mchillo
JF-Expert Member
- Oct 13, 2010
- 500
- 224
We ni kilaza uliyetumwa na Makamba au Kikwete. Mbona hujatuambia ni wajumbe wangapi walioshiriki kupiga kura za kumchagua huyo meya wenu wa kubumba? Quorum ilikuwa ya wajumbe wangapi? na kwa nini wajumbe wa CHADEMA wanaokaribia nusu ya wajumbe wote hawakushirikishwa katika zoezi hilo? Hoja zako zinaashiria wewe hutumii mfumo wa akili za kawaida kufikiri, labda kipo kiungo kingine unachotumia; bila shaka tumbo kama ilivyo kwa mafisadi wenzako wengine! Tunataka uongee facts na si pumba zilizooza kama ulivyofanya. Shame be unto you and your CCM. Mungu ibariki Tanzania.Wana JF najua ni wengi wanajiuliza maswali mengi juu ya uhalali wa uchaguzi wa meya wa jiji la Arusha ambao umekuwa mjadala mpaka leo. Swali wengi wanalojiuliza je uchaguzi ulikuwa halali au si halali?
Nataka niweke wazi uchaguzi ule ulikuwa halali kabisa na taratibu zilifuatwa kabisa. Kabla ya uchaguzi kufanyika kulikuwa na utata wa mjumbe mmoja wa CCM Mary Chitanda kupiga kura kwa sababu yeye si mwakilishi wa mkoa wa Arusha. Yeye ni katibu wa CCM mkoa wa Arusha lakini kwa sasa yeye ni mbunge wa viti maalum mkoani Tanga. CCM ilikuwa na wajumbe 15 ie madiwani na huyo mwenye utata 1 jumla ni 16. CDM ilikuwa na wajumbe 14 pamoja na G. Lema mbunge.
Utata huu ulipelekea kuomba ufafanuzi, na ufafanuzi ulipatikana kuwa mjumbe yule yaani Mary Chitanda alikuwa halali kwa maandishi na siyo mdomo kwa vyama vyote, hiyo ilikuwa siku ya pili baada ya kuahirisha uchaguzi jana yake.
Hilo ndiyo jambo kuu lilikuwa likibishaniwa. Sasa endapo jambo hili lilipatiwa ufumbuzi kwa maandishi inakuwaje leo hii viongozi wa CDM waendeleze malumbano jukwaani?
Ni jambo lisilofichika kwa nini Mary Chitanda asiende kupiga kura Tanga badala yake Arusha. Hilo ndilo suala la msingi kabisa lakini majibu yake vile vile kisheria hakuna kipengele kinachomkataza kupiga kura kwani bado ni kiongozi wa wanaCCM Arusha, na kuzingatia sheria haimbani CCM wakaonelea basi ni vema wakaitumia loopwhole hiyo.
Tuachane na ubishi kama sheria haimkabi basi CDM hawana haja ya malumbano. Machoni pa watu itaonekana si halali lakini mbele ya sheria inaonekana sawa. Katika uchaguzi wa urais hakuna mahakama yenye uwezo wa kutengua mara baada ya matokeo kutangazwa na tume ya uchaguzi. Hapa tunajifunza mapungufu ya sheria zetu za bongo. Hili ni jambo lisilopingika kabisa na kwa hili linahitaji mabadiliko.
Uchaaguzi umekwisha na meya keshapatikana sasa kama sheria zilikikwa basi tukapate haki yetu mahakamani na siyo kwa mashinikizo ya jukwaani.
CDM ni chama makini lakini kimepotoka kwa hili kwa ndiyo maana yake hawataki kwenda mahakamani kwa sababu wanajua hawana jipya. Kinachofanyika saizi ni propaganga ya sintofahamu ya tukio hili kwa wananchi!
Ni kweli mara baada ya kupewa taarifa ya uhalali wa Mary Chitanda CDM walitoka nje kujadili wakawaacha wajumbe wengine 17 wakiwa ndani na kipindi hicho walishasaini tayari column ya mahudhurio! Ilipoonekana wamechelewa kurudi CCM hapo ndipo walipocheza rafu kwa kuendesha uchaguzi kwani tayari walikuwa na sababu zote za kushinda kesi. Sijui ni daftari au niiteje umesaini, kisha umetoka nje kujadili basi jamaa wakaendelea ndani na uchaguzi. CDM walishituka pindi matokeo yanatangazwa na kuja ukumbini wakiongozwa na mbunge wao Lema wakaambiwa nyie si MMESUSIA uchaguzi basi endeleeni ila viongozi wamepatikana.
Huo ndiyo ukweli wa uchaguzi wa meya Arusha.
Kwa kuwa ukweli huu umejificha kauli nyingi za kulaani zilitokea na kuzidi hasa baada ya maandamano kuzuiliwa na kupeleka vifo.
Kauli za kiburi toka kwa viongozi wa CCM akiwemo Makamba zikaamsha hisia kali. CCM ni kama walikuwa wanawakebehi CDM kwa sababu walijua hawana pa kushika mahakamani na ndiyo maana wanawashinikiza viongozi wa CDM waande huko ili haki ijulikane.
Usichokijua ni hiki, kwa nini wasiende mahakamani wafungue kesi kisha waitishe maandamano ili kushinikiza haki ya kusikilizwa kesi upesi. Kukataa kwao kwa kisingizio mahakama haitatenda haki kunatilisha mashaka na waelewe kuwa mashinikizo yao hayana direct impact badala yake yanawapa changamoto viongozi wa CCM.
Mwisho naalani kwa kauli moja kuwa nguvu iliyotumika kuzima maandamano yale ilikuwa kubwa mno na viongozi wetu wa serikali waache kutumika kisiasa. La Arusha latosha kuwa funzo.
Kikwete zlisema tukio la Arusha ndiyo mwanzo na mwisho naomba iwe kweli ingawaje nasikia Mbeya vijana wake wamekwisha ua tena!!!
MD usiichangane na thread yoyote ile, iweke ili watu wajue na ku challange pale wanapoona siyo sahihi.