VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Mambo yameanza kunoga. Deusdedith Kakoko wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ametiwa nguvuni na yuko chini ya TAKUKURU kwa mahojiano na uchunguzi. Sote tunajua kuwa Mwendazake alikuwa akimwamini na kumtetea sana Kakoko. Alikuwa akimsifu na kumpa 'sapoti' ya kutosha na kutisha. Rangi halisi ya Kakoko wa Bandari imeanza kuonekana. Rangi ya kutisha, ufisadi wa kutisha.
Kakoko alikuwa Mungumtu pale Bandari. Amewachafua na kuwafukuza wote waliokuwa na uwezo wa kikazi kuliko yeye waliokuwa Mameneja wa Bandari katika mikoa mbalimbali hapa Tanzania. Mfano ni Bwana Salama aliyekuwa Meneja wa Bandari kule Kigoma. Alimchafua na kumfukuza kazi pamoja na ufanyakazi wake uliotukuka ulioongeza hata faida na kuimarisha Bandari ya Kigoma. Kwasasa Bwana Salama anapambana na kesi yake Tume ya Utumishi.
Kakoko ni mfano tu ya waliojificha kwenye kuaminiwa na Mwendazake na kufanya ufisadi/wizi/dhulma kubwa. Muda wa kuwashughulikia umefika. Muda wa kuwachunguza umewadia. Muda wa kuchoma kichaka chao ni huu. Wamefanya mengi sana mabaya kuzihusu fedha za umma na fedha za watu binafsi. Wametesa watumishi na wananchi wa kawaida. Nawataja baadhi: Makonda, Sabaya, Chalamila na Dotto James.
Kuaminiwa na Mwendazake kulikuwa ndiyo kisingizio chao. Nasema hivi, wale wote waliokuwa wakiaminiwa sana na Mwendazake wachunguzwe. TAKUKURU tafadhalini wasaidieni watanzania kujua ukweli kuwahusu hao na wengine watakaotajwa na wananchi. Tunahitaji kusafisha nchi yetu ili tusonge mbele bila kelele. Mafisadi washughulikiwe kwa kuonekana. Mafisadi wawajibike.
Propaganda na uongo ndizo zilizokuwa nguzo za Serikali ya Mwendazake!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)