Ukweli wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar yakimuhusisha mtu asiye maarufu sana, John Okello

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Taifa la Zanzibar limekulia na kudumaa katika uongo, ulaghai, ghiriba, vitisho na mauaji kwa miaka 51 sasa. Vizazi vimelishwa uongo wa uhalisia wa mapinduzi na wanamapinduzi wa kweli wa Zanzibar bila sababu za msingi, lakini kwa maslahi ya watawala wa Zanzibar kwa msaada wa watawala wa Tanganyika leo Tanzania. Ifahamike na kueleweka kuwa bendera ya Taifa huru la Zanzibar ilipeperushwa tarehe 12 Disemba 1963. Na huu ndio uhalisia wa uhuru wa Zanzibar nje ya mapinduzi ya John Okello yaliyotekwa na Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume

Leo taifa la Zanzibar linaadhimisha kile kiitwacho ni mapinduzi matukufu ya Zanzibar, lakini uadhimishwaji huo upo katika msingi ule ule wa kilaghai na ghiriba. Wanamapinduzi halisi wametupwa, hawatajwi wala kukumbukwa popote na zaidi wengi wamefutwa usoni pa dunia. Wamevishwa wengine taji la mapinduzi ilihali hawakujua hata kilichotokea Usiku wa tarehe 12 Januari 1964. Karume huyu Abeid hakujua hata mapinduzi hayo yaliandaliweje na nini kilitoke bali aliyajua mapinduzi yao yaliyokuwa yakiratibiwa Dar es Salaam chini ya Juius Nyerere

Lakini ukweli unaanzia kwenye kundi la watu 300 waliokitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi wa meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.

Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.

Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbalimbali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhidi ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.

John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello. Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.

Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.

Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa "Mapinduzi". Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.
Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.

Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyingine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.
John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye.

John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine.sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito. Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".

Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha" Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na PembaNafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija", " na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"

Huko mjini Dar es Salaam ndani ya kipindi cha mapinduzi kulikuwa kugumu sana, hata Julius aliingiwa na hofu ya utawala wa mkono wa chuma wa Okello, sasa ikaanza kusukwa mikaka ya kumpoka mamlaka Okello, Okello hakuwa na chama cha siasa hivyo Mwalimu akapendekeza liundwe baraza la mapinduzi na Okello awe ndie mkuu wa baraza hilo ambalo ndilo litakuwa na mamlaka yote ya Zanzibar.
Okello alikubali wazo hilo ambalo kikao kilifanyikia Dar es Salaam 1/2/1964, ikakubaliwa urais apewe kiongozi wa chama cha siasa yani Karume lakini asiwe na sauti yoyote katika Zanzibar. Baraza hilo lilijumuisha wapiganaji watiifu wa Okello ambao hawakuwa Wazanzibari asilia. Nao ni pamoja na Field Marshal (John Okello (Mganda) na msaidizi wake, Absalom Anwi Ingen (Mjaluo kutoka Kenya). Wengine ni Saidi Washoto (Tanganyika) sasa Tanzania Bara, Mohamed Kaujore (Mmakonde wa Msumbiji) na Hamisi Darwesh (Tanganyika). Walikuwapo pia akina Abdallah Mfaranyaki (Tanganyika), Saidi Natepe (Tanganyika), Seif Bakari (Tanganyika) na Edington Kisasi (Mchaga wa Kilimanjaro-Tanganyika).

Baada ya mgawanyo huo ilikubaliwa pia Abdulahman Babu awe mkuu wa vyombo vya habari pia akiwa ni mjumbe wa baraza la mawaziri. Walikubalikubaliana kuwa tare 1/4/1964 warejee tena Dar kwaajili ya kumalizia mipango ya kuitawala Zanzibar. Hapo ndipo siku aliyokwenda kufutwa Okello katika ardhi ya Tanganyika na Zanzibar katika msingi na muundo wa kisiasa, viongozi na wajumbe wote wa baraza la mapinduzi walipanda ndege moja kuja Dar akiwemo Mungu wa Afrika Okello, walipofika uwanja wa ndege, itifaki iligeuzwa na John Okello akaambiwa asubiri kushuka awe wa mwisho. Baada ya kushuka wajumbe wote ndani ya ndege ile, alikwende komandoo mmoja wa Kitanganyika aliyeita Mzena ambaye baadae alikuwa kuwa mkuu wa ujasusi. Alimwamuru Okello asalimishe silaha yake na kisha kumwamuru rubani aipaishe ndege kuelekea Nairobi.

Kenyatta alimuambia Nyerere kuwa mtu huyo (Okello) sio wa Kenya hivyo ndege ikaelekezwa Uganda ambako alibwagwa na historia yake ikaishia hapo. Huku nyuma kazi ya propaganda ya kubadili ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli ilisimamiwa na Babu, alipiga propaganda kupitia radio kuwa akiyefanya mapinduzi ni Karume na ASP, hata chama chake cha UMMA Party hakukisemea tena.

Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi. Wanamapinduzi hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika. Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.

Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995, 2000, 2010 na mwingine unatarajiwa hapo Oct 2015. Viongozi walaghai na wenye kujali hali za siasa zao wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani kwa jicho la tatu. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe,

Katika uga huu wa kisiasa nikuwa matakwa ya Wazanzibar katika siasa mpya bado yanafinyangwa bila sababu za msingi. Tutumie mda wetu kumuenzi mwanamapinduzi wetu Che Guevara wa Afrika Field Marshal John Okello baba wa Taifa la Zanzibar.

Niwapongeze ndugu zangu Ahamed Bargash, Mohame Said, Dr Harith Ghasany na wengine wengi japo historia zao zimejaa udini angalau wapigania kurejeshwa kwa historia ya kweli ya Zanzibar
 
Last edited:
Historia ya Zanzibar itanyoka tu pale mkombozi wake Field Marshall John Gideon Okello atakapopewa stahiki yake kama shujaa wa Unguja aliyekata minyororo waliyofungwa ndugu zetu huko Kisiwani na kuutimua utawala wa walowezi kutoka Oman. Jina lake halitasahaulika na njama zozote zinazofanywa kufuta jina lake kama Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar kamwe hazitafanikiwa. RIP Field Marshall.
 
Ipo vyema Mkuu, ila nakuhisi waelezea hii kitu huku joto na hisia dhidi ya Zanzibar zikipanda na kushuka, kiasi kwamba some time unashindwa Ku control hisia zako na huonekanwa wazi wazi utashi wako....
Mwisho ni kwamba sio Kila mtu huwa baba wa Taifa kama huko kwenu mulivyogaiyana hicho kijicheo.. Kisicho mbele wala nyuma maana kikatiba hakijulikani ndio nini...
Hivyo eti kusema John Okello ni Baba wa Taifa la Zanzibar, maana yake niniiiii??? HISIA zilee niokwambia ulishindwa kuzi control, hatukatai kwamba yeye ndio alikuwa Jemedari wa Mapinduzi kama vile kwenye kikosi cha wanajeshi hakosi aliyekuwa mahiri zaidi kwa mapambano... But kuna walee ambao hawapo kwenye Battle field.. wao ndio Ma engineers wa mipango yoote ya kivita, hao ndio Majemedari zaidi... lakini kwa vile hisia na mihemko imekutawala moyoni kwako, hilo kwako haulioniii... waliona la Nyerereee tu kumpiga Iddi Amini wakati yeye yupo Dar wenziwe wakipambana Kageraa.... still wasema Nyerere kapiga Amino Dada, huko ni kuhemkwa...
#HappyRevolDay
#RrvolutionForJustice
 
Taifa la Zanzibar limekulia na kudumaa katika uongo, ulaghai, ghiriba, vitisho na mauaji kwa miaka 51 sasa. Vizazi vimelishwa uongo wa uhalisia wa mapinduzi na wanamapinduzi wa kweli wa Zanzibar bila sababu za msingi, lakini kwa maslahi ya watawala wa Zanzibar kwa msaada wa watawala wa Tanganyika leo Tanzania. Ifahamike na kueleweka kuwa bendera ya Taifa huru la Zanzibar ilipeperushwa tarehe 12 Disemba 1963. Na huu ndio uhalisia wa uhuru wa Zanzibar nje ya mapinduzi ya John Okello yaliyotekwa na Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume

Leo taifa la Zanzibar linaadhimisha kile kiitwacho ni mapinduzi matukufu ya Zanzibar, lakini uadhimishwaji huo upo katika msingi ule ule wa kilaghai na ghiriba. Wanamapinduzi halisi wametupwa, hawatajwi wala kukumbukwa popote na zaidi wengi wamefutwa usoni pa dunia. Wamevishwa wengine taji la mapinduzi ilihali hawakujua hata kilichotokea Usiku wa tarehe 12 Januari 1964. Karume huyu Abeid hakujua hata mapinduzi hayo yaliandaliweje na nini kilitoke bali aliyajua mapinduzi yao yaliyokuwa yakiratibiwa Dar es Salaam chini ya Juius Nyerere

Lakini ukweli unaanzia kwenye kundi la watu 300 waliokitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi wa meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.

Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.

Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbalimbali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhidi ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.

John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello. Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.

Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.

Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa "Mapinduzi". Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.
Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.

Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyingine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.
John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye.

John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine.sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito. Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".

Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha" Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na PembaNafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija", " na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"

Huko mjini Dar es Salaam ndani ya kipindi cha mapinduzi kulikuwa kugumu sana, hata Julius aliingiwa na hofu ya utawala wa mkono wa chuma wa Okello, sasa ikaanza kusukwa mikaka ya kumpoka mamlaka Okello, Okello hakuwa na chama cha siasa hivyo Mwalimu akapendekeza liundwe baraza la mapinduzi na Okello awe ndie mkuu wa baraza hilo ambalo ndilo litakuwa na mamlaka yote ya Zanzibar.
Okello alikubali wazo hilo ambalo kikao kilifanyikia Dar es Salaam 1/2/1964, ikakubaliwa urais apewe kiongozi wa chama cha siasa yani Karume lakini asiwe na sauti yoyote katika Zanzibar.

Baada ya mgawanyo huo ilikubaliwa pia Abdulahman Babu awe mkuu wa vyombo vya habari pia akiwa ni mjumbe wa baraza la mawaziri. Walikubalikubaliana kuwa tare 1/4/1964 warejee tena Dar kwaajili ya kumalizia mipango ya kuitawala Zanzibar. Hapo ndipo siku aliyokwenda kufutwa Okello katika ardhi ya Tanganyika na Zanzibar katika msingi na muundo wa kisiasa, viongozi na wajumbe wote wa baraza la mapinduzi walipanda ndege moja kuja Dar akiwemo Mungu wa Afrika Okello, walipofika uwanja wa ndege, itifaki iligeuzwa na John Okello akaambiwa asubiri kushuka awe wa mwisho. Baada ya kushuka wajumbe wote ndani ya ndege ile, alikwende komandoo mmoja wa Kitanganyika aliyeita Mzena ambaye baadae alikuwa kuwa mkuu wa ujasusi. Alimwamuru Okello asalimishe silaha yake na kisha kumwamuru rubani aipaishe ndege kuelekea Nairobi.

Kenyatta alimuambia Nyerere kuwa mtu huyo (Okello) sio wa Kenya hivyo ndege ikaelekezwa Uganda ambako alibwagwa na historia yake ikaishia hapo. Huku nyuma kazi ya propaganda ya kubadili ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli ilisimamiwa na Babu, alipiga propaganda kupitia radio kuwa akiyefanya mapinduzi ni Karume na ASP, hata chama chake cha UMMA Party hakukisemea tena.

Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi. Wanamapinduzi hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika. Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.

Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995, 2000, 2010 na mwingine unatarajiwa hapo Oct 2015. Viongozi walaghai na wenye kujali hali za siasa zao wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani kwa jicho la tatu. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe,

Katika uga huu wa kisiasa nikuwa matakwa ya Wazanzibar katika siasa mpya bado yanafinyangwa bila sababu za msingi. Tutumie mda wetu kumuenzi mwanamapinduzi wetu Che Guevara wa Afrika Field Marshal John Okello baba wa Taifa la Zanzibar.

Niwapongeze ndugu zangu Ahamed Bargash, Mohamed Said, Dr Harith Ghasany na wengine wengi wanaopigana na kurejeshwa kwa historia ya kweli ya Zanzibar
Ndugu Jericko,
Umejenga hoja, hebu tuangalie makabrasha yaliyobakia.

https://www.youtube.com/watch?v=7uPi3vh2hGE
 
Yericko ukitaka utuaminishe anza na nini maana ya Zanzibar,wapemba walitokea wapi?waarabu walitokea wapi baadae tuje kwenye mapinduzi ya Zanzibar...... hujaeleweka bana
 
anza na historia ya Zanzibar kama neno la asili ya wapi na kwanini iitwe Zanzibar kabla ya Zanzibar iliitwaje acha uongo
 
Angalau Tumepata Lamaana kwa siku ya Leo..

Ule upuzi wakupitisha majeshi na waimba taarabu uwanjani Kamwe hautakaa kumsaidia mtu kujua umuhimu wa maadhimisho haya ya kitaifa..

Yericko Salute u broo
 
Ahsante yeriko, kwa taarifa yako ss wazanzibar hususan wapemba tunajua yote hayo, mtoto akifika umri wa miaka25 lazima ajue Hilo, huwa tunafunzwa kupitia family zetu, kwa taarifa yako baba yake Hamad rashid ndio alompokea na kumchorea michoro okello!
 
Taifa la Zanzibar limekulia na kudumaa katika uongo, ulaghai, ghiriba, vitisho na mauaji kwa miaka 51 sasa. Vizazi vimelishwa uongo wa uhalisia wa mapinduzi ....

Leo taifa la Zanzibar linaadhimisha kile kiitwacho ni mapinduzi matukufu ya Zanzibar, lakini uadhimishwaji huo upo katika msingi ule ule wa kilaghai na ghiriba. Wanamapinduzi halisi wametupwa, hawatajwi wala kukumbukwa popote na zaidi wengi wamefutwa usoni pa dunia. Wamevishwa wengine taji la mapinduzi ilihali hawakujua hata kilichotokea Usiku wa tarehe 12 Januari 1964. Karume huyu Abeid hakujua hata mapinduzi hayo yaliandaliweje na nini kilitoke bali aliyajua mapinduzi yao yaliyokuwa yakiratibiwa Dar es Salaam chini ya Juius Nyerere

......
Huko mjini Dar es Salaam ndani ya kipindi cha mapinduzi kulikuwa kugumu sana, hata Julius aliingiwa na hofu ya utawala wa mkono wa chuma wa Okello, sasa ikaanza kusukwa mikaka ya kumpoka mamlaka Okello, Okello hakuwa na chama cha siasa hivyo Mwalimu akapendekeza liundwe baraza la mapinduzi na Okello awe ndie mkuu wa baraza hilo ambalo ndilo litakuwa na mamlaka yote ya Zanzibar.
Okello alikubali wazo hilo ambalo kikao kilifanyikia Dar es Salaam 1/2/1964, ikakubaliwa urais apewe kiongozi wa chama cha siasa yani Karume lakini asiwe na sauti yoyote katika Zanzibar. Baraza hilo lilijumuisha wapiganaji watiifu wa Okello ambao hawakuwa Wazanzibari asilia. Nao ni pamoja na Field Marshal (John Okello (Mganda) na msaidizi wake, Absalom Anwi Ingen (Mjaluo kutoka Kenya). Wengine ni Saidi Washoto (Tanganyika) sasa Tanzania Bara, Mohamed Kaujore (Mmakonde wa Msumbiji) na Hamisi Darwesh (Tanganyika). Walikuwapo pia akina Abdallah Mfaranyaki (Tanganyika), Saidi Natepe (Tanganyika), Seif Bakari (Tanganyika) na Edington Kisasi (Mchaga wa Kilimanjaro-Tanganyika).

Baada ya mgawanyo huo ilikubaliwa pia Abdulahman Babu awe mkuu wa vyombo vya habari pia akiwa ni mjumbe wa baraza la mawaziri. Walikubalikubaliana kuwa tare 1/4/1964 warejee tena Dar kwaajili ya kumalizia mipango ya kuitawala Zanzibar. ......
Niwapongeze ndugu zangu Ahamed Bargash, Mohame Said, Dr Harith Ghasany na wengine wengi japo historia zao zimejaa udini angalau wapigania kurejeshwa kwa historia ya kweli ya Zanzibar

Nyerere aliratibu Mapinduzi ya Zanzibar?

Je nani aliratibu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?

Kwa nini "Nyerere" alitaka kuitawala Zanzibar?

Je bado "Nyerere" anaitawala Zanzibar?

Wazanzibari ni nani?
 
1. Ndio Nyerere aliratibu mapinduzi kwakutumia mamluki wa Kipumbwi wakiongozwa na kamanda wao Mkwawa, lakini hawakufanikiwa kufanya mapinduzi kwakuwa waliwahiwa na Okello ikawalazimu kuyadandia mapinduzi ya Okelllo.

2. Nyerere aliratibu muungano wa Tanganyika na Znb kwamkono wa CIA, lengo la Nyerere ni kulinda madaraka yako (usalama tgk), huku lengo la USA ni maslhahi ya vita baridi duniani. Yani kuzuia maslahi ya Urusi ya kale.

3. Limejibiwa na namba mbili.

4. Ndio bado anaitawala chini ya uwepo wa ccm na watawala wake Shein nk
 
Yericko katika ubora wako, pole kwa maswahibu yaliyokukuta karibu kamanda, jasusi mbobezi katika kile chama chetu. huwa nakosa raha ya siku nikipitwa hata uzi mmoja kutoka kwako wewe Pasco Mchambuzi Nguruvi3 mungu na awe nanyi katika uchambuzi murua wa siasa uchwara wa chama kile kile zaidi ya miaka 54 na mwezi mmoja sasa na siku 4.
 
Back
Top Bottom