Ukwiukwaji wa Haki za Binaadamu Tarime: Waziri Mkuu aomba Msamaha... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukwiukwaji wa Haki za Binaadamu Tarime: Waziri Mkuu aomba Msamaha...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Jun 10, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Katika Kipindi cha Maswali na ya papo kwa papo leo kwa Waziri Mkuu, Mbunge wa Tarime. Mhe. Charles Mwera, ameuliza swali kuhusu vitendo vya udhalilishaji, unyanyasaji na uvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu kulikofanya na polisi mkoa wa kipolisi wa Tarime, cha kuwalazimisha kina mama kuvua nguo zao zote mpaka za ndani, na kuwalazimisha kuwanyonya hao polisi sehemu zao za siri!

  Waziri Mkuu alioneshwa kushtuka na kuguswa sana tukio hilo la Tarime. Kwa mara ya kwanza, Waziri Mkuu Pinda, ameomba msamaha kwa niaba ya Serikali kwa yaliyotokea kama ni kweli yametokea, pili ameitisha kikao cha dharura kati ya Mwera, Waziri wa mambo ya ndani na wahusika wengine, kikao hicho kitafanyika asubuhi hii hii baada ya kipindi cha maswali na majibu.

  My Take:
  Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kupokea hoja ya upinzani na sio tuu kuifanyia kazi promptly, bali pia kuiombea msamaha jamii husika na umma kwa jumla.

  Huu ni ustaarabu wa ziada wa Mhe. Pinda, anayo sifa ya ziada iitwayo 'humility', ndio maana kwenye mauaji ya albino, ni kiongozi pekee ambaye chozi lilimtoka.

  Huu unaweza kuwa ni utamaduni mpya wa serikali kukubali hoja za msingi za wapinzani na kuzifanyia kazi promptly.
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Pasco,

  Nimeisoma habari hii kwa masikitiko makubwa sana,lakini pia nimefarijika kusikia waziri mkuu alivyorespond yamkini hatua sahihi zitachukuliwa dhidi ya polisi waliofanya kitendo cha kinyama kiasi hicho.

  Nadhani Tarime ni kanda maalumu [mkoa wa kipolisi] labda polisi wamechukulia sababu za kuanzishwa kwa mkoa wa kipolisi Tarime ni sababu tosha ya kufanya ushenzi dhidi ya raia.Nategemea polisi wote waliohusika watafukuzwa kazi na kuchuliwa hatua nyingine zaidi za kisheria.

  Napenda kumpa pole mbunge wa Tarime na wakaazi wote wa Tarime kwa mateso na manyanyaso wanayopata.
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kuna mambo yakifanyika mtu unashindwa kuamini kama yanafanyika tanzania hii. Hili tukio la Tarime kwa kweli limetuumiza watu wengi. Hawa polisi wetu mbona kuna wakati wanakuwa kama vichaa? Unawezaje kumvua mwana mama nguo zote na kumlazimisha anyonye nyeti za mwanaume mbele ya kadamnasi? Jamani tuko Tz au Somalia? Ukatili huo na manyanyaso hayo hayavumiliki. Serikali ichukue hatua kwa kweli.
   
 4. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...I am reserving my praises first for the PM untill I hear some heads rolling! This was the most inhumane someone could do to our Mothers.
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  We Pasco, mama yako ananyonya askari halafu unaombwa msamaha unafurahia! namna gani hapa!
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Shalom, hivi nimeonyesha nimefurahi?
  Unaweza kutofautisha kufurahi na appreciation?.
  Mimi ni appreciate humility ya Pinda ambayo, hata rais wako hana, na waziri Masha ndio kabisa. Polisi wamefanya mambo mabayo, maovu na ya ajabu kuliko haya and no one showed any humility japo angalau kusema pole tuu an samahani. Pinda limemgusa kasema pole.

  Ukiondoa Nyerere alipoomba msamaha kiutu uzima na kwa kusema " kufanya kosa sio kosa, kosa kurudia kosa, na kukubali kuwa huko nyuma tulifanya makosa, kiongozi gani kati viongozi wetu wakuu amewahi kuomba msamaha wowote hadharani?.

  Madudu mangapi yamefanywa na polisi bila hata watu kupewa pole, nimesikia kifuta machozi kwa wale waliouwawa Pemba, kilitoka mwaka jana, ni Sh. 50,000 kwa kila familia!, Brother Ditto (RIP), alipomditto yule dereva wa daladala pale Lugalo kwa ditto, serikali ilikimbiza ubani wa 1,000,000 kwa mjane, na VC kumtembelea kumpa pole. Hata wale wachimba madini wa Zombe, umewahi sikia hata pole, au ubani, ua serikali kuomba msamaha kwa yaliyotokea?.

  Ndio maana nikaapreciate hii humility ya Pinda, inaweza ikawa ni mwanzo wa utamaduni japo sio wa kuwajibika serikali, bali kuonyesha concern na ku act first which is "a good thing" na sio kufurahi kama unavyodhani.
   
 7. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Pamoja na kuomba msamahaa, hao askari wamechukuliwa hatua gani mpaka sasa?
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Pasco ndugu yangu Oktoba sio mbali sana, kitu chochote negative kinaeza kuwa na athari kubwa kwa wapiga kura. Kumbuka Gordon Brown aliponzwa na neno bigot, ikabidi arudi kuomba msamaha kwa yule mama na msamaha ukaonyeshwa live ili watu waone waziri mkuu wao anajali.

  hii yote i kubemebeleza kura oktoba 2010, yaani ingekuwa kwenye boxing tungesema wamebanwa kwenye kona.
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nadhani kikao hicho cha pamoja PM, Mwema na Lau ndo kitaamua kuwa wapigwe risasi, wafukuzwe kazi, wapelekwe mahakamani au watoroshwe, hii ni Tanzania. where the obvious does not happen and the unexpected always happens.
   
 10. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Muda wa kura umekaribia...kila mmoja sasa anajitahidi kuwa mwema...angalieni kwa makini. hata hivyo tunahitaji actions zaidi kuliko msamaha hewa...
   
 11. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #11
  Jun 10, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Hizi Response zimekaa kisiasa zaid...
  Waziri Masha akiulizwa hili atasema pia hajui..
   
 12. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #12
  Jun 10, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Alikuwa wapi hadi aje aombe msamaha bungeni tena baada ya kuulizwa!!!!!tusidanganywe na hawa jamaa....tofauti ya Pinda na viongozi wengine ni kwamba Pinda anajua Wa TZ wanataka nini,thats why hata majibu yake yako so smoothe,ila inatusaidia nini kuomba msam,aha tena mpaka uulizwe!!!!in maana alikuwa hajui, ila atlest tunashukuru..angekuwa Masha angejibu "Tunalichunguza hilo na tutalitolea tamko"
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Ngambo Ngali, nakubaliana na wewe kuelekea Octoba, wazee watawaamkia vijana, watoa pesa watatoa pesa na kutanguliza asante, badala ya mpokeaji kushukuru na mengine mengi.

  Ila naomba nimtete Pinda, jamaa ni kweli ana humility, humble na down to earth sio kwa ajili ya kuombea kura. Ndio maana hata kusikika hasikiki sana katika mikiki mikiki ya kuelekea 2015.
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Pasco, kama ni hivyo nakubaliana nawe kwenye second take yako kuwa Mheshimiwa PM ana humility ya Ziadan aya hali ya juu, ni kiongozi aliyejiweka chini ya watu, myenyekevu, anajali shida za watu, lakini maskini hakuna anayemsikiliza.
   
 15. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Miaka ya sabini kuna madudu yaliyofanyika usukumani yanayofananafanana na haya. Pengine Pinda anaweza kujifunza kutokana na hatua zilizochukuliwa na serikali ya kipindi kile. RPC, RSO walihukumiwa kifungo miaka 7 baada ya kusota rumande zaidi ya miaka 3.

  Huu ni uovu mkubwa ambao hauwezi kufanywa na askari wa chini bila baraka za wakuu wao. Kama huyo kamanda wa kanda maalum bado yuko ofisini, huo msamaha unaoombwa na Pinda itakuwa mzaha na kejeli kwa waliofanyiwa uovu huo!
   
 16. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  My take:
  a) Kuomba msamaha haitoshi na kiongozi hatakiwi kuomba msamaha bila kutuambia hatua zinazochukuliwa kwa wahusika.
  b) Mwema umechukua muda sana kutupa feedback ya uchunguzi wako na hatua zilizochukuliwa, WHY WHY WHY? Kuvua watu nguo na unyama huo unahitaji siku ngapi kufanyiwa uchunguzi wakati hadi watoto wadogo wameona?
  c) Fanya uchunguzi wa askari wako mara kwa mara, kuna wagonjwa wa akili, wavuta bange, wala unga, ukizingatia wengi waliingia baada ya kufeli shule. Wasio na maadili watafutie sababu-OUT!
   
 17. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #17
  Jun 11, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kaipokea postively kwa kuwa waniogopa Tarime zaidi ya hapo hakuna lolote.
   
 18. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2010
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Unachokoza mashetani ndugu yangu
   
Loading...