Ukweli wa Kiini cha Mgogoro wa Waisrael/Wayahudi na Wapalestina

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,256
Mgogoro wa Israel na Wapalestina Chimbuko na Ukweli wake.

Je Wayahudi wana haki ya kuishi eneo la Mashariki ya Kati? Je hakukuwepo Kundi la wenyeji waliofahamika kwa jina la Wapalestina toka mwanzo? Je Wayahudi si kwamba walifika mara baada ya Vita ya Pili ya Dunia na kuchukua Ardhi hiyo toka mikononi mwa Wapalestina?

Haya ni maswali mengi ambayo watu wamekuwa wakiuliza nap engine kuamini mambo flan kuhusiana na maswali haya. WAYAHUDI waliishi nchi ile toka siku za Musa na ndio inayofahamika kama nchi ya ahadi pale Musa alipowatoa Waisraeli/Wayahudi toka Utumwani Huko Misri.Pamoja na kuwa walipata wakati mgumu wakati mwingine kupigana na Wasiria na Wababiloni ila kwa miaka yote hiyo ilibaki kuwa ni nchi ya Wayahudi mpaka walipokuja Warumi na kuwasambalatisha. Tito mtoto wa Mfalme aliliharibu Hekalu mwaka 70 Baada Ya Kristo na baadaye karne ya Pili Mtawala Hadrian alizima Uasi wa Wayahudi. Kipindi hiki Wayahudi wengi sana walifukuzwa na wengine wakachukuliwa Utumwani na Warumi.

Idadi ndogo ya Wayahudi walibaki katika ardhi hiyo mpaka ilipofika karne ya 20. Hata hivyo Jina la nchi hii lilibadilishwa kwa kuwa Hadrian alidhamilia kufuta kabisa uwepo au utambulisho wa Wayahudi. Na Hivyo akaiita hii nchi kuwa ni Syria-Palestinia” Palestinian i neno la Kilatini likimaanisha Philistine au kwa jina Maarufu Wafilisti hawa ambao tunakumbuka mara nyingi walipigana sana na Waisrael na kama umewahi kusikia kisa cha Daudi na Goliathi ambaye alikuwa ni Mfilisti au Samsoni na Delila. Hawa walikuwa ni maadui wakubwa wa Waisrael. Ukitaka zaidi vifungu vipo kwenye Biblia.leo nimeleta habari hizi Kihistoria si Kiimani au kufuata Biblia. Kwa hiyo Hadrian kwa makusudi kabisa aliamua kuwaudhi na kuwatukana Wayahudi.

Hivyo hakukuwa na nchi iliyokuwa ikiitwa Palestina. Hili lilikuwa jina la Utani kwa nchi Takatifu lililotolewa na Warumi. Watu wanaojiita leo hii kuwa ni Wapalestina ni Waarabu na siku zote walikuwa wakijitambulisha kuwa wao ni Waarabu mpaka Walipokuja kuitwa kuwa wao ni Wapalestina na Mwanzilishi wa PLO Yassir Arafat (Mungu aiweke roho yake panapostahili amen) Mwaka 1964.

Hata tungesema ni Kweli kuwa Waarab walishi Katika ardhi ile kwa Karne nyingi

Kwa miaka mingi waarabu wamekuwa wakipatikana sehemu nyingi nyinginezo lakini hawakuwah kuwa katika ardhi takatifu kwa kiasi kinachoeleweka Mpaka wakati Muhamad alipokuja kueneza Uislamu. Na waislamu walifanikiwa kuiteka ardhi yaw a bizantina ambao walikuwa ni Kanisa la mabaki ya Himaya ya Kirumi.

Kwa miaka mingi wakipigana vita vya kidini na vita mbalimbali nchi ikawa inakua chini ya tawala tofaut tofaut chini ya Kanisa la Katoliki na Waislamu. Yaani wakibadilishana kutegemeana na matokeo ya vita hivyo. Mwishowe iliangukia chini ya Himaya nyingine y kiislamu iliyokuwa ikifahamika kama Himaya ya Ottoman au (Ottoman Empire) Baada ya Himaya ya Ottoman kushindwa katika vita ya Kwanza ya Dunia Mashariki ya Kati iliangukia chini ya Utawala wa Uingereza Kuu( Great Britain). Hata hivyo Mashariki ya kati ikawa ni kama Zawadi ya Himaya ya Uingereza. Uingereza haikuwa na Nia wala uwezo wa kulishikiria eneo hilo milele.

Kwa sababu hiyo walianza kuunda states mbalimbali ambazo walishirikisha Waarabu waliowasaidia katika vile vita(kulikuwa na waaarabu ambao waliunga mkono upande wa Uingereza katika vile vita) walipewa states hizi waendeshe mambo yao wenyewe.. neno Arabia lilikuwa tayari limekuwa likitumika kuelezea sehemu kubwa ya eneo hili. Mashariki ya kati hii tunayoifahamu leo haikuwa huru mpaka Uingereza ilipojiondoa katika mambo ya kiutawala ya eneo hili.

Wakati waingereza wakiunda state mbalimbali. Kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa enzi hizo (League of Nations) wakatoa tamko kuwa watatoa nafasi kwa Wayahudi walio sehemu mbalimbali Duniani kurudi katika nchi yao. Na mwaliko au nafasi hii iliitwa Tamko la Balfour. Hivyo Wayahudi wengi waliamua kurudi toka huko walipokuwepo nchini mwao ambako walifukuzwa miaka mingi sana na Utawala wa Kirumi. Hivyo wana hawa wa Ibrahimu wakajikusanya toka Urusi,Ulaya Magharibi na maeneo mbalimbali kurudi nchini kwao kujumuika na wenzao Wakristo na Waislamu waliokuwa katika nchi hiyo ambayo nao waliiona kuwa ni nchi Takatifu.

Wayahudi wengi walipofika walinunua Ardhi kutoka kwa wamiliki Wakiarabu waliokuwepo wakati huo ambayo haikuwa nzuri,ilikuwa ni yenye madimbwi na taratibu wakaanza kuigeuza kuwa ni ardhi nzuri kwa kilimo na kupanda miti kila sehemu. Uchumi ukakua na wakaligeuza eneo hili kuwa zuri hata maeneo yaliyokuwa makame au majangwa.Wakageuza eneo hili kuwa la kuchumi na kazi zikawa zinapatikana kwa wingi Waaabu wengi wakaja wakiona kama ni sehemu yenye fursa. Wakulima na Wafanyabiashara wa Kiyahudi ndio walioweza kugeuza eneno hili kuwa lenye manufaa.

1. SWALI MUHIMU “ NI NANI MWENYE HAKI NA ARDHI/NCHI HII”
Naomba sasa niwaletee chimbuko la ugomvi huu kuanzia miaka ya nyuma kabisa kabla ya Uislamu na ukristo.
Naomba sasa niwaletee chimbuko la ugomvi huu kuanzia miaka ya nyuma kabisa kabla ya Uislamu na ukristo.

MADAI YA HUU MGOGORO
Israel ambayo ina wananchi wa kutoa jamii na makundi mbalimbali ya dini kwa kikubwa ni nchi ambayo inatawaliwa Wayahudi. Ina wakazi wapatao Mil 6.5 na zaidi ya Mil 5.ni wenye asili ya Kiyahudi. Wayahudi duniani kote hudai wao ndiyo wakazi halisi wa eneo hili. Na wao histori yao inarudi nyuma miaka 4000 kipindi cha Ibrahim, Isaka na Yakobo ambao ni wazazi wa Kwanza kabisa kuanza kuishi Nchini hapo. Na hapa tunaona au tunapata Kumbukumbu zao kwnye Kitabu kiitwacho Biblia.

Wapalestina pia wao wanadai kuwa wana uhusiano mkubwa na eneo hilo. Wanasema kuwa waarabu pia walitokana na Uzao wa Ibrahim ambaye alimzaa Ishmael, Esau na wengineo. Wao kiasili ni Wapwa wa Wayahudi. Na hawa wengi wao wanaishi maeneo ya Ukanda wa Magharibi na pia Gaza wakisema wana haki sawa na wayahudi kwa sababu ya uzao huo.

Uwepo wa Wayahudi na Waarabu.
Hebu tuangalie kwa kifupi matukio yaliyopelekea hali iliyopo . inabidi kurudi nyuma mbali zaidi ya mwaka 1948 au 1967. Na hivyo kurudi miaka mingi zaidi kipindi cha waanzilishi wa Makabila haya ya Kiyahudi na Kiarabu. Hebu kwa sasa tuangalie miaka 2000 iliyopita.

Haina ubishi kuhusiana na ukweli kuwa mwanzoni mwa karne ya kwanza 1st C. AD. Kipindi cha Yesu Kristo eneo la Palestina lilianza kukaliwa na Wayahudi. Eneo Kipindi hiki lilikuwa chini ya Utawala wa Kirumi. Hata hivyo Wayahudi waliasi kiasi kwamba Warumi waliuzingira mji wa Yerusalem . mwaka 70 B.K (70AD.) Yaani BAADA ya Kristo. hekali lilibomolewa

Wayahudi wengi waliangamizwa na wengine walifukuzwa katika Huo Mji wa Yerusalem. Na wengi walitawanyika sehemu mbalimbali duniani wakikimbia utawala wa Kirumi uliokuwa katili sana.

Hata hivyo kuna Wayahudi ambao walibaki katika ardhi hiyo hasa hasa sehemu za Galileya na kuendelea na maisha yao ya Kiyahudi.Karne nyingi zikapita weng zaidi wakawa wanarudi kwenye Miji Mikuu ya Uyuda ambayo ni Yerusalem, Hebrofeni,Tiberia na Safed. Huko kulikuwa na makazi ya Kiyahudi toka enzi za Kibiblia. Na kule mwanzo nlisema toka Karne 1 hadi ya 19 hakukuwa na Taifa lililoitwa Palestina. Waarabu na Wayahudi waliishi pamoja kwa amani kabisa.

Kwa mtizamo wa mgogoro ulipo kwa sasa ulichocehwa sana na Imani ya Uislam na Uyahudi. Na hapa tunajiuliza nini athari za kuibuka kwa |Dini ya Kiislamu? Mpaka Karne ya 7 B.K Wayahudi walikuwa wakiishi vizuri pasipo Ugomvi na Waarabu. Na Wayahudi wengi waliishi sehemu mbalimbali za Kiarabu ikiwepo Arabia. Na baadaye akaja Muhamad akasema kuwa haiwezekani kwa DINI MBILI KUKAA SEHEM MOJA katika peninsula ya Waarab. Na kuna sehemu katika quran inayowataka Waislamu kuwachukia au kuwapinga Wayahudi(sitoiweka hapa si lengo langu kuzungumzia dini,ila mtu akitaka naweza weka. Naepuka kuingiza UDINI katika historia) hata hivyo kwa zaidi ya miaka 1300 Wayahudi na Waarabu waliishi kwa kuvumiliana huko Mashariki ya kati.na Hapa lazima pia mjue baadaye Wayahudi pia walikuja Kupata shida sana na kuteswa na Wakristo wakati wa Vita Takatifu.

UZAYUNI NA KURUDI KWA WAYAHUDI.
Karne ya 19 Wayahudi walianza kurudi Nchi Takatifu.na mwisho wa Karne hiyo tuliona mwanzo wa kuanza Uzayuni mapak mwanzo mwa karne ya 20 Waingereza walipoamua kushikiria na kusimamia suala la Wayahudi kurudi Israel kupitia Azimio la Balfrour. Tuliona kule mwanzo kuwa baada ya vita ya kwanza ya Dunia Umoja wa Mataifa uliikabidhi Uingereza kuisimamia Palestina kwa kwa neno Palestina hapa hatumaanishi Jordan peke yake ila mpaka Bahari ya Mediteraniani,Arabia mpaka kwenye eneo la Iraq ya leo. Na pia kuanzia Misri,Lebanoni na Syria. Hata hivyo Mwaka 1921 katika hali ya kujenga imani kwa Waarab wakatoa sehemu ya Jordan Mashariki(Trasnjordan) kwa Sheikh Abdulllah. Na Hii ikawa Ufalme wa Jordan na wakapata mpaka Ukanda wa Magharib eneo ambalo mwaka 1948 likawa Jimbo la Israel. Na mpaka Waingereza wanaondoka mwaka 1948 kulikuwa kumeshaibuka Vita kati ya Wayahudi na Waarabu na Nusu Karne iliyofuatia tumejionea wenyewe.

HISTORIA YA MGOGORO HUU KIBIBLIA.
Ukiona kuwa Biblia si imani yako soma Biblia kama Kitabu cha Historia pia itakusadia kuelewa asili ya Wayahudi na Waarabu.

Ibrahimi ametajwa sana kuhusiana na uhusiano wa Mataifa yote Mawili yaani Waisrael na Wapalestina. Wayahudi na Waarabu wanamchukulia Ibrahim kuwa ni mwanzilishi wa Mataifa yao.Mataifa mengine au asili za watu wengine inasemekana ni Uzao wa Shemu motto mkubwa wa Nuhu. Baada ya Mafuriko Makuu vizazi vya Nuhu vilisambaa Dunia yote.
Ilikuwa ni kutokea kwa Ile Jamii iliyokuwa Ikiabudu Mwezi Kaldea ambako Bwana Mungu alimuita Ibrahim na Mkewe Sara na mpwa wake Lutu kuishi Kaanani. Hili ni eneo Kusini mwa Mto Yufrate kuelekea chini Misri.Hili eneo walikuwa wakiishi Wakaanani, Wafilistini na Makabila mengine ambayo hayakuwa yakimwabudu Mungu. Kwa Imani Ibrahimu aliambiwa kuwa ile laana ya Babiloni siku moja itaondolewa na atafanywa kuwa Taifa Kubwa na ardhi/nchi itabarikiwa. Mwanzo (12:2-3)

Ilikuwa ahadi nzuri kweli kweli. Lakini Ibrahim alipofika Shekem(kwa sasa inaitwa Nablusi huko ukanda wa Magharibi) kwa mara ya kwanza alipokanyaga Kaanani Mungu akamwambia kuwa kwa uzao wake atampatia hiyo Nchi( Mwanzo 12:7) na baadaye Mungu akamwambia nitakupa nchi hii milele (Mwanzo 13:14-15) kuanzia mto wa Misri kusini mpaka kwenye Mto Yufrate Kaskazini Mashariki)......

TUTAENDELEA.....
ASILI YA WAARABU NA URITHI WA NCHI YAO. 
Tito mtoto wa Mfalme aliliharibu Hekalu mwaka 70 Kabla Ya Kristo

Hapa unahitaji kurejea historia yako tena. Hekalu lilivunjwa mwaka 70 Baada ya Yesu na Wayahudi wengi kutawanyika sio mwaka 70 kabla ya Yesu.
 
Haya tuendelee, maana tulikuwa Mahakamani Kisutu kushuhudia mpambano baina ya T. Lissu dhidi ya Jamuhiri.
Na mpaka sasa Lissu anaongoza.

Tundu Lissu apewa Dhamana

Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mheshimiwa Kamanda Tundu Lissu amepewa dhamana Muda huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam.

Mungu mkubwa, Tulianza na MUNGU, Tuko na MUNGU na tutamaliza na MUNGU.

Mapambano yanaendelea.
 
nashukuru kwa kunikumbusha hilo nlikosea kuliweka sawa hili. Ni kweli mwaka 70 baada ya Kristo Yesu. ASANTE SANA.
Hapa unahitaji kurejea historia yako tena. Hekalu lilivunjwa mwaka 70 Baada ya Yesu na Wayahudi wengi kutawanyika sio mwaka 70 kabla ya Yesu.
 
Back
Top Bottom