Ukweli wangu kuhusu utata rambirambi za mjane wa Mwangosi...

M

maggid

Verified Member
Joined
Dec 3, 2006
Messages
1,084
Likes
398
Points
180
M

maggid

Verified Member
Joined Dec 3, 2006
1,084 398 180
Ndugu zangu,
Chris Lukosi ameandika haya kwenye Jamii Forums jana...

"Ndugu zanguni

Naona kila kukicha makamanda wa chadema wamekuwa wakiendeleza ile singo yao ya rambi rambi dhidi yangu.

Huu wimbo umenikera sana na nadhani sasa ni wakati muafaka kwa Mchungaji Msigwa kujitokeza hapa na kutoa ufafanuzi ziliko hizo hela ambazo mimi nilizifikisha kwake kupitia Maggid Mjengwa

Sio vyema kwa kiongozi wa dini tena mbunge kukaa kimya kwenye suala kama hili.

Watu walitoa kwa moyo, hivyo ni vyema wajue hela zao kama zilifika au zilitumika kwenye mikutano ya pale mwembetogwa

JITAMBUE!"-
Ref: https://www.jamiiforums.com/habari-...bi-rambi-za-mwangosi-alikabidhiwa-msigwa.html

Mwingine amechangia...

Re: Namuomba Mchungaji Msigwa aje hapa kutueleza ziliko rambirambi za Mwangosi nilizompa.

Hapa kuna watu watatu wanaoujua ukweli wa nani ametafuna pesa za rambi rambi. Chris Lukosi, Maggid Mjengwa, au Mchungaji Msigwa. Lukosi anasema amekabidhi pesa kwa Mjengwa, sasa kama Msigwa anakanusha hakupewa pesa, basi pesa aidha zimeliwa na Lukosi au Mjengwa. Tunataka Maggid Mjengwa aje hapa athibitishe kama ni kweli alikabidhiwa pesa na Lukosi? Na yeye jee alizikabidhi kwa Msigwa?

Embu mwenye namba ya simu ya Mjengwa aiweke hapa tafadhali. " ( Chanzo JF)
Ukweli wangu:

Kwa kufuatilia mjadala kwenye mada hii mtandaoni nimeona dhahiri, kuwa wasionitakia mema wameanza hila za kuliingiza na kulichafua jina langu na rekodi yangu ya kujitahidi kuishi na kutenda yalo mema na kwa uadilifu. Na mengine si ya kuyapuuzia, maana kuna wenye kuamini upuuzi pia. Ndio sababu nimeamua kuweka ukweli wangu hapa...

Baada ya kuawa kinyama kwa rafiki na mwanafamilia mwenzetu katika tasnia ya habari, Daud Mwangosi, niliitisha harambee kupitia Mjengwablog ili kumsaidia mjane wa marehemu na watoto wake.

Yafuatayo yawe wazi;
1. Ni kweli kuwa Cris Lukosi kupitia nduguye Augustino Lukosi aliniingizia shilingi milioni moja kwenye akaunti yangu ya MPESA kama mchango wa rambirambi uliokusanywa UK kutoka kwa wanachadema Lukosi akiwa mwenyekiti wao.( Angalia siku, tarehe na muda kwenye kiambatanishi)
2. Kwenye orodha ya wachangiaji niliorodhesha mchango huo kama kutoka kwa Jumuiya ya Watanzania UK. Ni kwa vile kama mratibu, niliweka wazi kuwa suala hili la msiba na rambirambi halihusiani na itikadi za vyama.
3. Cris Lukosi hakukubaliana na utaratibu huo na kunitaka niwakilishe mchango wao kwa Mh. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na uwakilishwe kwa mjane wa marehemu Mwangosi kama mchango kutoka kwa WanaChadema UK. Nilifanya kama alivyotaka Lukosi ( Ushahidi ni kiambatanisho hapo chini).

Hitimisho: Ukweli wangu ndio huo. Hakuna hata senti moja ya rambirambi kwa mjane wa marehemu Mwangosi iliyopotea mikononi mwangu. Na chini hapo ni risiti ya CRDB ikionyesha fedha zote zilizochangwa na nilizoziingiza kwenye akaunti ya Itika Mwangosi, mjane wa marehemu Mwangosi. Ushahidi wa majina ya waliochangia na kiasi walichochanga pia upo.

Nimeyaweka haya hadharani kwa nia njema ili kuzuia upotoshaji na hali ya kuchafuana majina kama ningeamua kubaki kimya.

Nawashukuru nyote mnaoendelea kuniamini hata mnaposikia yenye kuzushwa juu yangu.

Wenu Katika Ujenzi wa Nchi Yetu.

Maggid Mjengwa.
Iringa.

Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2009
Messages
18,302
Likes
6,018
Points
280
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2009
18,302 6,018 280
Kwa hiyo hakuna kilichoibiwa na fedha ilifika sehemu husika... alkini tarehe za hizo risiti sijazielewa elewa
 
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
13,469
Likes
2,412
Points
280
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined Oct 4, 2007
13,469 2,412 280
Majid pesa ulimkabidhi Msigwa sasa ilikuwa tena ukaziingiza Benki wewe au sijaelewa hapa!
 
J

jzm-teak

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Messages
1,629
Likes
19
Points
135
J

jzm-teak

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2013
1,629 19 135
hata huyo mjane aitwe adhibitishe kama alipata pesa yake, kwani hayo si unaweza kubumba?
 
M

Misterdennis

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2007
Messages
1,678
Likes
192
Points
160
M

Misterdennis

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2007
1,678 192 160
msigwa, (Mchungaji/Rev.)

Unasomeka hapo juu (kwenye attachment) kutumiwa shs 1,000,000/= na Maggid Mjengwa.
Tafadhali njoo useme hadharani kama hiyo pesa ya rambirambi uli ifikisha kwa mjane wa Mwangosi.

Asante
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,598
Likes
526
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,598 526 280
As long as mjane wa Mwangosi au mwanafamilia ya Mwangosi hajalalamika, wengine wote ni mavuvuzela ya Bavicha yanayopaswa kupuuzwa...
 
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
13,469
Likes
2,412
Points
280
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined Oct 4, 2007
13,469 2,412 280
msigwa, (Mchungaji/Rev.)

Unasomeka hapo juu (kwenye attachment) kutumiwa shs 1,000,000/= na Maggid Mjengwa.
Tafadhali njoo useme hadharani kama hiyo pesa ya rambirambi uli ifikisha kwa mjane wa Mwangosi.

Asante
Huenda Majjid ni muumini kanisani kwa Mch. Msigwa hivyo alivyoona kondooo katuma 1,000,000.00 akaona ni sadaka na kwa kuwa makuhani hula madhabahuni basi naye kama kuhani akala!
 
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,476
Likes
3,058
Points
280
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,476 3,058 280
Duh...kwa hiyo "zigo" limebaki kwa Mchungaji?
 
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
31,831
Likes
5,195
Points
280
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
31,831 5,195 280
dah! mambo gani haya hebu njooni mseme kitu hapa!
 
Mentor

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Messages
19,933
Likes
10,924
Points
280
Mentor

Mentor

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2008
19,933 10,924 280
Kwani mjane amelalamika au!??
 
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,476
Likes
3,058
Points
280
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,476 3,058 280
Kwani mjane amelalamika au!??
Labda hajui kama kuna rambi rambi zilikuwa stahili yake!

Lakini kama alivyosema Maggid, kwa kuwa kuna watu wanalitumia suala hili vibaya, ni vizuri ukweli ukawekwa wazi ili kuondoa utata au uwezekano wa watu kutumia suala hili kuchafuana wakati pengine kiukweli halipo. Lakini, kwa sababu ya uwepo wa opportunists, tuhuma kwamba kuna watu wame "kula" pesa za rambi rambi, sio za kupuuzia sana!
 
M

maggid

Verified Member
Joined
Dec 3, 2006
Messages
1,084
Likes
398
Points
180
M

maggid

Verified Member
Joined Dec 3, 2006
1,084 398 180
UKWELI WANGU KUHUSU UTATA RAMBIRAMBI ZA MJANE WA MWANGOSI...

Ndugu zangu,

Cris Lukosi ameandika haya kwenye Jamii Forums jana...

"Nndugu zanguni

Naona kila kukicha makamanda wa chadema wamekuwa wakiendeleza ile singo yao ya rambi rambi dhidi yangu.

Huu wimbo umenikera sana na nadhani sasa ni wakati muafaka kwa Mchungaji Msigwa kujitokeza hapa na kutoa ufafanuzi ziliko hizo hela ambazo mimi nilizifikisha kwake kupitia Maggid Mjengwa

Sio vyema kwa kiongozi wa dini tena mbunge kukaa kimya kwenye suala kama hili.

Watu walitoa kwa moyo, hivyo ni vyema wajue hela zao kama zilifika au zilitumika kwenye mikutano ya pale mwembetogwa

JITAMBUE!"-

Mwingine amechangia...

"JF Senior Expert Member Array

Default Re: Namuomba Mchungaji Msigwa aje hapa kutueleza ziliko rambirambi za Mwangosi nilizompa.

Hapa kuna watu watatu wanaoujua ukweli wa nani ametafuna pesa za rambi rambi. Chris Lukosi, Maggid Mjengwa, au Mchungaji Msigwa. Lukosi anasema amekabidhi pesa kwa Mjengwa, sasa kama Msigwa anakanusha hakupewa pesa, basi pesa aidha zimeliwa na Lukosi au Mjengwa. Tunataka Maggid Mjengwa aje hapa athibitishe kama ni kweli alikabidhiwa pesa na Lukosi? Na yeye jee alizikabidhi kwa Msigwa?
Embu mwenye namba ya simu ya Mjengwa aiweke hapa tafadhali. " ( Chanzo JF)

Ukweli wangu:

Kwa kufuatilia mjadala kwenye mada hii mtandaoni nimeona dhahiri, kuwa wasionitakia mema wameanza hila za kuliingiza na kulichafua jina langu na rekodi yangu ya kujitahidi kuishi na kutenda yalo mema na kwa uadilifu. Na mengine si ya kuyapuuzia, maana kuna wenye kuamini upuuzi pia. Ndio sababu nimeamua kuweka ukweli wangu hapa...

Baada ya kuawa kinyama kwa rafiki na mwanafamilia mwenzetu katika tasnia ya habari, Daud Mwangosi, niliitisha harambee kupitia Mjengwablog ili kumsaidia mjane wa marehemu na watoto wake.

Yafuatayo yawe wazi;
1. Ni kweli kuwa Cris Lukosi kupitia nduguye Augustino Lukosi aliniingizia shilingi milioni moja kwenye akaunti yangu ya MPESA kama mchango wa rambirambi uliokusanywa UK kutoka kwa wanachadema Lukosi akiwa mwenyekiti wao.( Angalia siku, tarehe na muda kwenye kiambatanishi)
2. Kwenye orodha ya wachangiaji niliorodhesha mchango huo kama kutoka kwa Jumuiya ya Watanzania UK. Ni kwa vile kama mratibu, niliweka wazi kuwa suala hili la msiba na rambirambi halihusiani na itikadi za vyama.
3. Cris Lukosi hakukubaliana na utaratibu huo na kunitaka niwakilishe mchango wao kwa Mh. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na uwakilishwe kwa mjane wa marehemu Mwangosi kama mchango kutoka kwa WanaChadema UK. Nilifanya kama alivyotaka Lukosi ( Ushahidi ni kiambatanisho hapo chini).

Hitimisho: Ukweli wangu ndio huo. Hakuna hata senti moja ya rambirambi kwa mjane wa marehemu Mwangosi iliyopotea mikononi mwangu. Na chini hapo ni risiti ya CRDB ikionyesha fedha zote zilizochangwa na nilizoziingiza kwenye akaunti ya Itika Mwangosi, mjane wa marehemu Mwangosi. Ushahidi wa majina ya waliochangia na kiasi walichochanga pia upo.

Nimeyaweka haya hadharani kwa nia njema ili kuzuia upotoshaji na hali ya kuchafuana majina kama ningeamua kubaki kimya.

Nawashukuru nyote mnaoendelea kuniamini hata mnaposikia yenye kuzushwa juu yangu.

Wenu Katika Ujenzi wa Nchi Yetu.

Maggid Mjengwa.
Iringa.
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio
 
Attachments:

  • File size
    54.5 KB
    Views
    4,699
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
37,832
Likes
23,162
Points
280
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
37,832 23,162 280
mnhhhhh pole sana
funny how you end up in the mix always.....

unakumbuka ishu ya kibanda?
 
ndetichia

ndetichia

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Messages
27,735
Likes
2,005
Points
280
ndetichia

ndetichia

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2011
27,735 2,005 280
duu yamekuwa haya tena..
 
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
32,485
Likes
68,509
Points
280
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
32,485 68,509 280
Kila siku jukwaa hili halikosi vioja!
 
Forum statistics

Threads 1,250,290
Members 481,278
Posts 29,727,194