Ulaya na Marekani: Sasa kiuchumi taabani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulaya na Marekani: Sasa kiuchumi taabani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sammy Sr., Nov 14, 2008.

 1. S

  Sammy Sr. Member

  #1
  Nov 14, 2008
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulaya na Marekani rasmi sasa hoi bin taabani WATANZANIA TUANZE KUJIANDAA KUFUNGA MIKANDA KWA MIEZI ISHIRINI NA NNE na pengine zaidi na kama tusipokuwa watundu na wabunifu na kuachana na mazoea basi mamb o yanaweza yakawa magumu zaidi. Mkakati mmoja ni kuacha kukumbatia nchi za Magharibi na k uanza kuzikumbatia nchi za BRICs.


  KATIKA miezi hii iliyobakia kufikia Juni 2009 Watanzania tunatakiwa kurudia somo la Ujamaa na Kujitegemea kwa makini sana.

  Maana imetangazwa rasmi kwamba nchi za Ulaya Magharibi na awali Marekani yenyewe zimeingia katika hali ya uchumi inayoitwa 'depression' au 'recession' au 'deflation'
  ambayo ni hali inayoendana na watu, makampuni na nchi kukosa fedha za kutosha kuwekeza na kuzalisha kwa kiwango cha juu zaidi kuliko ongezeko la watu, kupanda gharama za maisha na vitu kama hivyo.

  Hii ina maana kwamba nchi kama Uingereza zitapunguza matumizi yake mbalimbali katika nchi ambazo wanaona wanatumia zaidi kuliko ya kile wanachopata, mathalani, Tanganyika na Zanzibar na kuzijali zaidi nchi wanazopata kuliko wanavyotumia kama vile Kenya na Rwanda.

  Kwa mantiki hii, utegemezi wa Tanzania kwa Uingereza na Marekani kutokana na maono na mtazamo dhaifu wa uongozi wetu umetufanya tule chuya.

  Hivi sasa, ili tusipate hasara zaidi, inatakiwa pia tushirikiane kwa kila namna na nchi nyingine kama vile zile za China, Russia, Uarabuni, Marekani Kusini na kadhalika ili kutoweka mayai yetu yote kwenye kiota kimoja. Yanaweza yasianguliwe yote na yakaishia kuwa viza na kuyatupa.

  Kwa mtazamo wangu binafsi ninadhani huu ni wakati muhimu wa kujenga mkakati na mbinu za kushirikiana kikweli kweli na Uchina ili waweze:

  . kututengenezea matrekata ya bei nafuu,
  . mitambo mbalimbali inayotumia nishati tofauti na mafuta na umeme na hasa ile inayotumia gesi, upepo na nishati ya jua,
  . kuunda vifaa mbalimbali vya mahospitali, mashule na maofisi kwa gharama nafuu,
  . kutengeneza vyombo mbalimbali vya usafiri wa anga, majini na nchi kavu vinavyotumia nishati mbadala badala ya peteroli na dizeli,
  . kutuundia mitambo ya kupampu na kusambaza kwa maji inayotumia upepo, nguvu za maji au gesi,
  . na vitu vingine mbalimbali ambavyo itawezekana kwa kuwa mashine zilizokuwa zikinguruma kutengeneza vitu vya kuuza Ulaya na Marekani sasa imenyamaza na inataka shughuli mpya kufufuliwa.

  Hebu tuliangalie hili kwa makini maana kwangu huu ni mwanzo wa nchi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutumia rasilimali mali asili na rasilimali watu na ushirikiano na nchi za BRICs, yaani, Brazili, India, China na kama hizo kupunguza gepu kubwa kati ya nchi tajiri na sisi.
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana nawe Mkuu Sammy Sr.......once again you are hammering good stuffs at JF.......however, hapa najiuliza aren't these BRICs undergoing similar situation as we are?..........In addition to what you have just said.....nafikiri pia serikali yetu inapaswa kuchukua hatua zifuatazo........

  1. Ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.......kwa mfano strategically yale matangazo ya utalii pale Uingereza sina hakika sana kama yatatusaidia sana.....naambiwa tumetumia TShs 800 millioni kwa kipindi cha miezi sita......pale nilimuona Waziri, Katibu Mkuu + Wakurugenzi wake + Wafanyakazi wengine wa Wizarani................
  SAFARI ZA VIONGOZI NAZO ZIPUNGUE....alah

  2. Hatua za makusudi zichukuliwe kuchochea kilimo bora .....ofcourse at a bigger scale

  3.Hatua za makusudi mbali na kufufua pia ku-support local industries

  4. Miundo mbinu kama Barabara nimuhimu nayo ikapewa special attention


  Kinachoniudi sana sana sana.......ni kuwa hivi sasa tulitakiwa tuwe tunapiga miluzi tukii-enjoy madini yetu.....lakini ndio hivyo tena MIKATABA MIBOVU....inaendelea kutuangusha.........kwani tunaweza kuchukua hatua nzuri sana kwa maendeleo yetu lakini jamaa wanakuja na IPTLs, RDCs, et al........yaani inaudhi sana
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Nov 15, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Tanzania ilipotea sana ilipoamua kuvunja vunja siasa ya "Ujamaa na Kujitegemea." At least wangekataa siasa ya "Ujamaa" wakasisitiza siasa ya "Kujitegemea;" lakini naona viongozi wetu waliamua kuwa tutaanza kujenga siasa ya "Ubepari yenye Kutegemea Misaada na Maamuzi Kutoka Nchi za nje." Tumekalia kaa la moto.
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kichuguu,

  Hivi karibuni nilikutana na mzee mmoja, ambaye zamani aliwahi kuwa RC wa Mara, under Mwalimu, akanipa a very interesting story kuhusu "Kiabakari Mines" mkuu unajua lolote kuhusu hili?
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Nov 15, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hili swali nadhani umelielekeza kwa Ogah.


  Ma-RC waliongoza mkoa wa Mara wakati wa mwalimu ni pamoja na Luhangisa, Auckland Mhina, Stephen Wassira, Nsa Kaisi, na Butiku kama kumbukumbu zangu ziko sahihi.


  Ninavyojua mimi, katika maeneo ya Kiabakari na Mugeta kulikuwa na deposits za dhahabu. Hata hivyo nilikuwa nadhani Jeshi la wananchi lilikuwa linamiliki sehemu kubwa ya ardhi iliyokuwa na dhahabu pale Kiabakari. Hiyo ni kumbukumbu yangu ya zaidi ya miaka 30 iliyopita. Leo hii kuna nini kweli sijui.
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni nilipata bahari ya kuongea kwa muda mefu sana na mmoja wapo kati ya uliowataja, akanipa avery moving story kuhusu madini ya "Kiabakari Mines", sikuwa ninajua kuwa kulikuwa na kitu kama hicho na kwamba Mwalimu aliwafukuza wazungu waliokuwepo hapo wakichimba madini hayo, kwa sababu ya uhuni wa kutuibia wananchi.
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Nov 15, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nadhani hayo yanaweza kuwa na ukweli. Sehemu kubwa ya ardhi iliyokuwa na dhahabu pale Kiabakari iliwekwa chini ya jeshi lwa wanachi (wakati ule ikiwa Batallion ya 10), na sehemu za Mugeta na Rwamukoma ambazo nazo zilikuwa na traces za dhahabu ziliwekwa chini ya JKT. Unajua Nyerere alikuwa na imani kuwa Watanzania tutakapoamka sawasawa ndipo tutakapoanza kuyatumia madini yetu; akasema kuwa hayataoza huko ardhini yakiusbiri wana wa nchi hii wayatumie. Kosa kubwa sana akaacha nchi chini ya watu wasioona hivyo.
   
 8. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Siku zote watoto wa matajiri huwa na matendo yanayoleta umaskini wa kufisha. Hii iko wazi kwa wataofanya survey katika jamii zetu ambazo wananchi na pengine vijana wa familia tajiri wengi wao wanaporithi mali za wazazi au jamaa zao wao hawataweza kuzifikisha kwa watoto wao zitaishia njiani; hujali zaidi anasa kuliko ku-maintain mali.

  Sii kama hata wahindi wafanyavyo sisi Watanganyika ni wine, beer, nyama choma, ufuska, tamaa ana ulafi wa mambo ya anasa kuu inayohitaji fedha nyingi na matokeo ni outlet kuwa kubwa kuliko inlet then ukame.

  Hivyo hawa jamaa walioko na mamalaka hivi sasa ni sawa kabisa na vijana waliorithi mali kutoka kwa babaze na kubadilika kuwa mabazazi. Sijui maana kamili ya bazazi but nafikiri ni terminology mahsusi hapa labda.
   
 9. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #9
  Nov 15, 2008
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0


  Ulaya na Marekani kutakuwa na kupoteza kazi sana hasa kwa watu ambao hutegemea kazi za kubangaiza zinazohitaji visomo vidogo kama vile college diploma,associate degrees,high school graduates au wasio na elimu kabisa walioko katika sekta zisizo rasmi kama za sanaa,Ngo n.k Wasomi wengine nao watajikuta pabaya maana ajira zitakuwa si za uhakika sana waweza pata kazi mwezi huu ukaja ujao ukajikuta huna kazi.

  Njia mojawapo ya kujikwamua kwa kila mtanzania aliye nje ya Tanzania kama ana ki akiba kidogo afikirie kutumia uwezo wake kuwekeza Tanzania ambako sekta zote zina nafasi bado ya kuwekeza kwani hata kama waweza kukuta biashara ziko nyingi lakini bado nyingi hazifikii kiwango cha ubora wa kimataifa ziwe za huduma au uzalishaji hivyo ukija na viwango vya ubora zaidi waweza pata wateja.Pia bado soko ni kubwa kuna maeneo mengi hayajafikiwa na wafanyabiashara serious kuna machinga wahuni tu maeneo mengi ya biashara ambao huendesha biashara duni,kiduni duni ambako akitokea mfanyabiashara serious aweza wapiga mateke ya hali ya juu na kuwatupa nje ya goli la biashara na akawachukua wateja wao wote.

  Mtu ukiwa umekaa nje ya nchi ukapata exposure ukiamua kwa dhati kuwekeza Tanzania eneo lolote lazima uibuke tajiri tu.Ushindani Tanzania ni mdogo na si tishio labisa kiasi kuwa mtu yeyote serious akiamu kijitosa awe mtanzania au si mtanzania aweza fanikiwa kirahisi mno hasa kama kakaa nje ya Tanzania akajifunza ule utamaduni wa kudhamiria,kujituma kudhibiti barabara eneo la mapato yanayoingia na matumizi,kusimamia barabara na kuwabana wafanyakazi uliowaajiri ili uhakikishe wanakuzalishia unachotaka wazalishe kabla ya kuwalipa ,kusimamia raslimali za kibiashara na hadhi ya biashara na mfanyabiashara lazima mtu uibuke tu.

  Nchi nayo iharakishe kuidhinisha suala la uraia wan chi mbili ili watu watanzania walioko nje ya nje waliochukua uraia huko wajisikie huru zaidi kurudi kuja kuwekeza visenti vyao walivyochuma.

  Mfano eneo la kilimo cha mashamba makubwa ya vyakula na uwekaji viwanda vya kusindika vyakula (FOOD PROCESSING AND PACKAGING) kwenye hayo mashamba makubwa kwaweza zalisha faida ya ajabu kwa mtu ambaye aweza amua kujitosa kilimo cha mashamba makubwa na kusindika vyakula na kuviuza vikiwa na brand name ndani na nje ya nchi.Eneo la kilimo la mashamba makubwa Tanzania liko wazi halina wakulima wakubwa wa kibiashara wanaozalisha kwa viwango vya hali juu vinavyokubalika kimataifa na kufanya food processing na packaging kwenye viwanda vilivyomo mashambani mwao.
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Nov 15, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  FMES,Kichuguu,

  ..tungefuata mfano wa Botswana,Saudia,Kuwait,UAE,... wa kuchimba madini wakati huo huo tukijenga uwezo wa kujitegemea ktk sekta nyingine.

  ..mimi nafikiri mikataba ya madini ingesainiwa kipindi kile cha utawala wa Mwalimu labda tungepata deal nzuri kuliko hizi za sasa hivi.
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wacheni hizo ndot za mchana biashara imesimama ulimwengu mzima hakuna Marekani wala kusini,kila raia wa nchi hiyo au hizo hivi sasa anabana matumizi,kwa uangalifu zaidi ikiwa mpo nchi za nje basi hakikisha fedha yako iliyoko benki unaikwapua kwa haraka na kuitunza nyumbani ,bakiza kiasi kidogo tu ili account isifungwe.kwani fedha ikikosekana katika benki na wewe unahitaji ukiingiza kijikadi chako tena kama una bahati utapata nusu ya unachohitaji na kama benki imekauka utaambiwa machine out of order.
  Muhimu kwa sasa ni kuhakikisha una akiba ambayo huigusi na kuichezea chezea au kujidai unaekeza sijuii unaenda kuekeza Tz ,aloo utaumia huu si wakati wa kuekeza huu ni wakati wa kukusanya ulichonacho na kukipangia bajeti ya kweli kimatumizi.
  Kama unaweza basi ni kununua nyumba au ardhi na sio dhahabu,soko linaonyesha kila kitu hakina mnunuzi hata wakipunguza bei badu watu wamebana ndio ukaona kila kitu kimepwaya na kila mmoja anamtazama mwenzake ,hizo fedha za uokozi kila zikiingizwa kwenye mabenki huwa zinayeyuka ghafla na kuifanya benki kuwa tupu,hii inaashiria kuwa wateja wanaziondoa fedha zao mabenki..mpo ?
  Nchi zote zenye viwanda hivi sasa wenye viwanda wamejaliwa na mabidhaa hakuna anae nunua kimataifa.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Nov 15, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa la Mwalimu ni kuwa hakutaka hata chembe moja ya raslimali zetu ichukuliwe na watu wa nje. Kama angepunguza ukali huo na kuwaruhusu wachukue angalu asilimia 20 na kutuachia asilimia themanini basi leo hii tungekuwa ahueni sana.
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Kichuguu:

  Usiumize kichwa na watu hawa. Wengi hawataki hata kuuza ng'ombe kupeleka watoto shule.
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Watu mnapo-bonda uchumi wa Marekani na Ulaya wakati 40% ya bajeti yetu inategemea nchi hizo.

  Ubondaji huu unakuwa kama yule mkata tawi la mti ambaye amekalia tawi lenyewe.
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu Zakumi, si kwamba watu wanabonda, ni ukweli usiopingika kuwa kuna matatizo ya kiuchumi Ulaya na Marekani, iwe tinawategemea au vinginevyo
   
 16. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Ogah;
  excellent summarization!! Kama muungwana anasoma hapa alibidi akutumie PM umpe-advise; that is what we were supposed to be doing in the passed 10 years! bravo Ogah!
   
 17. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Mtoa hoja hii pamoja nawe ilibidi muelewe kuwa Duniani Uchumi ni mbaya mno; siyo Marekani Wala Ulaya pekee. China, Russia, Japani everywhere. China juzi katoa Dollar 586billion stimulus; Japan, Korea, wote hawa washatoa stimulus. For China to grow it needs a rich USA, rich EU and rich Japan to boost its export oriented economy. The situation in China now is even worse; plants/factories are closing people are loosing their jobs.

  Ikifika mwezi wa pili mwakani third world kama sisi tutakula mchanga. I do not see any startegy being taken by our Gov.
   
 18. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkae mkifahamu kuwa hata mikoa itazuia usafirishaji wa kitu chochote toka mkoa kwenda mkoa mwengine hapo ndio JIJI la Dar litakapoonja uvivu wa kulima.
   
 19. M

  Mama JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  sijui hali itakuwaje katika nchi jirani Zanzibar
   
 20. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #20
  Nov 16, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...parapanda limeshalia, huku (ughaibuni) asiyemwana ndie aeleke jiwe, kama huna kazi ndio imetoka, redundancy ndio wimbo wa kila siku, kila kukicha watu wanakuwa laid off makazini, makampuni makubwa makubwa yanafungwa...

  keshanadiwa nyoka huyooo, nyumbani Tanzania watu wanabakia naapite... mara hamadi JOKA lipo mlangoni! hali inatisha jamani... kama alivyotanabahisha ndugu yangu Mwiba, ipo siku Dar mtakula vumbi, kama watu weshasahau ile migao ya unga wa yanga, na mchele wa mdundiko miaka ya mwanzoni 80's, kilio hichooo kinakuja...

  Wachumi endeleeni kutuhabarisha.
   
Loading...