Ukweli usiopingika: CHADEMA ndicho chama kinachozuia Upinzani kuingia Ikulu. Watanzania tujitathmini kabla ya 2025

Kwa sasa bado ni hitaji letu sisi wanachama wa chadema, msitupangie kabísa ... Siku ccm ikiondoka madarakani ndo cku na huku mbowe ataachia uenyekiti... Msitupangie na wala msitulazimishe
hitaji lako wewe
 
Habari JF,

Kuna kitu hakiko sawa katika siasa za Tanzania. Kama ilivyo kwa viongozi na wanachama wakongwe wa vyama vya upinzani wengi wao walitoka CCM.

Kwa kipindi hicho kuunda kwao vyama vya siasa ilikuwa ni kuhakikisha kuna mfumo wa vyama vingi na SIO KUCHUKUA NCHI, hivyo viongozi hao walikuwa wanajua fika wanaingia kwenye uchaguzi lakini mshindi ni CCM.

Mfano mzuri kina Mzee Mrema, Mbowe na wengine wengi waliingia kwenye huu mfumo kuhakikisha Tanzania inakuwa na mfumo wa vyama vingi kama matakwa ya nje ili tuweze kusaidiwa.

CHADEMA haina ubishi ndio chama kikuu cha upinzani, wananchi wengi tunaimani nacho lakini je kinaweza kuingia Madarakani kwa Mwenyekiti Mbowe ambae anajua fika lengo lilikuwa ni kuhakikisha kunakuwa na vyama vya upinzani na sio kuingia madarakani?

Kila Uchaguzi CHADEMA wanasimamisha mgombea Urais lakini kiuhalisia Mwenyekiti anajua nini kitatokea .

Tume Huru kwa Huu upinzani wenye mamluki Itasaidia nini? Kwanini kina Mnyika ,Heche ,Tundu lissu,Lema ,Msigwa na wajumbe wengine..msifanye jambo Chama kiwe Imara?

Je, kuelekea 2025 tuendelee kuwaamini CHADEMA ya Aina hii? Najua kwenye ubunge upinzania utashinda sana vijana jipangeni.
Well, hapa kiuhalisia mbowe ndio humtaki! Bas saw
 
CCM mnamuogopa sana eeeh? Kwnn mnataka mbowe aondoke kwenye uenyekiti? Mnajifanya mna huruma na chadema saaaana kumbe mbowe ni kikwazo kwenu ktk kuisambaratisha chadema eeeh. Mlifanikiwa kuisambaratisha NCCR Mageuzi kwa kuwa haikuwa na mkiti strong, ikazaliwa TLP ambayo ilikuwa ni CCM B kwa 100%

Bado NCCR Mageuzi ikajikongoja weee lkn mkaona haitoshi mkawaalika wahuni na hatimaye imesambaratika mazima sasa mkaenda CUF, hatimaye nayo iko hoi bin taabani. ACT Wazalendo iko chini yenu vzr kbs. Siku ikifika Mhe Mbowe atakaa pembeni lkn sio kwa kutushinikiza.
wana mbinu nyingi sana
 
Nje ya chadema hakuna chama pinzani ...na hilo mnalijua
Kwani chamadema kinafanyaje kinachofanya uone kuwa ndio chama cha kweli cha upinzani?nakumbuka Lissu aliwahi kusema ACT hakijawahi kuwa chama cha upinzani ila baadaye ACT na Chadema wakajakuungana na kusimamisha mgombea mmoja.

Chadema ndio imekuwa hivyo miaka kusema vyama wenzie kuwa sio vyama vya upinzani na ni tokea zamani hiyo tabia.
 
Tanzania hakuna chama madhubuti cha upinzani cdm ni wapiga dili tu.
CCM wabaki tu madarakani muhimu wajisahihishe walipokosea.
 
  • Thanks
Reactions: RNA
CCM mnamuogopa sana eeeh? Kwnn mnataka mbowe aondoke kwenye uenyekiti? Mnajifanya mna huruma na chadema saaaana kumbe mbowe ni kikwazo kwenu ktk kuisambaratisha chadema eeeh. Mlifanikiwa kuisambaratisha NCCR Mageuzi kwa kuwa haikuwa na mkiti strong, ikazaliwa TLP ambayo ilikuwa ni CCM B kwa 100%

Bado NCCR Mageuzi ikajikongoja weee lkn mkaona haitoshi mkawaalika wahuni na hatimaye imesambaratika mazima sasa mkaenda CUF, hatimaye nayo iko hoi bin taabani. ACT Wazalendo iko chini yenu vzr kbs. Siku ikifika Mhe Mbowe atakaa pembeni lkn sio kwa kutushinikiza.
Mnaambiwa ukweli mnaanza kuleta mapenzi badala ya siasa ,mtakapotambua kuwa mbowe ni pandikizi ndipo mtakuwa mmejielewa
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Mlifanikiwa kuisambaratisha NCCR Mageuzi kwa kuwa haikuwa na mkiti strong, ikazaliwa TLP ambayo ilikuwa ni CCM B kwa 100%

Bado NCCR Mageuzi ikajikongoja weee lkn mkaona haitoshi mkawaalika wahuni na hatimaye imesambaratika mazima sasa mkaenda CUF, hatimaye nayo iko hoi bin taabani. ACT Wazalendo iko chini yenu vzr kbs. Siku ikifika Mhe Mbowe atakaa pembeni lkn sio kwa kutushinikiza.
Kuuumbeee!!!!!
 
Kwani chamadema kinafanyaje kinachofanya uone kuwa ndio chama cha kweli cha upinzani?nakumbuka Lissu aliwahi kusema ACT hakijawahi kuwa chama cha upinzani ila baadaye ACT na Chadema wakajakuungana na kusimamisha mgombea mmoja.

Chadema ndio imekuwa hivyo miaka kusema vyama wenzie kuwa sio vyama vya upinzani na ni tokea zamani hiyo tabia.
Hatujawahi kuungana na Act
 
Watashindaje CDM na kuingia ikulu kwa katiba na Tume hii kweli, haiwezekani hata kwa mijeredi. Sawa na ngamia kuingia kwenye tundu la sindano.
 
Habari JF,

Kuna kitu hakiko sawa katika siasa za Tanzania. Kama ilivyo kwa viongozi na wanachama wakongwe wa vyama vya upinzani wengi wao walitoka CCM.

Kwa kipindi hicho kuunda kwao vyama vya siasa ilikuwa ni kuhakikisha kuna mfumo wa vyama vingi na SIO KUCHUKUA NCHI, hivyo viongozi hao walikuwa wanajua fika wanaingia kwenye uchaguzi lakini mshindi ni CCM.

Mfano mzuri kina Mzee Mrema, Mbowe na wengine wengi waliingia kwenye huu mfumo kuhakikisha Tanzania inakuwa na mfumo wa vyama vingi kama matakwa ya nje ili tuweze kusaidiwa.

CHADEMA haina ubishi ndio chama kikuu cha upinzani, wananchi wengi tunaimani nacho lakini je kinaweza kuingia Madarakani kwa Mwenyekiti Mbowe ambae anajua fika lengo lilikuwa ni kuhakikisha kunakuwa na vyama vya upinzani na sio kuingia madarakani?

Kila Uchaguzi CHADEMA wanasimamisha mgombea Urais lakini kiuhalisia Mwenyekiti anajua nini kitatokea .

Tume Huru kwa Huu upinzani wenye mamluki Itasaidia nini? Kwanini kina Mnyika ,Heche ,Tundu lissu,Lema ,Msigwa na wajumbe wengine..msifanye jambo Chama kiwe Imara?

Je, kuelekea 2025 tuendelee kuwaamini CHADEMA ya Aina hii? Najua kwenye ubunge upinzania utashinda sana vijana jipangeni.
Ngoja nisome comments

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom