Ukwepaji kodi unaokubalika kisheria, ‘tax avoidance’

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Katika biashara, watu hutaka kupata faida kubwa hivyo hulazimika kukwepa kodi kwa namna moja au nyingine ili kujiongezea kipato. Kwa nchi yetu ya Tanzania, kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakikutwa na kesi za kukwepa kodi na wakakutwa na mkono wa sheria na kuitwa wahujumu uchumi au watakatishaji pesa

Lakini katika ukwepaji kodi, ni muhimu kujua uko wa namna mbili, kwa kiingereza kuna ‘Tax Evasion’ huu ni ukwepaji ambao ukikutwa nao ni lazima uwe na kesi ya kujibu, na kwa hali ya sasa uhujumu uchumi unaweza kukuhusu.

Pia kuna ‘Tax Avoidance’, hii ni namna halali ya kukwepa kodi kwa kuangalia mianya ya iliyopo kwenye sheria za kodi nchini. Kwa mfano, kwa sababu mashirika ya dini hayatozwi kodi, mtu anaweza kufanya namna ya kuwa na taasisi inayojihusha na hayo ili kukwepa kodi, na hatokamatwa kwa kuwa amekwepa kisheria

Mianya mingine mingi ya kisheria ambayo inaweza kumfanya mtu akwepe kodi inaweza fundishwa na washarauri wa biashara ambao kwa kiasi kikubwa wanajua sheria za biashara zilivyo na mianya ya kukwepa kodi husika
 
Huo siyo ukwepaji kodi.

Kiswahili ni 'Uepukaji wa kodi'

Ukwepaji Kodi - Tax Evasion ( Illegal )

Uepukaji Kodi - Tax Avoidance ( Legal )
 
Huo siyo ukwepaji kodi.

Kiswahili ni 'Uepukaji wa kodi'

Ukwepaji Kodi - Tax Evasion ( Illegal )

Uepukaji Kodi - Tax Avoidance ( Legal )
Shukrani, nilikosa kiswahili kizuri cha hizo terms
 
Weka mfano mwengine wa kukwepa kodia.

Kuna Jamaa huwa namuona cartons na cartons za Maji na vinywaji kadhaa, vinatosha kujaza duka/flem lkn anauza jumla kando ya Morogoro Rd. Sa sijui yule anakwepa ama analipa kodi yao?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mfano Bodaboda inabidi walipie SUMATRA, 22,000 kila mwaka. Kukwepa hii anaweza kusajili pikipiki kama binafsi badala ya commercial, kumbuka kbadili usajili ni elfu 20 na hautalipa tena

Hapo atakuwa na plate namba za njano na atakula vichwa bila fujo za SUMATRA, provided ni ngumu kusema kama aliyepakiwa ni abiria au ni sehemu ya familia ya wenye pikipiki, pia haizuiwi mtu kumpa mtu lifti
 
Mfano huu sio sahihi maana mamlaka za usafirishaji zitamtia hatiani hivyo technically atakuwa amefanya kosa

Tax avoidance ni ile hali ya kutengeneza au kulazimisha matumizi ambayo haukuyafanya kwenye hesabu zako, mara nyingi kwenye corporate business unaweza kulazimisha ulifanya donation flani,ulitoa lunch au kuna matumizi ya ziada ya kutibia watu hivyo ukitoa kwenye mapato Kodi inapungua

Mfano uliotoa ni sahihi, lakini pia nasimama kuwa sahihi.

Mamlaka zinakamata kama kifaa cha usafiri ni for commercial use, halafu hakijalipiwa leseni, otherwisehaukamatwi na umeepuka hizo kodi
 
Kwa mfano Bodaboda inabidi walipie SUMATRA, 22,000 kila mwaka. Kukwepa hii anaweza kusajili pikipiki kama binafsi badala ya commercial, kumbuka kbadili usajili ni elfu 20 na hautalipa tena

Hapo atakuwa na plate namba za njano na atakula vichwa bila fujo za SUMATRA, provided ni ngumu kusema kama aliyepakiwa ni abiria au ni sehemu ya familia ya wenye pikipiki, pia haizuiwi mtu kumpa mtu lifti
Hii sio sahihi ni( tax evasion) huwezi kukwepa kodi kwa njia hiyo, ukikamatwa ni kosa. Tax avoidance ina hitaji umakini na sio kila mtu anaweza, kuna wenye fani yao, kwani ni kutumia mapungufu ya sheria za kodi zilizopo. Lakini ukienda kichwa kichwa baba, money loundering itakuhusu!!!
 
Katika biashara, watu hutaka kupata faida kubwa hivyo hulazimika kukwepa kodi kwa namna moja au nyingine ili kujiongezea kipato. Kwa nchi yetu ya Tanzania, kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakikutwa na kesi za kukwepa kodi na wakakutwa na mkono wa sheria na kuitwa wahujumu uchumi au watakatishaji pesa

Lakini katika ukwepaji kodi, ni muhimu kujua uko wa namna mbili, kwa kiingereza kuna ‘Tax Evasion’ huu ni ukwepaji ambao ukikutwa nao ni lazima uwe na kesi ya kujibu, na kwa hali ya sasa uhujumu uchumi unaweza kukuhusu.

Pia kuna ‘Tax Avoidance’, hii ni namna halali ya kukwepa kodi kwa kuangalia mianya ya iliyopo kwenye sheria za kodi nchini. Kwa mfano, kwa sababu mashirika ya dini hayatozwi kodi, mtu anaweza kufanya namna ya kuwa na taasisi inayojihusha na hayo ili kukwepa kodi, na hatokamatwa kwa kuwa amekwepa kisheria

Mianya mingine mingi ya kisheria ambayo inaweza kumfanya mtu akwepe kodi inaweza fundishwa na washarauri wa biashara ambao kwa kiasi kikubwa wanajua sheria za biashara zilivyo na mianya ya kukwepa kodi husika
Tax avoidance is not synonymous to tax evasion. Kukwepa kodi ni tax evasion na KUEPUKA KODI ndiyo tax avoidance. Kwa hiyo Tax avoidance siyo sawa na kukwepa kodi, ni kuepuka kodi
 
Mtu mwenye duka anawezaje kuepuka kodi
Fanya liwe genge, lisiwe duka utakuwa umeepuka. Au haujawahi kuona baadhi ya maeneo mtu anakuwa na boonge la genge na hataki liitwe duka kabisa
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Hii sio sahihi ni( tax evasion) huwezi kukwepa kodi kwa njia hiyo, ukikamatwa ni kosa. Tax avoidance ina hitaji umakini na sio kila mtu anaweza, kuna wenye fani yao, kwani ni kutumia mapungufu ya sheria za kodi zilizopo. Lakini ukienda kichwa kichwa baba, money loundering itakuhusu!!!
How wakati chombo kama pikipiki inakuwa ni private thing, na zipo pikipiki private
 
Tax avoidance is not synonymous to tax evasion. Kukwepa kodi ni tax evasion na KUEPUKA KODI ndiyo tax avoidance. Kwa hiyo Tax avoidance siyo sawa na kukwepa kodi, ni kuepuka kodi
Nakuelewa mkuu, ubaya ni kuwa haya madude tunasoma kwa kiingereza kwa hiyo kuna wakati kuyaleta kwenye kiswahili inakuwa shida.

Hilo swala la marekebisho nawaacha watoa BAN
 
Tax evasion is absolutely a criminal offense; you ought not advise anyone for that!
 
How wakati chombo kama pikipiki inakuwa ni private thing, na zipo pikipiki private
Ndio maana private vehicles zote zina kuwa plate number za njano, ila ikiwa ni ya biashara lazima iwe na plate number nyeupe!! Ndio sheria, sasa wewe unafanya biashara kwa kutumia private vehicle, ni kosa, kwani kuna kodi ambayo ulitakiwa kulipa, ambayo mwenye public vehicle anailipa!! Hiyo lazima iwe tax ni ukwepaji kodi tu!! Kwani kama ni gari huwa kuna tozo za halimashauri pia, kwa gari za abiria.
 
Thus hapo nilitaja pikipiki na sio gari mkuu.

Pikipiki ni rahisi kuwa na plate namba ya njano na kuwa kwenye kijiwe na kupiga shughuli kama kawa
 
Tax evasion is absolutely a criminal offense; you ought not advise anyone for that!
Nimezungumzia tax avoidance, kwa concept

Ningetaka kuzungumzia evasio ningezungumzia madude mengine kabisa
 
Thus hapo nilitaja pikipiki na sio gari mkuu.

Pikipiki ni rahisi kuwa na plate namba ya njano na kuwa kwenye kijiwe na kupiga shughuli kama kawa
Ndio maana nikasema hapo utakuwa unavunja tu sheria, kwa kujua, na mke mkono wa sheria hautaukwepa endapo utakamatwa!! Ila kwenye uepukaji kwa kodi hutendi kosa, kwa makusudi bali ni kwa madhaifu (loopholes) ya sheria za kodi zilizopo, na hata huwezi funguliwa mashitaka ya kikodi!!! Ndio maana hufanywa kwa ushauri wa wataalamu wa mambo ya kodi, sio kila mtu unaweza.
 
Back
Top Bottom