Ulaji sana wa Nyama za Ng'ombe Unasababisha Upofu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Watu wanaopenda sana kula nyama nyekundu kama vile nyama za ng'ombe , mbuzi au 'kitimoto' wana uwezekano mkubwa wa kupata upofu kwenye uzee wao. Matokeo ya utafiti wa wanasayansi umegundua kwamba watu wanaopenda kula sana zaidi ya mara kumi kwa wiki nyama za ng'ombe, mbuzi au kondoo na nguruwe wana uwezekano wa asilimia 50 wa kupata upofu kulinganisha na wale wanaokula nyama hizo chini ya mara tano kwa wiki.

Utafiti huo pia umeonyesha kuwa watu wanaopenda sana kula nyama za kuku walionekana kuwa na kinga dhidi ya ugonjwa unaosababisha upofu kutokana na kuharibika kwa retina ya jicho unaojulikana kitaalamu kama Age-related macular degeneration (AMD) ambao husababisha upofu kwa wazee wenye umri zaidi ya miaka 50.

Utafiti huo ulifanywa na chuo kikuu cha Melbourne cha nchini Australia ambapo wanaume na wanawake 5,600 wenye umri wa kwenye miaka ya hamsini na sitini walifanyiwa majaribio kwa miaka 13.

Ingawa ulaji wa nyama nyekundu ulionekana una madhara, watu walioonekana kupenda kula sana nyama ya kuku mara tatu hadi nne kwa wiki walionyesha kuwa na uwezekano mdogo sana wa asilimia 57 kupata upofu kulinganisha na wale waliokuwa wakila nyama za kuku mara moja au mbili kwa wiki.

Ugonjwa wa AMD kawaida huanza kushambulia mtu anapofikisha umri wa miaka 50 ambapo macho huanza kuvuja vimiminika ambavyo huharibu uwezo wa kuona.

Ni mtu mmoja tu kati ya kumi wanaokumbwa na ugonjwa wa AMD hufanikiwa kupata tiba.
 
Na Fredy Azzah


ULAJI wa nyama nyekundu hasa ya ng'ombe, pamoja na maharage mekundu ni sababu kubwa zinazosababisha magonjwa ya magoti na viungo.

Sababu nyingine zinazo sababisha ugonjwa huo, ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa pamoja na kutofanya mazoezi.

Hayo yamesemwa juzi na Mtaalam wa Mifupa na Viungo wa Hosptali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam Dk Sohail Panawala alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Tofauti na imani ya watu wengi kuwa nyama ya Mbuzi ndiyo husababisha magonjwa ya miguu, Dk Panawala alisema, "Ulaji wa nyama nyekundu na hasa nyama ya Ng'ombe uwezekano wa kuwa na matatizo ya miguu ni mkubwa sana,".

Mtaalam huyo ambaye toka aingie nchini mwezi Februari mwaka huu, ameshafanya upasuaji kwa zaidi ya wagonjwa 100 na wengine wengi kupatiwa matibabu yasiyo husisha upasuaji.

Alisema kutokana na ukubwa wa tatizo la miguu na viungo nchini, mara kadhaa hulazimika kuwa na kliniki ya bure ya mifupa na miguu, ili kutaka kubadilishana mawazo na wagojwa pamoja na matibabu.

Dk Panawala pia alionya juu ya matumizi ya madawa ya kupunguza maumivu, kuwa ni hatari na kuwa huzalisha magojwa mengine.

"Unajua madawa yote yana kemikali na kawaida ya kemikali huwa na madhara (side effect) katika mwili wa binaadamu, tatizo la watu kutumia madawa ya kupunguza maumivu lipo duniani kote lakini ni bora mtu ukiumwa mara moja aende hospitalini ama katika kituo cha afya apate matibabu," alisema Dk Panawala.

Hospitali hiyo ya Aga Khan pia, imefanikiwa kuwafanyia upasuaji wa ubongo, zaidi ya wagonjwa 20 kwa kipindi cha miezi minne.
Mbali na wagonjwa hao, waliopatiwa fanyiwa upasuaji pia wagonjwa wengine zaidi ya 200, wamefanyiwa vipimo mbali mbali vikiwemo vya ubongo na uti wa mgongo.
 
Too much is harmful everybody knows that! Kwahyo tule kwa kiasi. Hakuna madhara yoyote yale. Anayekula mara kumi huyo kashaonekana anakula too much.

Ataanywaye maji mengi pia yanamadhara. Kwahiyo kula kwa kiasi ndipo panatakiwa si kutokula kabisa nyama ya aina yoyote.
 
Back
Top Bottom