Ukweli usiopingika: CHADEMA ndicho chama kinachozuia Upinzani kuingia Ikulu. Watanzania tujitathmini kabla ya 2025

Habari JF,

Kuna kitu hakiko sawa katika siasa za Tanzania. Kama ilivyo kwa viongozi na wanachama wakongwe wa vyama vya upinzani wengi wao walitoka CCM.

Kwa kipindi hicho kuunda kwao vyama vya siasa ilikuwa ni kuhakikisha kuna mfumo wa vyama vingi na SIO KUCHUKUA NCHI, hivyo viongozi hao walikuwa wanajua fika wanaingia kwenye uchaguzi lakini mshindi ni CCM.

Mfano mzuri kina Mzee Mrema, Mbowe na wengine wengi waliingia kwenye huu mfumo kuhakikisha Tanzania inakuwa na mfumo wa vyama vingi kama matakwa ya nje ili tuweze kusaidiwa.

CHADEMA haina ubishi ndio chama kikuu cha upinzani, wananchi wengi tunaimani nacho lakini je kinaweza kuingia Madarakani kwa Mwenyekiti Mbowe ambae anajua fika lengo lilikuwa ni kuhakikisha kunakuwa na vyama vya upinzani na sio kuingia madarakani?

Kila Uchaguzi CHADEMA wanasimamisha mgombea Urais lakini kiuhalisia Mwenyekiti anajua nini kitatokea .

Tume Huru kwa Huu upinzani wenye mamluki Itasaidia nini? Kwanini kina Mnyika ,Heche ,Tundu lissu,Lema ,Msigwa na wajumbe wengine..msifanye jambo Chama kiwe Imara?

Je, kuelekea 2025 tuendelee kuwaamini CHADEMA ya Aina hii? Najua kwenye ubunge upinzania utashinda sana vijana jipangeni.
Acheni upuuzi mnawaumiza wanyonge kwa siasa za kishenzi na kibinafsi. Watu wengi wanateseka na kufa kwa wewe kuendelea kuitetea CCM na udhalimu wao wa miaka mingi. Utajibu hilo siku moja mbele ya Mungu!
 
Back
Top Bottom