Ukweli Vs Usiri katika MMU....Ni taarifa kiasi gani apewe mwenza?

Hapo (blue) umeniangusha.....Siyo kawaida yako kuficha ficha...Mbona hata zile SRM zinazikufanya kichaa umetueleza??Weka wazi tu, ni 100% unamwaga kwenye public domain ya mwenyewe?

Umenifurahisha kweli... Mie nilifikiri kua nisema kama nivizuri iwe siri ama lah!...lol... But nimeenda kuangalia.. nimenotice kweli i have left something out.... Hicho nilicho quote...

Mambo ya kwenye bedroom...Sanaa iwe kiasi gani na ukweli uwe kiasi gani?? Asilimia ngapa ya yale unayomweleza ni fix?

Mambo ya Chumbani

Mpenzi ambae ni wakudumu hasa Mwenza ni muhimu saana kuwa wazi na wakweli katika issue nzima ya 6/6 if kweli mwataka jenga ndoa yenu katika suala zima la Love making... Mwanzoni hua nivigumu i believe but with time mkishazoeana ni muhimu saana mkawa free and comfortable to talk about it... Tumeona jinsi maswali meengi hapa MMU hupostiwa na kuuliza maswali kibao kuhusu wapenzi wao wakati wa mda wa hilo tendo.. Yale maswali yakiwa directed kwa mhusika hujenga saana na with time mwaweza jikuta compactible...

Naamini in most cases Mapenzi yale ya Gizani ama tu kukutana usiku yameisha/pitwa na wakati... Naamini wapenzi wawe wazi nakueleza what and how the like most (asikubali tu kwenda back doors); Hiio humsaidia hata Mpenzi wako wepesi katika kukuridhisha... Hivo fix katika hili eneo halifai kabisa... Labda kama ni one night stand.. au uko kwenye tempo uhusiano na sex sio kilichokupeleka hapo...
 
Hehehehhehe cheka siku ziongezeke babu!!

Mhhh hivi kwani wa 1947 wanahitaji upendeleo?

Waongelee kidogo tu (siyo upendeleo) ili wasidhani kwamba unawatenga na kupendelea hawa wajukuu wa dot com peke yao.

Hivi kwa hayo uliyosema, unaweza kutuelezea ni asilimia ngapi walau tuziweke wazi??
 
MTAZAMO WANGU....

Past relationships…

Mie naamini kusema kuhusu past relationships… only kama huyo ex- bado mwawasiliana for what ever reasons… (i.e mtoto).. AU labda huyo Ex- yupo mazingira ya karibu na hua mwagongana mitaani… AU Kuna sababu yoyote ya msingi ya kueleza nje ya for the sake of knowing… Sababu kubwa ikiwa watu wamepitia mapito mengi katika relationships… Waweza kuta mwingine alibakwa na ndugu/mtu yoyote when very young/hata ukubwani… Alikua hajitambui alikua mama Huruma but akaja akajitambua na kujutia… Na kwa mwanaume hivo hivo – kwamba alikua player mno mpaka alikua haangali mradi kamaliza haja zake… In this situations unapata edited version of the Story… Sasa why bother??

Mambo Ya Fweza..

Ni muhimu saana Mpenzi/mwenza kujua kiasi cha pesa wapokea ama kutengeneza… But tokana na kwamba wanadamu tume evolve for the worse na watu wameweka saana pesa mbele… inafanya iwe kazi kweli katika maamuzi ya kusema… Kinachochangia uwe wazi au msiri wa mambo ya Fweza ni the way Mpenzi wako alivo… Je nimuelewa?? Ana economise?? Hana tama?? Akaijua una pesa saana ndo hubweteka?? Ni msumbufu wa mahitaji kila mara?? Mwaribifu – yaaani mfujaji (e.g.. Utunzaji wa vitu vya thamani)?? Nae pia ana kipato?? Haya yoote ni ya msingi katika kuweka/kuto weka bayana kuhusu pesa…

Mambo ya Familia….

Kila familia ina mamboa yao ambayo hustahili iwe siri ya family (mara nyingi haya mambo ni ya aibu mno) ingawa huzidiana from family to family… Siri za namna hii hakuna haja ya Mpenzi ama Mchumba wako kujua.. labda on the condition kua akijua basi kutakua na unafuu, ama kufutika kwa hio siri.. otherwise kweli haipendezi… waweza hata sababisha spouse wako ajenge dharau kwa familia yakko – ambayo sio nzuri in the long term…

Mambo ya Chumbani

Ya chumbani DC hayo hubaki chumbani…

U real good u know.
 
Umenifurahisha kweli... Mie nilifikiri kua nisema kama nivizuri iwe siri ama lah!...lol... But nimeenda kuangalia.. nimenotice kweli i have left something out.... Hicho nilicho quote...

Mambo ya Chumbani

Mpenzi ambae ni wakudumu hasa Mwenza ni muhimu saana kuwa wazi na wakweli katika issue nzima ya 6/6 if kweli mwataka jenga ndoa yenu katika suala zima la Love making... Mwanzoni hua nivigumu i believe but with time mkishazoeana ni muhimu saana mkawa free and comfortable to talk about it... Tumeona jinsi maswali meengi hapa MMU hupostiwa na kuuliza maswali kibao kuhusu wapenzi wao wakati wa mda wa hilo tendo.. Yale maswali yakiwa directed kwa mhusika hujenga saana na with time mwaweza jikuta compactible...

Naamini in most cases Mapenzi yale ya Gizani ama tu kukutana usiku yameisha/pitwa na wakati... Naamini wapenzi wawe wazi nakueleza what and how the like most (asikubali tu kwenda back doors); Hiio humsaidia hata Mpenzi wako wepesi katika kukuridhisha... Hivo fix katika hili eneo halifai kabisa... Labda kama ni one night stand.. au uko kwenye tempo uhusiano na sex sio kilichokupeleka hapo...

Duuuuhhhh,

Kweli maendeleo yameshafika mbali...Hivi kweli sijaachwa...

Enzi zetu ukijaribu kuwasha taa wakati wa dinner (the great dinner) basi kesho lazima kiitwe kikao cha wazee na usipokuwa makini mama anaweza kuomba talaka....Tuliamini kwamba ni kahaba tu anatakiwa kuchezewe hata kama jua linatua utosini (12.00 noon)!!

Na hata kama hujashiba ....wewe unashukuru tu na kutegea kesho ije na mema zaidi!!

Bado siafiki hata diclosure ya 50%........Nadhani usanii zaidi unalipa!
 
Waongelee kidogo tu (siyo upendeleo) ili wasidhani kwamba unawatenga na kupendelea hawa wajukuu wa dot com peke yao.

Hivi kwa hayo uliyosema, unaweza kutuelezea ni asilimia ngapi walau tuziweke wazi??

Babu nadhani niliyosema mwanzo hata kwao yanaAPPLY vile vile.

Kuhusu asilimia ngapi isemwe siwezi kusema kwasababu inategemea kati ya mtu na mtu.Kuna watu ambao past zao zinazoweza kuhusika/hitaji nafasi kwenye mahusiano yao ni kubwa wakati wengine ni kidogo sana. Hivyo anaweza pata asilimia gani aseme baada yakupitia yale anayoona ni muhimu kujulisha pamoja na yake anayoona hayana ulazima. Mwisho wa siku wapo wanaosema kila kitu (muhimu or not) kitu ambacho ni kizuri maana hapo unakua umempa mwenzako hata yale unayoamini sio muhimu kumbe kwake ni muhimu kufahamu, na wapo wale wanaoficha mengi na kutoa kidogo. Msome mwenzako kujua kiasi gani cha ukweli anahitaji....nakama kitu ni kigumu kusema waweza kukiacha na kukivutia muda badala ya kudanganya moja kwa moja.
 
Mimi bana nachagua la kuongea na kuweka wazi!

Malavidavi - hapa natumia trick kumuimprove lakini never kumwambia kwamba ex alikuwa bomba kuliko wewe, DNA za kinamama zinapenda kusifiwa tu aisee.

Mshahara: Hii ni siri ya serikali, mwanamke ukimueleza mshahara wa kweli mara hela ya mboga unaskia kaenda kuinunulia wigi na meno ya bandia.

mambo ya familia: hapa nitamwaga mboga zote, nitamjulisha kakaangu gani ni kibaka, mjombaangu gani ni mpiga chabo, mpwa wangu gani ana busha, na nani ascheke cheke nae ovyo nakazalika.

Nitaendelea post ijayo
 
Dark City kwa dunia ya sasa hata ukificha kuna uwezekano mkubwa ubani wako kujua kama akitaka. Hizi wikileaks nasikia zimeanza kujikita hata uswahilini pia.
 
Sawa kabisa,

Sasa tupe practical picture..were umeweka hewani asilimia ngapi???
 
Sidhani kama tunatakiwa kuwa na wasi wasi na hizo cable zao...Wikiliki ikikulipukia unaikana na macho maangavu kabisa kama panya kanaswa na mtego.

Kwani hukuona ya akina Salva mtoto wa Rweyemamu na boss wake???

Halafu sasa huku kwetu uswahilini watu wameanza kudharau hizo cables kwamba ni mtandao wa umbeya tu!!
 
Mimi bana nachagua la kuongea na kuweka wazi!

Malavidavi - hapa natumia trick kumuimprove lakini never kumwambia kwamba ex alikuwa bomba kuliko wewe, DNA za kinamama zinapenda kusifiwa tu aisee.

Mshahara: Hii ni siri ya serikali, mwanamke ukimueleza mshahara wa kweli mara hela ya mboga unaskia kaenda kuinunulia wigi na meno ya bandia.

mambo ya familia: hapa nitamwaga mboga zote, nitamjulisha kakaangu gani ni kibaka, mjombaangu gani ni mpiga chabo, mpwa wangu gani ana busha, na nani ascheke cheke nae ovyo nakazalika.

Nitaendelea post ijayo

Haya bwana....wewe ni balaa!!

Yaani ukianza kuongea naamini hata shetani anafungua masikio yanakuwa kama mabawa ya penguin!!

Nasubiri part 2.....Ngoja nikajaze upepo kwenye mbavu zangu!!
 
Duuuuhhhh,

Kweli maendeleo yameshafika mbali...Hivi kweli sijaachwa...

Enzi zetu ukijaribu kuwasha taa wakati wa dinner (the great dinner) basi kesho lazima kiitwe kikao cha wazee na usipokuwa makini mama anaweza kuomba talaka....Tuliamini kwamba ni kahaba tu anatakiwa kuchezewe hata kama jua linatua utosini (12.00 noon)!!

Na hata kama hujashiba ....wewe unashukuru tu na kutegea kesho ije na mema zaidi!!

Bado siafiki hata diclosure ya 50%........Nadhani usanii zaidi unalipa!

aaaisee! Hii post ina insight ya kufa mtu kwa ADI... Na kufanya tu nivunje mbavu...

Hapo kwenye Red... yaani hilo tendo na nguo??
 
ADii,

Unajua enzi zetu na kwa wale waliopata bahati ya kuwa na babu/bibi, ilikuwa lazima kuota moto kila jioni,

Uzuri wake ulikuwa ndo huo.....mnajaribu kujipa confusion kwa kuchanganya mawazo yanayotoka kwenye generations zinazotofautiana kwa zaidi ya miaka 40!!

Hivi siku hizi bado mnaota moto kweli???
 
Nilipo kuna baridi... Hivo nimehakikisha nina heater.... Hio si nayo kuota moto?? (alafu umenipoteza.. whats it with tendo lenyewe na kuota moto)
 
Sawa kabisa,

Sasa tupe practical picture..were umeweka hewani asilimia ngapi???

Hahahahah...Babu bwana..!Kwahiyo kumbe nia yako ni watu wajilipue hapa?

Well kwa sasa hivi 0% kwasababu sijahitaji kufanya hivyo. Ila nikiangalia huko nyuma ukweli ni kwamba niko very selective kuhusu watu nnaofunguka kwao. Kama sijapata ile connection ya kunishawishi/nifanya nitamani kumwambia mpenzi/mtarajiwa mambo yangu bila kuchagua basi naangalia machache tu (siwezi kuweka asilimia maana hii inategemea na huyo mtu ila yaweza kuaanzia 10% na kuendelea) nnayoona ni muhimu huku nikitumaini kwamba kadiri muda unavyoenda nitafunguka zaidi.
 
Dark City kwa dunia ya sasa hata ukificha kuna uwezekano mkubwa ubani wako kujua kama akitaka. Hizi wikileaks nasikia zimeanza kujikita hata uswahilini pia.

Yapo ya kujulikana but mengine once buried... buried for good.
 
Back
Top Bottom