Uchaguzi 2020 Ukweli wenye ukali: Dkt. Magufuli lazima abadilike, runinga ya Watanzania aitazame na kuizingatia

Hawawezi waonyesha watu wamaobeza, kila uchao Serikali ya wanyonge. Chadema Kwa pesa ya ruzuku, ingetosha na nyie kuwa na TV yenu. Tatizo mwenyekiti wenu mchwa Sana, atawatafuna mpaka mwishe nyote.
 
Hawawezi waonyesha watu wamaobeza, kila uchao Serikali ya wanyonge.Chadema Kwa pesa ya ruzuku, ingetosha na nyie kuwa na TV yenu. Tatizo mwenyekiti wenu mchwa Sana, atawatafuna mpaka mwishe nyote.
Issue ni kuwa na TV au sheria mbovu zinazodhibiti vyombo vya habari. Wenye TV wanakuwa controlled na CCM kwa remote. Hawako huru. Ni uduanzi kufanya biashara ya TV Tanzania Kama wewe ni msemaukweli!
 
Umekata tamaa. Wenye akili tulijua utafikia hapo.

Hiyo Runinga pia imeuonyesha udhaifu wa Chadema na Lisu.... eti tuwape nchi kwa sababu walipata majeraha, eti tuwape nchi kwa sababu tumewaudhi mabeberu, eti tuwape nchi kwa sababu wakwepa kodi wameyumba, eti kwa sababu wazembe na wezi wametumbuliwa. NO

Mzee zisome vizuri post zako za nyuma
 

 
Sio rahisi kubadilika. Hali inavo onekana tutarajie hali mbaya zaidi.
Wapinzani wataumizwa zaidi
Kwa visasi
Wafanya biashara watavutwa hela zaidi
Biashara zitadorora
Shughuli nyingi zitasimama kujaribu kuokoa miradi ya umeme na Sgr.
Trafic wata waana zaidi wenye magari.
Na tutatengwa zaidi na dunia
 
Wawaulize Nape, na January Makamba, sijui wanajihisi vipi
Kinana, January na Nape ndio walikuwa wajuzi wa fitina. Waifanye wakati gani na wapi. Lakini huyo mshamba alipoingia akaunda ccm yake na kuwaona hao wote ni maadui. Akiponyoka, kama itatokea, atabadilika sana. Ataona kuwa kumbe ni mshamba na limbukeni tu.
 
Hulka ya mtu kubadilika ni ngumu Sana.Mwalimu wetu alishawahi kutuambia,"Ni rahisi kwa mtu kumtoa shamba kumleta mjini lakini sio rahisi kumtoa ushamba wake".
 
Ni rahisi usiku kuwa mchana ghafla kuliko jiwe kubadilika,kipindi cha kuomba kura ni kipindi ambacho muomba kura anatakiwa awe fala,lakini angalia jiwe alivo,anaomba kura na bado anawatisha wapiga kura kwamba wasipowachagua wabunge wa ccm hawataletewa maendeleo iwapo atapita huku hata huko kupita kwenyewe ni kwa magumashi
 
Duh! Mungu atuepushie hii balaa!! Iddi Amini tena!! Ila kwa namna madaraka yalivyo mlevya, siamini kama atakuja kuondoka madarakani huyu kiumbe kwa hiyari. Labda mabeberu waje kutusaidia maana jeshi letu liko mfukoni mwake.

Kwanza ni muongo na ni mtu asiye aminika kwa lolote. Na kupitia mchakato wa kura za maoni za Wabunge ndani ya chama chake kwa kuwapitisha kibabe watu wake walioshindwa mfano Patrobasi Katambu, Gwajima, nk. na kuwaambia Wananchi kwenye kampeni zake 'mniletee huyu', hakika hiyo 2025, lolote linaweza kutokea.

Binafsi sitakuja nimkubali wala kumuelewa magufuli. Ana mapungufu mengi sana ya kiuongozi. Anaamrisha watu wazima mbele ya hadhara as if ni watoto wake wa kuwazaa. Hana adabu kabisa kwa wasaidizi wake. Mtu wa aina gani huyu!!!
 
Kwanza ni vigumu sana kumfundisha Simba mzee mbinu mpya za kuwinda na pili kwa hulka yake na kwamba hii labda ni awamu yake ya pili na ya mwisho, hana cha kupoteza kwa sababu hagombei chochote tena HAWEZI KUBADILIKA hata kidogo na kuna uwezekano akalipiza visasi katika maeneo yatakayomuonyesha hasira zao kwenye debe la kura! Muda utaongea.
 
Usiwe na wasiwasi atashinda na maisha yatakuwa mazuri zaidi ninaimani utakuwa miongoni mwa watu ambao mtatamani hata aongeze muda (ingawa naamini kwa uaminifu alio nao hawezi kuvunja katiba).

Mazuri yanakuja twendeni tukamchague JPM October 28.

JPM ANATOSHA
CCM USHINDI NI JADI
 
Back
Top Bottom