Ukweli wa mashirika ya kutoa misaada, sio kila unachokiona kinaelea kimeundwa


eden kimario

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Messages
9,039
Likes
14,166
Points
280
eden kimario

eden kimario

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2015
9,039 14,166 280
Shetani anatumia vitu vinavyong'aa nje kumbe ndani vimeoza,kumbe ndani kuna mtego wa kukunasa, ukitaka umkamate kuku dondosha mahindi atakufuata mwishowe utamkamata na kumchinja

Kuna mashirika yanayotoa misaada kwa lengo la kusaidia watu kumbe ni kutaka kuwaingiza mikononi mwa shetani
Kuna mashirika ya serikali na kuna mashirika ya vikundi binafsi.
Shetani na yeye ana mashirika yake ya kutoa misaada ya bure,wana mashirika ya kusomesha watoto yatima, kutunza wajane na jamii isiyojiweza kiujumla.

Sera kubwa ya shetani ni kuwafanya watu kuona kila kinachong'aa ni almasi au lulu
Moja ya mashirika ya kishetani yanayofanya kazi zao kwa siri ni ni pamoja na Freemansons, rosicrucia order (AMORC),Eastern order of sacred mystery, Eckankar, Aguarian mystery order, Aetheius society, Golden Dava,science initiation of international society

Lengo la makundi haya ni kutoa misaada kwa watu na makundi mbalimbali na kuwaingiza mikononi mwa shetani.

Mashirika ya kishetani yanafanya kazi zake kwa siri sana,na sera ya mashirika haya ni kutangaza utajiri unaopatikana kwa njia ya mkato.

Kitu ambacho nataka ujue shetani haogopi bible bali huogopa wanaoisoma
Shetani haogopi watu wanaokataa misaada yake ila wanaogopa wanaoangalia ndani ya mashirika kuna nini kinafanyika humo!

Misaada inayotolewa inalenga nini, ila haogopi wanaoona nje ya mashirika bila kuona ndani.

Tujihadhari na misaada tusiyoijua inatoka wapi, tusitegemee misaada ambayo inaweka maisha yetu panya, inayofupisha maisha yetu,na inayofanya ndoto zetu kupotea

Tuombe Mungu atujalie kutambua kilicho chake na kisicho chake


Eden kimario
 

Forum statistics

Threads 1,235,431
Members 474,565
Posts 29,221,679