fitr inapaswa kutolewa kwa aliyoko karibu na aliyoko mbali, ilimradi matunzo yake yapo juu ya mabega ya mzee wake. Hivyo, mwanafunzi anayesoma ugenini–na anayetunzwa na wazee wake–anapaswa kutolewa Zaka yake ya Fitri.
5. Zakatul-Fitr ni mfano wa Sijdatus-Sahw kwenye Swala. Imefaradhishwa ili kuziba mapengo yatayotokea, bila ya kujua, wakati wa kufunga mwezi wa Ramadhani, kwa aliyefunga, au makosa madogo madogo mengine, kwa aliyeruhusiwa kutokufunga–yaani makosa madogo madogo yanayoweza kuchumwa katika mwezi wa Ramadhani. Kwa lugha nyengine ya kisasa: Zakatul-Fitr ni RABA ya kufuta makosa madogo madogo.
6. Kwa maana hiyo, Zakatul-Fitr anatolewa vile vile mtumishi Mwislamu, kwa vile wajibu wa Swaumu upo juu yake kama Mwislamu yeyote mwengine. Ama asiyekuwa mwislamu hatolewi Zakatul-Fitr, maana wajibu wake kwanza, ni kuwa Mwislamu kabla ya kuanza kufunga.
7. Inaitwa Zakatul-Fitr kwa sababu ni Sadaka iliyokusudiwa kumlisha masikini katika siku ya Idi. Yaani ni Zaka ya kumsaidia masikini aweze kufungua kinywa Sikukuu ya Idi, na afurahike kama wanavyofurahika Waislamu wenziwe wenye kujiweza.
8. Kutokana na sababu hiyo kuu, ndiyo maana inatakiwa itolewe KABLA ya Swala ya Idi. Na kama itatolewa mwishoni mwa Ramadhani ni bora zaidi. Hivyo, mwezi mzima wa Ramadhani, hadi kabla ya kuswaliwa Swala ya Idi, ni muda halali wa kutoa Zakatul-Fitr.
9. Kwa vile lengo la Zakatul-Fitr ni kumlisha masikini, basi kinachotolewa ni chakula kinacholiwa sana katika jamii. Hivyo basi, ama ni ngano, shayiri, tende, kitoweo kikuu (samli) na kadhalika. Kwa jamii zetu, ni mchele, sembe, maharage, ulezi nk.
10. Kwa sababu kumetajwaa “Kumlisha” au “Chakula” kwa masikini, basi maulamaa wengi, wanashurutisha kutolewa chakula chenyewe na si mbadala wa chakula. Huu ndio msimamo rasmi, wa Imam Shafi, Malik na Ahmad.
11. Hata hivyo, Imam Abu Hanifa–na anaungwa mkono na maulamaa wengi kutoka madhehebu zote nyengine–inajuzu kutoa mbadala, yaani thamani ya chakula kikuu cha jamii–maana lengo ni kumwezesha masikini kujipatia chakula siku ya Idi, na siyo kumlazimisha kula chakula kinacholiwa na watu wengi kwenye jamii. Amejenga hoja yake kwamba siku ya Idi, mtu hupenda kula kile ambacho ni nadra kukipata. Hula chakula tunu. Kwa hivyo, anaweza kupewa thamani ya kiwango kinachotakiwa kutolewa.
12. Kiwango cha wastani ni pishi moja ya chakula cha kawaida–sawasawa na kilo mbili na nusu.
13. Kwa nchi kama zetu za Afrika ya Mashariki, mchele wa kawaida huuzwa mfuko wa Kilo TANO kwa bei ya baina ya shilingi 10,000 hadi 12,000. Hivyo, kilo mbili na nusu ni sawa na 5000 hadi 6000 kwa kila mtu mmoja (sijui bei za sasa ni kiasi gani. Ila kigezo ni hicho cha mfuko wa kilo tano). Bila ya shaka, bei ya sembe itakuwa tofauti na bei ya mchele, ila kwa vile sembe ni kitu kinacholiwa sana na watu wengi wasiojiweza, na hula wali nyakati za furaha na nadra, basi ni bora kutoa mchele kuliko sembe.
*INAENDELEA …*
والله أعلم وبالله التوفيق
الحقير إلى الله تعلى الدكتور السيد عبدالقادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef
Kutoka “Kitalu cha Waja Wema: Maneno ya Muokozi wa Umma”, kitabu ambacho ni tafsiri kamili ya رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين للإمام النووي kilichotungwa na Imam An-Nawawi na kufasiriwa kwa Kiswahili na Sayyid Abdulqadir Shareef Aal Shaykh Abi Bakr bin Salim.
NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, na kuweka kwenye FB yako, WhatsApp, na kwenye Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, kwa lengo la kusambaza na kuelimisha Dini. Changia kusambaza Dini, ujipatie thawabu.
kcwajawema@gmail.com