Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Nimesoma mahali kwamba mpaka hivi majuzi nchi za Ulaya ulikuwa hauruhusiwi kumpa mtoto wako jina la Kiafrika, yaani kama wewe ni Raia wa nchi ya Ulaya halafu ukapata mtoto wa Kiafrika ambaye atakuwa raia moja kwa moja sasa labda ukataka kumpa jina la KitanZania sheria za Ulaya haziruhusu, yaani lazima umuite mtoto jina la hiyo nchi!
Na ndiyo maana Mario Baloteli ambaye wazazi wake asilia walikuwa ni wahamiaji haramu ktk Ghana kutokana na ugumu wa maisha ikabidi wamkabidhi mtoto wao kwa familia ya Kiitaliano, sasa ikawa ili aweze kuwa Muitalino ni lazima awe na jina la Kiitaliano na ndiyo hapo alipopoteza jina lake la Kiafrika na kupewa Mario Baloteli!
Na ndiyo maana hata Marekani, Wamarekani weusi wote hakuna mwenye jina la Kiafrika ingawaje walipoondoka Afrika walikuwa na majina yao ya kiafrika, sasa yalienda wapi?
Wazungu wote Wamarekani mpaka leo hii jina lake linaashiria nchi yake asilia ambako wazazi wake walitoka huko Ulaya, na hawajabadilisha!
Je kuna cha kujifunza hapa? Kama Wazungu hawaruhusu kumuita mtoto wako jina la Kiafrika ni kwa nini sisi tunaita watoto wetu majina ya Kizungu? Unakuta mtoto kazaliwa Tanzania anaitwa Michelle, John, Michael, George, Christoph, Ahmad, Mohamad, kwa nini tusitumie majina yetu?
Tena tunakwenda mbali kabisa ukiwa na jina la Kiafrika unachekwa kwamba ni baya, ukimuuliza Mtanzania akwambie jina zuri utasikia Sidney, Florenz, Irene n.k sasa ni kwa nini?