MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,752
- 5,497
Habari wakuu.
Dunia nzima kama sio sehemu kubwa ya dunia tumeaminishwa kuwa kuna aina mbili za namba.Hata mimi nilijua hivyo hadi nilipokutana na maelezo hayo.
Namba za KIARABU: 0,1,2,3,4,5,6,7,8,9
au
Namba za KIRUMI: I,II,III,V,X,L,D,C,M kama tunavyojifunza kwenye elimu za awali.
Uhalisia ni kwamba tunazoziita namba za KIARABU ni wahindi. Wachina na Wajapani ziliwafikia 718 lakini Wakaziona hazina maana hadi karne ya 19 ndipo wakazikubali tena.
ILI KUWA KUWAJE ZIKAITWA NAMBA ZA KIARABU?
Namba hizi zilivumbuliwa na Mwanahesabu wa India karne ya 1 hadi 4. Mwanamahesabu mwarabu kutoka Uajemi Muhammad ibn Musa al-Khwarismi ambaye ndie anayechukua sifa ya kuwa nyuma ya uvumbuzi huu katika maandiko yake ameweka wazi kuwa alizitoa india na zilivumbuliwa katika kipindi cha dora la GUPTA. Kilichowapa umaarufu sana waarabu hawa Al-Khwarismi na mwenzake Al-Kindi kwa sababu mmoja wao ndio waliofikisha hiyo habari hadi ulaya.
Kati ya Mwaka 967 na 969 , Jamaa aliyeitwa Gerbert na baadae kuwa PAPA SYLVESTER II msomi aliyetukuka aliisoma kwenye vitabu vya waarabu huko hispania. Baadae Leonardo Fibonacce Akasambaza wazo hili ulaya nzima kwa kuziita Namba za Kiarabu na kwa sababu karibu dunia nzima tulipokea mambo mengi kutoka ulaya basi hadi kesho wazo hilo likatapakaa kuwa namba za KIARABU.