UKWELI USIOHITAJI UNAZI WA CHAMA

NKWENYE

Member
Feb 19, 2017
55
177
Ndugu wanabodi poleni na mihangaiko ya kujipatia kipato(kwa wale mnaotafuta kipato) poleni pia wote mliomaliza vyuo mbali mbali mkisubiri ajira na serikali haina mpango nanyi. Poleni nyooote kwa hali zenu

Kwa muda wa Wiki kadhaa sasa kumekuwepo na mambo mengi yanayoendelea hapa nchini kwetu.mojawapo ilikuwa ni masuala ya bunge huko Dodoma ambako bajeti ya nchi ilikuwa ikijadiliwa, huko kuna mengi ya akina mdee na wenzake (wabunge wasiopendwa na spika), kulikuwa na misiba ya hapa na pale akiwemo mwanasiasa maarufu NDESA.
lakini kubwa kuliko yote ni suala la MADINI YA TZ .

suala la usafirishaji wa kinachoitwa mchanga wa madini limekuwa ajenda kubwa sana. Kila mtu amekuwa akisema yake ila kubwa ni kuibuka kwa pande mbili zenye mtazamo tofauti.

Kundi la kwanza ni lile lililokuwa upande wa Rais kwa kuona namna anavyojitosa ktk kina cha maji marefu kutetea watanzania na mali zao dhidi ya "WEZI WALIOIDHINISHWA KUIBA " kuziiba.

Kundi la pili ni lile lililokuwa likikosoa style ya ujirushaji katika wa mheshimiwa Rais kuwa unaweza kuwa na kasoro kadhaa hata kama ana lengo la kuokoa wafa maji.

UKWELI USIOPASWA KUPINGWA NA MTU MWENYE AKILI TIMAMU

1: Nia ya Rais juu ya rasilimali za nchi ziko sawa na zinapaswa ziungwe mkono kwa juhudi zote

2:Tukubali kuwa pamoja na nia njema ya Rais, yapo mambo ambayo hawezi kukwepa kushauriwa. Mfano mikataba ya kisheria na mengine

3:Njia za kumshauri Rais siyo lazima kukaa nae meza moja kule magogoni, wapo wasioweza kumfikia kwa sbb mbalimbali. Wanaweza kumshauri hata kwa kupitia vyombo vya habari

4:Njia mojawapo nzuri ya kushauri ni KUKOSOA hasa kwenye nchi zenye demokrasia. Kukosolewa kusiitwe kuropoka bali mtazamo tofauti.

5: Kwa pamoja lazima tukubali kuwa SERIKALI YETU YA CHAMA CHA MAPINDUZI NDIYO IMESHUGULIKIA MASUALA YOTE YA MADINI, hivyo UCHAFU wote unaojitokeza wameuweka wao. Wasitafute ALIYETUROGA.

6: Tukubali kuwa AKINA TUNDU LISSU WANAPASWA KUPONGEZWA KWA KUIONESHA SERIKALI NJIA SAHIHI YA KUPITA hasa lile la kuiomba serikali ifuate sheria juu ya masuala ya madini ikiwemo kuleta sheria bungeni zifanyiwe marekebisho. TUNDU LISSU NI BORA KWA WATANZANIA KULIKO WALE WALIOJIFUNGIA OFISINI NA KUSAINI MIKATABA MIBOVU. NI BORA KULIKO WALIOLETA MIKATABA YA GESI KWA DHARURA BUNGENI.

mwisho tuwaombee wote wenye nia njema na nchi hii. Tuwakosoe wanaokosea lakini kubwa zaidi WABUNGE WA CCM wekeni maslahi ya nchi mbele kuliko kuwaza TEUZI ZA RAIS..


mwanachi wa kawaida kabisa.........
 
KWA HAYA MACHACHE TUNAPASWA KUMUUNGA MKONO RAISI.HAPA HAKUNA CHAMA BALI NI KWA AJILI YETU SOTE NA VIZAZI VIJAVYO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom