Ulaji wa Panya mikoa ya Kusini: Safari yangu ya siku 37 ilivyonifungua mambo mengi

shukrani, umeongea vizuri, we ni kweli umefanya uchunguzi mwenyewe hujakaririshwa.

kuna watu waliokaririshwa basi wao huishia kuiaminisha dunia kuwa panya hawa wa majumbani ndiyo wanaoliwa huko kusini wakati siyo kweli kabisa. pia huaminisha dunia kuwa watu wote wa kusini (lindi na mtwara) wanakula panya, wote! nimefurahi kuona hata wewe umejiridhisha kuwa si kweli, nikienda ndani zaidi ni kuwa ukweli ni kwamba maeneo yenye waumini wengi wasio waislamu km masasi ndiyo yanaongoza kwa ulaji huo wa panya. aina hii ya panya, pia huliwa maeneo fulani ya morogoro

ila nitajaribu kuweka sawa kidogo kama hautojali, ni kuwa si kila eneo la kusini utaona uuzaji wa panya. ni maeneo yale tu wanayopendelea hiyo kitu kama huko masasi. sehemu kama kilwa kamwe huwezi kukuta kitu kama hicho.
Kwahiyo kiislam panya Ni haram au?
 
Satoh Hirosh yupo sahihi panya wanaliwa sana hata mkoa wa Lindi maeneo yenye wakristo wengi.
Jamaa nimeamua kumkaushia Tu..sipendagi ligi,tena kaungana na Peramiho yetu wakawa wawili wananipinga,wakati Mimi nayajua nje ndani maeneo ya mikoa ya Lindi na Mtwara

Mkoa wa Lindi sehemu km Nyangao,mahiwa,namupa,sehemu za Rondo,Namangale,Baadhi ya vitongoji vya mtama,Nachingwea na baadhi ya vijiji vya Ruangwa vyenye wakristo wengi km luagalala,namahema NK panya wanalika vizuri tu
 
Kuna kisa kimoja cha mwalimu wangu juu ya ulaji wa panya..
nimesoma kusini mkoa wa Lindi shule moja inaitwa mahiwa high school

Mwalimu wangu wa geography aliitwa Mr mwazembe jitu la miraba minne kutoka mbeya alibahatika kupata binti wa pale kijijini,.Ruti za shuleni kwenda kijijini Kwa mchumba wake zilikuwa nyingi sn.

Km unavyojua mikoa ya Lindi na Mtwara ulaji wa panya ni kitu cha kawaida sn,Kwa hiyo mke wa ticha alikuwa mlaji mzuri sn wa panya.Km ilivyo kawaida ya wabongo,ticha alidharau sn watu wanokula panya,lkn Yule dada (demu wake) alikuwa mlaji wa panya..siku moja ticha akaamua kujaribu kuonja..asee Radha aliyokutana nayo,kuanzia siku hiyo akageuka kuwa ndiyo kinara wa walaji panya

Ticha akaenda mbali zaidi,akawa na mtu wake maalumu anachukua panya kwa bili,kisha analipia mwisho wa mwezi mshahara ukitoka..
aisee umenichekesha sana, inaonekana kuna vingi vitamu kumbe hatujavionja tu!

ngoka nijaribu kuongezea kidogo kuhusu huyo mwalimu wako...........

very rough,
baadae alipata ukuu wa shule katika shule moja inaitwa nahukahuka,
baadae akahamia shule flani inaitwa mtua (bado yupo) kama mwalimu wa kawaida,
mkulima mzuri wa nyanya na mbogamboga zingine.....haoni hatari kujitwisha tenga la mchicha/nyanya kichwani na kutembeza!
 
Nimesoma o level pale Kaka
Nimemaliza 2011..Bila Shaka Kwa hili swali lako unapajua mahiwa
Hongera kijana mdogo. Nimesoma Ndanda, tulikua tunakimbia mchaka mchaka toka Ndanda mpaka Nangoo mtoni darajani pale.

Unayoyasema ni sahihi. Wamakonde, ambao wengi ni Waislam hawali panya. Panya huliwa sana wilaya ya Masasi kwa Wamakuwa.
 
Yes ni kweli kabisa.masasi ndy wanakula sn samaki nchanga

Ila mm siyo kijana mdogo mkuu😁😁..tengua kauli yako
 
Safari yenye takribani kilomita 600+ hadi Mkoani Mtwara wilaya ya Masasi kijiji cha Nangoo napata fursa ya kuifahamu jamii ya watu wa mikoa hii japo kwa uchache.

Nikiwa eneo hilo nilipata fursa ya kufahamu baadhi ya tamaduni za kule, baadhi tu kama vile Unyago na aina ya vyakula ambavyo vipo tofauti na vingine.

Achana na kufanya Upupu kama ni chakula ila hili la ulaji panya lilinivutia zaidi, Panya!! Ukuaji wangu umenikuza nikiamini Panya ni sehemu ya wadudu waharibifu wa kwenye nyumba za watu au mashambani.

Biashara ya kitoweo hiki kule Kusini siyo ya kificho, ni biashara ya wazi inayotembezwa kama bidhaa nyingine tu ya kawaida. Panya wanawekwa kwenye mtungo wa mti au kupangwa fungu kwa idadi fulani na kufungwa na kamba.

UPATIKANAJI NA UANDAAJI WA PANYA
Mwanzo nilidhani ni rahisi tu kupata Panya kwasababu ni kawaida kuwakuta kwenye nyumba zetu za kawaida kumbe la hasha! Siyo kila panya ni kitoweo.

Panya wa Porini Vs Panya wa Nyumbani.

Ikae akilini mwako kuwa kule wametofautisha Panya kwa aina hizo mbili, sasa taarifa ikufikie wale Panya wa Porini ambao kwa kawaida wanapatikana mashambani huko hasa ndio maalumu kwajili ya Kitoweo. Muda wangu wote kule sijashuhudia Panya wa nyumbani wakifanywa kitoweo bali uuliwa na kutupwa kama ilivyo sehemu nyingine.

Panya wa Porini wanapatikana kwenye mashimo huko shamba na kuna utaalamu katika uwindaji wake. Sasa tutazame namna wanaandaliwa Panya hadi kuwa Kitoweo.

Wakishapatikana wanaondolewa uhai wao kwa kupigwapigwa chini, hatua inayofuata ni kuwasafisha/ kuwaandaa kwa kuweka viungo kama chumvi na pilipili kiasi halafu unawabanika jikoni kwa moto wa wastani.

Ni kama tu unavyobanika Kuku au vile wamasai wanavyoweka Nyama kwenye Mtungo na kubanika. Baada ya zoezi hilo hatua inayofuata ni kuwafunga mafungu au kuuza mmoja mmoja tayari kwa kitoweo.

JE, INASHANGAZA?
Hapana bali inavutia, hata mimi mwanzo kila nilipojaribu kuonesha kuwashangaa nao walinishangaa kwanini nina washangaa basi tukawa tunashangaana.

Hoja yao wanasema huo ni utamaduni wao na uheshimiwe ni kitu kilichobadili mtazamo wangu juu yao, wanasema mbona ipo jamii inakula Mbwa kitu ambacho kule kusini siyo utamaduni wao kabisa. Mwingine aliniambia wapo watu wa Mkoa fulani wanakula panzi, bahati nzuri kwao waliamua kukipa thamani kitoweo chao.

FAHAMU
Siyo watu wote wa Kusini wanakula Panya HAPANA, wapo wengine ni tofauti kabisa na hawajawahi kula hata mara moja. Nafikiri hii ni kawaida tu kwenye mambo mengi.

Siku zangu 37 za kuishi kusini nilijifunza mengi sana, watu wake ni wema na wakarimu wanaojali zaidi wageni kuliko wenyewe kwa wenyewe. Huu ni udhaifu toka kwao.

Mwisho.
Kula panya wa porini si mikoa ya Kusini tu, hata Zambia na Malawi. Malawi wakati mwingine watoto wanakacha kwenda shuleni ili waende kutafuta panya porini wakati wa kipindi cha jua ambapo almost chakula kinakuwa hakuna. Zambia wanakula pia 'caterpillars' na kama umetembelea familia mara ya kwanza huenda utakaribishwa na bakuli au sahani ya caterpillars kama alama ya kuonyesha heshima kwa mgeni wao.
 
shukrani, umeongea vizuri, we ni kweli umefanya uchunguzi mwenyewe hujakaririshwa.

kuna watu waliokaririshwa basi wao huishia kuiaminisha dunia kuwa panya hawa wa majumbani ndiyo wanaoliwa huko kusini wakati siyo kweli kabisa. pia huaminisha dunia kuwa watu wote wa kusini (lindi na mtwara) wanakula panya, wote! nimefurahi kuona hata wewe umejiridhisha kuwa si kweli, nikienda ndani zaidi ni kuwa ukweli ni kwamba maeneo yenye waumini wengi wasio waislamu km masasi ndiyo yanaongoza kwa ulaji huo wa panya. aina hii ya panya, pia huliwa maeneo fulani ya morogoro

ila nitajaribu kuweka sawa kidogo kama hautojali, ni kuwa si kila eneo la kusini utaona uuzaji wa panya. ni maeneo yale tu wanayopendelea hiyo kitu kama huko masasi. sehemu kama kilwa kamwe huwezi kukuta kitu kama hicho.

shukrani, umeongea vizuri, we ni kweli umefanya uchunguzi mwenyewe hujakaririshwa.

kuna watu waliokaririshwa basi wao huishia kuiaminisha dunia kuwa panya hawa wa majumbani ndiyo wanaoliwa huko kusini wakati siyo kweli kabisa. pia huaminisha dunia kuwa watu wote wa kusini (lindi na mtwara) wanakula panya, wote! nimefurahi kuona hata wewe umejiridhisha kuwa si kweli, nikienda ndani zaidi ni kuwa ukweli ni kwamba maeneo yenye waumini wengi wasio waislamu km masasi ndiyo yanaongoza kwa ulaji huo wa panya. aina hii ya panya, pia huliwa maeneo fulani ya morogoro

ila nitajaribu kuweka sawa kidogo kama hautojali, ni kuwa si kila eneo la kusini utaona uuzaji wa panya. ni maeneo yale tu wanayopendelea hiyo kitu kama huko masasi. sehemu kama kilwa kamwe huwezi kukuta kitu kama hicho.
Ni kweli, hata Lindi na Mtwara mjini huwezi kukuta wanakula hao panya, ni baadhi ya maeneo wilaya za masasi na nachingwea
 
Sjui lini na mie nitembelee Kusini,

Na panya hawana msimu. Hahah

SUKAH
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom