Ukweli wa mafuriko ya Lissu wafichuka, ni watoa rushwa CCM wanahaha kwa kuwatuma wafuasi wao

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,471
Hatimaye siri imefichuka baada Katibu itikadi na uenezi CCM, kuwatisha wabunge washindi wa kura za maoni, sasa wabunge hao waibuka na janjajanja wasikatwe.

Mbinu inayotumiwa na mafisadi wa CCM walionunua wajumbe, ni kuwatuma wafuasi wao katika misafara ya Tundu Lissu anayesaka wadhamini.

Lengo lao ni kuitisha kamati kuu CCM ione kuwa Lisu ana wafuasi na hivyo washindi wa CCM majimboni ndiyo pekee wenye uwezo wa kupambana na wagombea wa Chadema vinginevyo CCM itashindwa vibaya sana.

Wanawaaminisha kamati kuu ya CCM kuwa hali ni tete sana na bila wao, mwaka huu ndiyo mwisho wa CCM ila kiuhalisia tunaowaona Mikutano na misafara ya Lissu ni CCM njaa walionunuliwa na mafisadi wa CCM.
 
Najaribu kukuelewa nashindwa. Unamaanisha kuna Ccm wanawalipa watu wajae kwa lisu?
Ndiyo, wakihofia kukatwa. Ni wabunge walioshinda kura za maoni. Wanaitisha kamati kuu ya CCM ione hali ni tete na kukatana kuepukwe kwa mustakabali wa Chama.
 
Hii inanikumbusha kuna timu moja ya hapa nchini ilikwenda nje ya nchi kucheza mechi ya kimataifa ikaishia kupata kichapo.

Kisingizio waliporejea?

"wenyeji wetu walitupa msosi uliokuwa na pilipili kibao"!!
 
Hao wanaojifanya bila wao sisiemu itashindwa ndio watakaokatwa, na mwekt wao hapendi kusikia hivyo, hukumbuki ya nape? Ila sidhani kua ndio wamewatuma wafuasi wao kwa lissu, lissu ana wafuasi wake automatikali, tena alipo lissu masisiemu hua yanajikunyata ndani na kusikilizia tu
Hapana, wengi wametumwa na mafisadi kutikisa kiberiti kwa CCM. Siasa mchezo wa hovyo Sana.
 
Kauli ya Polepole imewakosesha usingizi, timing ya kutolewa kwake kabda. CCM wafanye maamuzi baada ya kujiridhisha kutoka kwa wananchi wa jimbo husika mwisho wa siku ndio wapiga kura.

Dalili za mvua ni mawingu, uhalisia wa mambo sehemu kubwa ya Tanzania kukubalika kwa Lussu, Dodoma ilitupa picha yake siku ya uchukuaji wa fomu. Haya mengine ni muendelezo wa genge la wale jamaa waliomtuma mtu wao Dodoma kumuuliza Mkt swali la"Nimetumwa Mkt ni kuulze"
 
Back
Top Bottom