Ulaya bana,kweli mnaoishi huko mna roho ngumu!

ubaguzi uko wapi hapo?, mi naona tu wanashangaa mzazi asiemjali mwanae kumwacha aende shule na baiskeli ya kuendeshea sebuleni nyumbani tena katika umri usiofaa kumwacha aende peke yake. Au ubaguzi ni kumpiga picha?(japo sijui kama aliempiga picha sio baba yake)
 
Mimi naona wanatakakumsaidia na si kumbagua huyu mtoto

attachment.php
 
uzuri wa nchi za ulaya kodi ya wananchi inatumika ipaswavyo, kila mtu anafanya majukumu yake kikamilifu, kwako mtoto mdogo kama huyo kuwa peke yake namna hiyo inaweza kuwa kitu kidogo, lakini wao wanaingia kiundani zaidi. btw ubaguzi upo siku zote , mahali popote.
 
Mtoa mada, siyo lazima uende ulaya! Kama vipi nenda uarabuni, India, China au hata Mongolia...!!
 
Mtoto inaoneka kama kapotea, askari wanajadili jinsi ya kupata wazazi. Hii ndio raha ya ulaya, ingekuwa Uarabuni, India au Uchina, khabri ingekuwa nyingine.
 
Mtoto inaoneka kama kapotea, askari wanajadili jinsi ya kupata wazazi. Hii ndio raha ya ulaya, ingekuwa Uarabuni, India au Uchina, khabri ingekuwa nyingine.

Duh! Maelezo yako yamenipa mshawasha wa kujua zaidi, huko kwa nchi hizo ulizozitaja, hali inakuwaje kwa mtoto aliyepotea kama huyo?
 
Wote mmekosea.
Huyo dogo alikuwa ame over speed na chombo chake.
 
nani kakwambia Africa hakuna ubaguzi?...........na hii picha haionyeshi lolote katika madai

yako

Mwambie huyo.
Ubaguzi si lazima uwe Ulaya na Marekani tu, ubaguzi upo wa namna nyingi sana hata Afrika, wa maeneo, makabila n.k.
Hata kumuita mwenzako "Kyasaka" ni ubaguzi mkubwa. Samahani kwa mnaotumia neno hilo, kama lina maana mbadala basi mtujulishe
 
Hapo ubaguzi uko wapi? Kumbuka Ulaya ni vigumu kumkuta hata mbwa mtaani bila mmiliki wake, iweje mtoto kama huyo kuvinjari pekee yake? Hapa Bongo mtoto kama huyo unamkuta bara barani na baiskeli yake kama hiyo anendesha bila shida. Huku Ughaibuni huwezi kumkuta mtoto mdogo kama huyo pekee yake mtaani na kibaiskeli kama hicho. Yaani katika hiyo picha Polisi wanajaribu kuhoji ili arudishwe kwao. Hapo huyo mzazi atachepigwa faini.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom